Nahumu 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Nahumu 2:1-13

Ninawi Kuanguka

12:1 Yer 51:20Mshambuliaji anasogea dhidi yako, Ninawi.

Linda ngome,

chunga barabara,

jitieni nguvu wenyewe,

kusanya nguvu zako zote!

22:2 Eze 37:23; Isa 60:15Bwana atarudisha fahari ya Yakobo,

kama fahari ya Israeli,

ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa

na wameharibu mizabibu yao.

32:3 Eze 23:14-15Ngao za askari wake ni nyekundu,

mashujaa wamevaa nguo nyekundu.

Chuma kwenye magari ya vita chametameta,

katika siku aliyoyaweka tayari,

mikuki ya mierezi inametameta.

42:4 Yer 4:13; Eze 23:24Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani,

yakikimbia nyuma na mbele uwanjani.

Yanaonekana kama mienge ya moto;

yanakwenda kasi kama umeme.

52:5 Yer 46:12Anaita vikosi vilivyochaguliwa,

lakini bado wanajikwaa njiani.

Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji,

ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa.

62:6 Isa 45:1; Nah 3:13Malango ya mto yamefunguliwa wazi,

na jumba la kifalme limeanguka.

72:7 Mwa 8:8; Isa 59:11; 32:12Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe

na upelekwe uhamishoni.

Vijakazi wake wanaomboleza kama hua

na kupigapiga vifua vyao.

8Ninawi ni kama dimbwi,

nayo maji yake yanakauka.

Wanalia, “Simama! Simama!”

Lakini hakuna anayegeuka nyuma.

9Chukueni nyara za fedha!

Chukueni nyara za dhahabu!

Wingi wake hauna mwisho,

utajiri kutoka hazina zake zote!

102:10 Yos 2:11; 7:5; Isa 29:22Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi!

Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea,

miili inatetemeka,

na kila uso umebadilika rangi.

112:11 Isa 5:29Liko wapi sasa pango la simba,

mahali ambapo waliwalisha watoto wao,

ambapo simba dume na simba jike walikwenda

na ambapo wana simba walikwenda

bila kuogopa chochote?

122:12 Yer 51:34; 4:7; Isa 37:18Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake,

alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake,

akijaza makao yake kwa alivyoua

na mapango yake kwa mawindo.

132:13 Isa 10:5-13; Yer 21:13; Nah 3:5; Za 46:9; 2Sam 2:26; Mik 5:6Bwana Mwenye Nguvu Zote anatangaza,

“Mimi ni kinyume na ninyi.

Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto,

na upanga utakula wana simba wako.

Sitawaachia mawindo juu ya nchi.

Sauti za wajumbe wako

hazitasikika tena.”