Mwanzo 5 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 5:1-32

Kutoka Adamu Hadi Noa

(1 Nyakati 1:1-4)

15:1 Mwa 1:27; 2:4; 1Nya 1:1; Kol 3:10; Efe 4:24Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.

Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. 25:2 Mwa 1:27-28; Mt 19:4; Mk 10:6; Gal 3:28Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”

35:3 Mwa 1:26; 4:25; 1Kor 15:49; Lk 3:38Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. 4Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 55:5 Mwa 2:17; 3:19; Ebr 9:27Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.

65:6 Mwa 4:26; Lk 3:38Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. 7Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 8Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.

95:9 1Nya 1:2; Lk 3:37Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 11Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.

125:12 1Nya 1:2; Lk 3:37Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 14Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 17Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

185:18 1Nya 1:3; Lk 3:37; Yud 14Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki. 19Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 20Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

215:21 1Nya 1:3; Lk 3:37Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 225:22 Mwa 6:9; 17:1; 24:40; 48:15; 2Fal 20:3; Za 116:9; Mal 2:6; Mik 6:8Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 23Enoki aliishi jumla ya miaka 365. 245:24 2Fal 2:1, 11; Za 49:15; 73:24; 89:48; Ebr 11:5Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

255:25 1Nya 1:3; Lk 3:36Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki. 26Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 27Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.

28Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. 295:29 1Nya 1:3; Lk 3:36; Mwa 3:17; Rum 8:20Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.” 30Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 31Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

325:32 Mwa 7:6, 11; 8:13; 6:10; 9:18; 10:1; Lk 3:36; 1Nya 1:4; Isa 65:20Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.