Mwanzo 50 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 50:1-26

1Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. 250:2 Mwa 50:26; 2Nya 16:14Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, 350:3 Kum 1:3; Mwa 30:27wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini.

450:4 Mwa 27:41Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, 550:5 Mwa 24:37; 2Sam 18:18‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ”

6Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.”

750:7 Mwa 45:16Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri. 8Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni. 950:9 Mwa 41:43Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana.

1050:10 Hes 15:20; 1Sam 31:13Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. 1150:11 Mwa 10:18; 37:34Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.50:11 Abel-Mizraimu maana yake Maombolezo ya Wamisri.

12Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza: 1350:13 Mwa 23:20Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Abrahamu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia. 14Baada ya Yosefu kumzika baba yake, akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wale wote waliokuwa wamekwenda naye kumzika baba yake.

Yosefu Awaondolea Ndugu Zake Mashaka

1550:15 Mwa 37:28Ndugu zake Yosefu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yosefu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” 16Kwa hiyo wakampelekea Yosefu ujumbe, wakasema, “Kabla baba yako hajafa aliacha maagizo haya: 1750:17 Mt 6:14; Mwa 29:11‘Hili ndilo mtakalomwambia Yosefu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako.” Ujumbe huu ulipomfikia, Yosefu akalia.

1850:18 Mwa 37:7Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.”

1950:19 Rum 12:19; Ebr 10:30Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? 2050:20 Rum 8:28; Mwa 45:5Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. 2150:21 Mwa 45:11; Efe 4:32Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawahakikishia na kusema nao kwa wema.

Kifo Cha Yosefu

2250:22 Mwa 25:7; Yos 24:29Yosefu akakaa katika nchi ya Misri, yeye pamoja na jamaa yote ya baba yake. Akaishi miaka 110, 23naye akaona kizazi cha tatu cha watoto wa Efraimu. Pia akaona watoto wa Makiri mwana wa Manase, wakawekwa magotini mwa Yosefu walipozaliwa.

2450:24 Rut 1:6; Za 35:2; Mwa 12:7Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.” 25Naye Yosefu akawaapisha wana wa Israeli na kuwaambia, “Hakika Mungu atawasaidia, nanyi ni lazima mhakikishe mmepandisha mifupa yangu kutoka mahali hapa.”

26Kwa hiyo Yosefu akafa akiwa na umri wa miaka 110. Baada ya kumtia dawa ili asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

創世記 50:1-26

安葬雅各

1約瑟伏在父親身上痛哭,親吻他, 2然後吩咐醫生用香料保存父親的遺體。醫生遵命而行, 3按照常例花了四十天用香料處理遺體。埃及人為他哀悼七十天。

4哀悼的日子完了,約瑟對法老宮中的人說:「如果你們恩待我, 5請告訴法老,我父親死前要我起誓把他葬在迦南他自己預備好的墳地。請准許我到迦南去安葬我父親,我辦完喪事就回來。」 6法老說:「去按照你的誓言埋葬你父親吧。」 7於是,約瑟啟程去埋葬他的父親,隨行的有法老所有的臣僕和埃及所有的達官顯貴, 8以及約瑟全家、他的眾弟兄和雅各的家眷,只有他們的孩子和牛羊仍然留在歌珊9隨行的還有大隊車輛和騎兵,人數眾多。 10他們來到約旦河附近的亞達麥場,在那裡痛哭哀悼。約瑟為父親哭喪七天。 11迦南人看見他們在亞達麥場痛哭,就說:「埃及人在痛哭哀悼。」因此,約旦河附近的那個地方叫亞伯·麥西50·11 「亞伯·麥西」意思是「埃及人在哀哭」。12雅各的兒子們遵照父親的遺言, 13把父親的遺體帶回迦南,安葬在幔利附近、麥比拉田間的洞裡。洞和田地都是亞伯拉罕以弗崙買來作墳地的。 14葬禮之後,約瑟就跟眾弟兄和一切隨行的人返回埃及

上帝的美好旨意

15約瑟的哥哥們見父親死了,就說:「約瑟會不會懷恨在心,因我們以前惡待他而報復我們呢?」 16於是,他們派人去對約瑟說:「你父親臨終時交待這樣的話給你, 17『從前你哥哥們惡待你,求你饒恕他們的罪惡和過犯。』我們是你父親的上帝的僕人,求你饒恕我們的罪惡。」約瑟聽見這些話,就哭了。 18約瑟的哥哥們來見他,俯伏在他面前,說:「我們是你的奴僕。」 19約瑟對他們說:「你們不要害怕,我豈能代替上帝? 20從前你們是要加害於我,但上帝有祂的美意,祂藉此保全許多人的性命,正如今日的光景。 21因此,你們不要害怕,我會照顧你們和你們的兒女。」約瑟好言好語地寬慰他們。

約瑟去世

22約瑟和他父親全家住在埃及約瑟享年一百一十歲。 23他看到了以法蓮的孫子,也曾把瑪拿西的兒子瑪吉剛出生的孩子抱在膝上。 24一天,約瑟對他的弟兄們說:「我快要死了,但上帝必看顧你們,帶你們離開這裡,回到祂起誓應許給亞伯拉罕以撒雅各的地方。」 25約瑟以色列的子孫起了誓,並說:「上帝必看顧你們,你們要把我的骸骨帶回迦南。」 26約瑟享年一百一十歲。他們把他的遺體用香料保存好,放在棺材裡,停放在埃及