Mwanzo 48 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 48:1-22

Manase Na Efraimu

148:1 Mwa 41:52; Ebr 11:2Baada ya muda Yosefu akaambiwa kwamba, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu, pamoja naye. 248:2 Mwa 48:8-9Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yosefu amekujia kukuona,” Israeli akakusanya nguvu zake, akaketi kitandani.

348:3 Mwa 17:1; 28:13Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezi48:3 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki, 448:4 Mwa 12:2; 15:7naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na kuongezeka hesabu yako, nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele wewe na wazao wako baada yako.’

548:5 Mwa 41:50-52; 29:32“Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa ni wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu. 6Lakini watoto utakaowazaa baada yao watakuwa wako. Katika nchi watakayoirithi, watatambuliwa kwa jina la ndugu zao. 748:7 Mwa 35:19; Rut 1:2Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu).

848:8 Mwa 48:2Wakati Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akauliza, “Hawa ni nani?”

948:9 Mwa 33:5; 24:60Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.”

Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.”

1048:10 Mwa 27:1; 29:13Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yosefu akawaleta wanawe karibu na baba yake, Israeli akawabusu na akawakumbatia.

1148:11 Mwa 44:28; 50:23Israeli akamwambia Yosefu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.”

12Ndipo Yosefu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli naye akasujudu hadi nchi. 1348:13 Za 16:8; Mt 25:33Yosefu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao. 14Lakini Israeli akaupeleka mkono wake wa kuume, akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa alikuwa ndiye mdogo, na mkono wake wa kushoto akaukatisha, akauweka juu ya kichwa cha Manase, ingawa Manase alikuwa ndiye mzaliwa wa kwanza.

15Ndipo akambariki Yosefu akisema,

“Mungu ambaye baba zangu

Abrahamu na Isaki walimtii,

Mungu ambaye amekuwa mchungaji

wa maisha yangu yote mpaka leo hii,

1648:16 Yer 15:21; Ebr 11:21Malaika ambaye aliniokoa kutoka madhara yote,

yeye na awabariki vijana hawa.

Na waitwe kwa jina langu

na kwa majina ya baba zangu Abrahamu na Isaki,

wao na waongezeke kwa wingi

katika dunia.”

1748:17 Mwa 48:14Yosefu alipoona baba yake akiweka mkono wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, hakupendezwa, kwa hiyo akauchukua mkono wa baba yake kutoka kichwa cha Efraimu na kuuweka juu ya kichwa cha Manase. 1848:18 Mwa 48:14Yosefu akamwambia, “Hapana, baba yangu, huyu ndiye mzaliwa wa kwanza; uweke mkono wako wa kuume juu ya kichwa chake.”

1948:19 Mwa 25:23; 12:2Lakini baba yake akakataa, akasema, “Ninajua, mwanangu, ninajua. Yeye pia atakuwa taifa, naye pia atakuwa mkuu. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, nao wazao wake watakuwa kundi la mataifa.” 2048:20 Mwa 24:60Akawabarikia siku ile na kusema,

“Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii:

‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ”

Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase.

2148:21 Mwa 26:3; 28:13Ndipo Israeli akamwambia Yosefu, “Mimi ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu. 2248:22 Yos 24:32; Yn 4:5Kwako wewe, kama aliye juu ya ndugu zako, ninakupa sehemu moja zaidi ya ndugu zako, lile eneo nililoteka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.”