Mwanzo 6 – NEN & NIRV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 6:1-22

Gharika Kuu

16:1 Mwa 1:28Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao, 26:2 Ay 1:6; 2:1; Kum 21:11; Mwa 4:19wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. 36:3 Ay 10:9; 34:14; Gal 5:15-17; Isa 40:6; 57:16; 1Pet 3:20; Za 78:39; 103:14Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”

46:4 Hes 13:33; Mwa 11:4Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.

56:5 Mwa 38:7; 8:21; Ay 34:26; Yer 1:16; 44:5; Eze 3:19; Za 14:1-3Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 66:6 Kut 32:14; 1Sam 15:11, 35; 2Sam 24:16; 1Nya 21:15; Isa 63:10; Efe 4:30; Yer 18:7-10Bwana akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko. 76:7 Eze 33:28; Sef 1:2, 18; Mwa 7:4, 21; Kut 28:36; 29:20Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” 86:8 Eze 14:14; Mwa 19:19; 39:4; Kut 33:12-17; 34:9; Hes 11:15; Rut 2:2; Lk 1:30; Mdo 7:46Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana.

96:9 Mwa 2:4; 5:22; 7:1; 17:1; Kum 18:13; 2Sam 22:24; Ay 1:1; 4:6; 9:21; 12:4; 31:6; Za 15:2; 18:23; 19:13; 37:37; Mit 2:7; Yer 15:1; Eze 14:14-20; Dan 10:11; Lk 1:6; Ebr 11:7; 2Pet 2:5Hivi ndivyo vizazi vya Noa.

Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. 106:10 Lk 3:36; Mwa 5:32Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

116:11 Kum 31:29; Amu 2:19; Za 73:6; Eze 7:23; 8:17; 28:16; Mal 2:16Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. 126:12 Kut 32:7; Kum 4:16; 9:12, 24; Za 14:1-3Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 136:13 Kum 28:63; 2Fal 8:19; Ezr 9:14; Yer 44:11, 27; Mwa 7:4, 21-23; Ay 34:15; Isa 5:6; 24:1-3; Eze 7:2-3Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. 146:14 Ebr 11:7; 1Pet 3:20; Kut 2:3Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135. upana wake dhiraa hamsini6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5. na kimo chake dhiraa thelathini.6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5. 16Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. 176:17 Za 29:10; 2Pet 2:5Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia. 186:18 Mwa 7:1, 7; 9:9-16; 17:7; 19:12; Kut 6:4; 34:10; Za 25:10; 74:20; 106:45; Eze 16:60; Kum 29:13-15; Isa 55:3; Hag 2:5; Yer 32:40; 1Pet 3:20Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao. 196:19 Mwa 7:15Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe. 206:20 Mwa 7:3, 15; 1:11Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai. 21Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”

226:22 Mwa 7:5; 9:16; Kut 7:6; 39:43; 40:16, 19, 21-32Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru.

New International Reader’s Version

Genesis 6:1-22

The Sins of Everyone on Earth

1There began to be many human beings on the earth. And daughters were born to them. 2The sons of God saw that the daughters of human beings were beautiful. So they married any of them they chose. 3Then the Lord said, “My Spirit will not struggle with human beings forever. They will have only 120 years to live.”

4The Nephilim were on the earth in those days. That was when the sons of God went to the daughters of human beings. Children were born to them. The Nephilim were famous heroes who lived long ago. Nephilim were also on the earth later on.

5The Lord saw how bad the sins of everyone on earth had become. They only thought about evil things. 6The Lord was very sad that he had made human beings on the earth. His heart was filled with pain. 7So the Lord said, “I created human beings, but I will wipe them out. I will also destroy the animals, the birds in the sky, and the creatures that move along the ground. I am very sad that I have made human beings.” 8But the Lord was very pleased with Noah.

Noah and the Flood

9Here is the story of Noah’s family line.

Noah was a godly man. He was without blame among the people of his time. He walked faithfully with God. 10Noah had three sons. Their names were Shem, Ham and Japheth.

11The earth was very sinful in God’s eyes. It was full of people who did mean and harmful things. 12God saw how sinful the earth had become. All its people were living very sinful lives. 13So God said to Noah, “I am going to put an end to everyone. They have filled the earth with their harmful acts. I am certainly going to destroy them and the earth. 14So make yourself an ark out of cypress wood. Make rooms in it. Cover it with tar inside and out. 15Here is how I want you to build it. The ark has to be 450 feet long. It has to be 75 feet wide and 45 feet high. 16Make a roof for it. Leave below the roof an opening all the way around that is a foot and a half high. Put a door in one side of the ark. Make lower, middle and upper decks. 17I am going to bring a flood on the earth. It will destroy all life under the sky. It will destroy every living creature that breathes. Everything on earth will die. 18But I will make my covenant with you. You will go into the ark. Your sons and your wife and your sons’ wives will enter it with you. 19Bring a male and a female of every living thing into the ark. They will be kept alive with you. 20Two of every kind of bird will come to you. Two of every kind of animal will also come to you. And so will two of every kind of creature that moves along the ground. All of them will be kept alive with you. 21Take every kind of food that you will need. Store it away as food for you and them.”

22Noah did everything just as God commanded him.