Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 49:1-33

Yakobo Abariki Wanawe

149:1 Hes 24:14; Kum 31:29Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo.

249:2 Yos 24:1; Za 34:11“Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo,

msikilizeni baba yenu Israeli.

349:3 Mwa 29:32; Kum 21:17; Za 78:51“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza,

nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu,

umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.

4Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena,

kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako,

kwenye kitanda changu na kukinajisi.

549:5 Mwa 29:33; Mit 4:17“Simeoni na Lawi ni wana ndugu:

panga zao ni silaha za jeuri.

649:6 Mit 1:15; Efe 5:11Mimi na nisiingie katika baraza lao,

nami nisiunganike katika kusanyiko lao,

kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao,

walikata mishipa ya miguu ya mafahali

kama walivyopenda.

749:7 Yos 19:1, 9; Mwa 29:35Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno,

nayo ghadhabu yao ni ya ukatili!

Nitawatawanya katika Yakobo

Na kuwasambaza katika Israeli.

849:8 1Nya 5:2; Kum 28:48“Yuda, ndugu zako watakusifu;

mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako;

wana wa baba yako watakusujudia.

949:9 Hes 24:9; Ay 38:39Ee Yuda, wewe ni mwana simba;

unarudi toka mawindoni, mwanangu.

Kama simba hunyemelea na kulala chini,

kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?

1049:10 Eze 21:27; Isa 42:1Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda,

wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake,

hadi aje yeye ambaye milki ni yake,

ambaye utii wa mataifa ni wake.

11Atamfunga punda wake katika mzabibu,

naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi;

atafua mavazi yake katika divai,

majoho yake katika damu ya mizabibu.

12Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai,

meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

1349:13 Mwa 30:20; 10:19“Zabuloni ataishi pwani ya bahari

na kuwa bandari za kuegesha meli;

mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.

14“Isakari ni punda mwenye nguvu

ambaye amelala kati ya mizigo yake.

1549:15 Yos 19:17-23; Eze 29:18Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika

na jinsi nchi yake inavyopendeza,

atainamisha bega lake kwenye mzigo

na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.

16“Dani atahukumu watu wake kwa haki

kama mmoja wa makabila ya Israeli.

1749:17 Amu 18:27; Yer 8:17Dani atakuwa nyoka kando ya barabara,

nyoka mwenye sumu kando ya njia,

yule aumaye visigino vya farasi

ili yule ampandaye aanguke chali.

18“Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.

19“Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji,

lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa.

2049:20 Mwa 30:13; Isa 25:6; Ay 29:6“Chakula cha Asheri kitakuwa kinono,

naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme.

21“Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru

azaaye watoto wazuri.

2249:22 Mwa 30:24; Eze 19:10“Yosefu ni mzabibu uzaao,

mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi,

ambao matawi yake hutanda ukutani.

23Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia,

wakampiga mshale kwa ukatili.

2449:24 Za 18:34; Isa 1:24Lakini upinde wake ulibaki imara,

mikono yake ikatiwa nguvu,

na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,

kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,

2549:25 Kut 18:4; Mwa 27:28kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,

kwa sababu ya Mwenyezi,49:25 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. yeye anayekubariki

kwa baraka za mbinguni juu,

baraka za kilindi kilichoko chini,

baraka za matitini na za tumbo la uzazi.

26Baraka za baba yako ni kubwa

kuliko baraka za milima ya kale,

nyingi kuliko vilima vya kale.

Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,

juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.

2749:27 Amu 20:12-13; Ebr 1:8; Hes 31:11“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;

asubuhi hurarua mawindo yake,

jioni hugawa nyara.”

28Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.

Kifo Cha Yakobo

2949:29 Mwa 25:8; 2Sam 2:32Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, 30pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. 3149:31 Mwa 25:9; 23:19Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. 32Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”

3349:33 Mwa 25:8; Mdo 7:15Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 49:1-33

雅各的預言

1雅各把他的兒子們都叫來,對他們說:「你們到我身邊來,我要把你們將來的遭遇告訴你們。

2雅各的兒子們啊,

你們都來聽,

聽你們父親以色列的話。

3呂便啊,你是我的長子,

是我年輕力壯時生的,

比眾弟兄更有尊榮和力量。

4可是,你必不再居首位,

因為你放縱情慾,

如沸騰不止的水,

你上了你父親的床,

玷污了我的榻。

5西緬利未串通一氣,

依仗刀劍,殘暴不仁。

6我的靈啊,不要與他們同謀。

我的心啊,不要與他們聯合。

他們洩憤殺人,

隨意砍斷牛腿的筋。

7他們狂暴兇殘,該受咒詛!

我要使他們分散在雅各的子孫中,

散居在以色列各地。

8猶大啊,你的兄弟們必讚美你,

你必制伏你的仇敵,

你父親的兒子必向你下拜。

9我兒猶大是頭小獅子,

他獵食回來,躺臥如雄獅,

蹲伏如母獅,誰敢驚擾他?

10王權必不離猶大

御杖必伴他左右,

直到那位執掌王權的來到,

萬民都必歸順他。

11「他把小驢拴在葡萄樹旁,

把驢駒拴在上好的葡萄樹旁;

他在葡萄酒中洗衣服,

在葡萄汁中洗外袍。

12他的眼睛比酒烏潤,

牙齒比奶潔白。

13西布倫必安居在海濱,

成為泊船的港口,

他的疆界必伸展到西頓

14以薩迦是頭壯驢,

臥在羊圈中。

15他見那地方好作安身之處,

地土肥美,就垂下肩頭,

做了奴隸。

16必治理他的人民,

以色列的一個支派。

17他必成為路邊的蛇,

道旁的毒蛇,

咬傷馬蹄,使騎馬的人墜落。

18「耶和華啊,

我切切等候你的拯救。

19迦得必被強盜劫掠,

他卻要反敗為勝追趕他們。

20亞設必有豐美的出產和供君王享用的美味。

21拿弗他利是頭自由的母鹿,

養育美麗的小鹿49·21 養育美麗的小鹿」或譯「口出佳美之言」。

22約瑟是多結果子的枝條,

長在水泉旁,

他的枝條探出牆外。

23弓箭手兇猛地攻擊他,

惡狠狠地射他。

24但他手持強弓,

雙臂穩健有力,

因為雅各的大能者——以色列的牧者和磐石幫助他。

25你父親的上帝必幫助你,

全能者必賜你天上的恩澤、

地上的百福,

使你子孫興旺、牛羊滿圈。

26你父親的祝福高過亙古永存的峰巒,

多如綿延無盡的群山,

願這一切的祝福都臨到約瑟頭上,

臨到這超越眾弟兄的人身上。

27便雅憫是匹貪婪的狼,

早晨吞吃獵物,

晚上瓜分戰利品。」

28以上是以色列的十二支派,他們的父親按著他們不同的福分給他們祝福。 29雅各又囑咐他們說:「我要離世了,你們要把我葬在以弗崙田間的洞裡,讓我與祖先在一起。 30那洞穴在迦南幔利附近的麥比拉田間,是亞伯拉罕以弗崙買來作墳地的。 31亞伯拉罕和他的妻子撒拉以撒和他的妻子利百加都葬在那裡,我把利亞也葬在了那裡。 32那塊田和田間的洞穴是向人買的。」 33雅各囑咐完眾子,在床上躺下,嚥了氣,去他祖先那裡了。