Wakazi Wapya Wa Yerusalemu
111:1 Isa 48:2; Neh 7:4; Isa 64:10; Zek 14:20-21Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe. 211:2 Amu 5:9Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.
311:3 1Nya 9:29; Ezr 2:44-45Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu,11:3 Yaani Wanethini (pia 11:21). na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali, 411:4 Ezr 1:5; Mwa 38:29; Ezr 2:70; 1Nya 9:3ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).
Kutoka wazao wa Yuda:
Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi. 5Naye Maaseya mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, mzao wa Mshiloni. 6Wazao wa Peresi walioishi Yerusalemu walikuwa 468, watu wenye uwezo.
7Kutoka wazao wa Benyamini:
Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya 8na wafuasi wake, Gabai na Salai watu 928. 9Yoeli mwana wa Zikri alikuwa afisa wao mkuu, naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa msimamizi juu ya Mtaa wa Pili katika mji.
1011:10 1Nya 9:10Kutoka makuhani:
Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini, 1111:11 2Fal 25:18; Ezr 7:2Seraya mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi katika nyumba ya Mungu, 12pamoja na wenzao waliofanya kazi hekaluni: watu 822. Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amsi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya, 13na wenzao, waliokuwa viongozi wa jamaa: watu 242. Amashisai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri, 14na wenzao waliokuwa wenye uwezo: watu 128. Afisa wao mkuu alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.
15Kutoka Walawi:
Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni; 1611:16 Ezr 10:15; 2Nya 34:13; Ezr 8:33Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu; 1711:17 1Nya 9:15; Neh 12:8; 2Nya 5:12Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi; Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake; na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. 1811:18 Ufu 21:2; Ezr 9:8; Mt 24:15Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu 284.
1911:19 1Nya 9:17; Neh 7:45; 12:25Mabawabu:
Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: watu 172.
20Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.
2111:21 Ezr 2:43; Neh 3:26; 2Nya 27:3Watumishi wa Hekalu waliishi katika kilima cha Ofeli. Siha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.
2211:22 1Nya 9:15Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu. 2311:23 1Nya 15:16; Neh 7:44Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.
2411:24 Mwa 38:30; 1Nya 23:28Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.
2511:25 Mwa 35:27; Yos 14:15; Hes 21:30Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyokizunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake, 2611:26 Yos 15:27katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti, 2711:27 Mwa 21:14katika Hasar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake, 2811:28 Isa 27:6katika Siklagi, katika Mekona na makazi yake, 2911:29 Yos 15:33-35; Yer 10:3katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi, 3011:30 Yos 10:39; 10:10; 15:28Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.
3111:31 Yos 21:17; Isa 10:29; 1Sam 13:2Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake, 3211:32 Isa 10:30; 1Sam 21:1katika Anathothi, Nobu na Anania, 3311:33 Yos 11:1; 18:25; 2Sam 4:3katika Hazori, Rama na Gitaimu, 3411:34 1Sam 13:18katika Hadidi, Seboimu na Nebalati, 3511:35 1Nya 8:12; 4:14katika Lodi na Ono, na katika Bonde la Mafundi.
36Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.
住在耶路撒冷的人
1民眾的首領住在耶路撒冷。其餘的人用抽籤的方式抽出十分之一的人口住在聖城耶路撒冷,剩下的人則住在其他城邑。 2眾人為所有自願住在耶路撒冷的人祝福。
3-4以色列人、祭司、利未人、殿役和所羅門僕人的子孫住在猶大各城自己的家園,有些來自猶大和便雅憫的人住在耶路撒冷。以下是住在耶路撒冷的猶大省首領:
猶大人中有法勒斯的子孫、烏西雅的兒子亞他雅。烏西雅是撒迦利雅的兒子,撒迦利雅是亞瑪利雅的兒子,亞瑪利雅是示法提雅的兒子,示法提雅是瑪勒列的兒子。 5此外還有巴錄的兒子瑪西雅。巴錄是谷何西的兒子,谷何西是哈賽雅的兒子,哈賽雅是亞大雅的兒子,亞大雅是約雅立的兒子,約雅立是撒迦利雅的兒子,撒迦利雅是示羅尼的兒子。 6住在耶路撒冷的法勒斯的子孫共有四百六十八人,都是勇士。
7便雅憫人中有米書蘭的兒子撒路。米書蘭是約葉的兒子,約葉是毗大雅的兒子,毗大雅是歌賴雅的兒子,歌賴雅是瑪西雅的兒子,瑪西雅是以鐵的兒子,以鐵是耶篩亞的兒子。 8此外還有迦拜和撒來,共九百二十八人。 9細基利的兒子約珥是他們的監督,哈西努亞的兒子猶大是耶路撒冷的副官。
10祭司中有雅斤,約雅立的兒子耶大雅, 11以及管理上帝殿的西萊雅,他是希勒迦的兒子,希勒迦是米書蘭的兒子,米書蘭是撒督的兒子,撒督是米拉約的兒子,米拉約是亞希突的兒子; 12還有他們在殿裡供職的弟兄,共八百二十二人;還有耶羅罕的兒子亞大雅,耶羅罕是毗拉利的兒子,毗拉利是暗洗的兒子,暗洗是撒迦利亞的兒子,撒迦利亞是巴施戶珥的兒子,巴施戶珥是瑪基雅的兒子; 13還有他們做族長的弟兄,共二百四十二人;還有亞薩列的兒子亞瑪帥,亞薩列是亞哈賽的兒子,亞哈賽是米實利末的兒子,米實利末是音麥的兒子; 14還有他們英勇的弟兄,共一百二十八人。他們的監督是哈基多琳的兒子撒巴第業。
15利未人中有哈述的兒子示瑪雅。哈述是押利甘的兒子,押利甘是哈沙比雅的兒子,哈沙比雅是布尼的兒子。 16還有利未人的族長沙比太和約撒拔,他們負責上帝殿外面的事務。 17還有米迦的兒子瑪他尼,他是帶領禱告和讚美的。米迦是撒底的兒子,撒底是亞薩的兒子。還有他的助手瑪他尼的弟兄八布迦。此外,還有沙姆亞的兒子押大。沙姆亞是加拉的兒子,加拉是耶杜頓的兒子。 18在聖城的利未人共有二百八十四名。
19殿門守衛有亞谷和達們,還有他們做殿門守衛的弟兄,共一百七十二人。 20其他以色列人、祭司和利未人住在猶大各城自己的家園。 21殿役住在俄斐勒,他們的首領是西哈和基斯帕。
22在耶路撒冷的利未人的監督是巴尼的兒子烏西,巴尼是哈沙比雅的兒子,哈沙比雅是瑪他尼的兒子,瑪他尼是米迦的兒子。烏西是亞薩的子孫,亞薩的子孫是負責聖殿事務的歌樂手。 23歌樂手每天應盡的責任由王決定。 24猶大的兒子謝拉的子孫、米示薩別的兒子毗他希雅幫助王處理民眾的事務。
住在其他城邑的人
25至於村莊及其周圍的田地,一些猶大人住在基列·亞巴、底本、葉甲薛和它們周圍的村莊, 26耶書亞、摩拉大、伯·帕列、 27哈薩·書亞、別示巴和別示巴周圍的村莊, 28洗革拉、米哥拿和米哥拿周圍的村莊, 29音·臨門、瑣拉、耶末、 30撒挪亞、亞杜蘭和它們周圍的村莊,拉吉及其周圍的田地,亞西加及其周圍的村莊。他們居住的地方從別示巴一直延伸到欣嫩谷。
31便雅憫人住的地方由迦巴起直到密抹、亞雅、伯特利和伯特利周圍的村莊, 32亞拿突、挪伯、亞南雅、 33夏瑣、拉瑪、基他音、 34哈第、洗編、尼八拉、 35羅德、阿挪和匠人之谷。 36一些原本住在猶大的利未人被安頓在便雅憫。