Nehemia 7 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Nehemia 7:1-73

17:1 1Nya 26:12-19; Neh 6:1; 8:9; Za 68:25Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 27:2 Neh 10:23; 2:8; Mit 26:24; 1Fal 18:37:2 Neh 7:3Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

(Ezra 2:1-70)

47:4 Mit 1:10; Neh 11:1Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 57:5 Mit 2:6; Rum 11:36; 1Kor 4:7; 2Kor 8:16; Yak 1:17; Ezr 2:1-70Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

67:6 Ezr 2:1-10; 2Nya 36:20Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 77:7 1Nya 3:19; Ezr 2:2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:

87:8 Ay 13:4; Dan 11:27wazao wa Paroshi 2,1729wazao wa Shefatia 37210wazao wa Ara 65211wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,81812wazao wa Elamu 1,25413wazao wa Zatu 84514wazao wa Zakai 76015wazao wa Binui 64816wazao wa Bebai 62817wazao wa Azgadi 2,32218wazao wa Adonikamu 66719wazao wa Bigwai 2,067207:20 Ezr 8:6wazao wa Adini 65521wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 9822wazao wa Hashumu 32823wazao wa Besai 32424wazao wa Harifu 11225wazao wa Gibeoni 95

267:26 2Sam 23:28; Mwa 35:6; Rut 2; 4watu wa Bethlehemu na Netofa 188277:27 Yos 21:18; Ezr 2:23watu wa Anathothi 12828watu wa Beth-Azmawethi 42297:29 Yos 18:25-26watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 74330watu wa Rama na Geba 621317:31 1Sam 13:2; Isa 10:27watu wa Mikmashi 122327:32 Mwa 12:8watu wa Betheli na Ai 12333watu wa Nebo 5234wazao wa Elamu 1,25435wazao wa Harimu 320367:36 Neh 3:2wazao wa Yeriko 345377:37 1Nya 8:12wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 72138wazao wa Senaa 3,930

397:39 1Nya 24:7Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973407:40 1Nya 24:14wazao wa Imeri 1,052417:41 1Nya 9:12; 24:9wazao wa Pashuri 1,247427:42 1Nya 24:8; Ezr 10:31wazao wa Harimu 1,017

43Walawi:

wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74

447:44 Neh 11:23Waimbaji:

wazao wa Asafu 148

457:45 1Nya 9:17Mabawabu wa malango:

wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138

467:46 Neh 3:26Watumishi wa Hekalu:7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

56wazao wa Nesia na Hatifa.

577:57 Mwa 9:25, 26; 1Fal 5:13, 14; 2Nya 2:17, 18Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,

58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.

607:60 1Nya 9:2Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

617:61 Ezr 2:59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

62wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642

637:63 2Sam 17:27; 19:31-34; 1Fal 2:7; Ezr 2:61Na kutoka miongoni mwa makuhani:

wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 657:65 Kut 28:30; Neh 8:9; Hes 7:89; 27:18-21Kwa hiyo, mtawala7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.

707:70 Neh 8:9; 10:1Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,0007:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. 717:71 1Nya 29:7; Ezr 2:69Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172. na mane 2,2007:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

727:72 Ay 34:10; Kut 25:2Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

737:73 Za 34:20; Neh 11:20; Kut 23:14-17; Law 23:24-44; Ezr 3:1Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezra Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,