Yakobo Aenda Misri
1Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake.
246:2 Mwa 15:1Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!”
Akajibu, “Mimi hapa.”
346:3 Mwa 12:2; 28:13Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. 446:4 Mwa 5:16Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.”
546:5 Mwa 45:19Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. 646:6 Kum 26:5; Mdo 7:15Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. 7Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri.
8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri:
Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.
9Wana wa Reubeni ni:
Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.
1046:10 Kut 6:15Wana wa Simeoni ni:
Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani.
11Wana wa Lawi ni:
Gershoni, Kohathi na Merari.
1246:12 1Nya 2:5; Mt 1:3Wana wa Yuda ni:
Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani).
Wana wa Peresi ni:
Hesroni na Hamuli.
13Wana wa Isakari ni:
Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.
1446:14 Mwa 30:20Wana wa Zabuloni ni:
Seredi, Eloni na Yaleeli.
1546:15 Mwa 30:21Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.
1646:16 Hes 26:15Wana wa Gadi ni:
Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.
1746:17 Mwa 30:13Wana wa Asheri ni:
Imna, Ishva, Ishvi na Beria.
Dada yao alikuwa Sera.
Wana wa Beria ni:
Heberi na Malkieli.
18Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita.
19Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni:
Yosefu na Benyamini. 2046:20 Mwa 41:51Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni,46:20 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu.
2146:21 1Nya 7:6-12Wana wa Benyamini ni:
Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi.
22Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne.
23Mwana wa Dani ni:
Hushimu.
2446:24 Mwa 30:8Wana wa Naftali ni:
Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu.
2546:25 Mwa 30:8Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba.
2646:26 Kut 1:5; Kum 10:22Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita. 2746:27 Mdo 7:14Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini.
2846:28 Mwa 45:10Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, 2946:29 Mwa 29:11gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.
3046:30 Mwa 44:28Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.”
3146:31 Mwa 45:10Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. 3246:32 Mwa 42:20Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’ 3346:33 Mwa 47:3Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ 3446:34 Mwa 43:32Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.”
以色列全家下埃及
1以色列带着他所有的一切来到别示巴,向他父亲以撒的上帝献祭。 2晚上,上帝在异象中对他说:“雅各!雅各!”他说:“我在这里。” 3上帝说:“我是上帝,是你父亲的上帝,不要害怕下到埃及,因为我要使你在那里成为大族。 4我必跟你一起下到埃及,也必带领你回来,约瑟必为你送终。”
5于是,雅各从别示巴启程。以色列的儿子们带着父亲和妻儿,乘坐法老送来的车, 6带着在迦南获得的牲畜和财物前往埃及。这样,雅各带着他所有的子孙, 7就是他的儿子、孙子、女儿和孙女一起去了埃及。
8以下是去埃及的以色列人,即雅各和他后代的名字。
雅各的长子是吕便, 9吕便的儿子是哈诺、法路、希斯伦和迦米。 10西缅的儿子是耶姆利、雅悯、阿辖、雅斤、琐辖和迦南女子生的扫罗。 11利未的儿子是革顺、哥辖和米拉利。 12犹大的儿子是珥、俄南、示拉、法勒斯和谢拉,珥和俄南死在了迦南,法勒斯的儿子是希斯伦和哈姆勒。 13以萨迦的儿子是陀拉、普瓦、约伯和伸仑。 14西布伦的儿子是西烈、以伦和雅利。 15这些都是利亚在巴旦·亚兰给雅各生的儿孙,加上女儿底娜共有三十三人。
16迦得的儿子是洗非芸、哈基、书尼、以斯本、以利、亚罗底和亚列利。 17亚设的儿子是音拿、亦施瓦、亦施韦、比利亚和他们的妹妹西拉,比利亚的儿子是希别和玛结。 18这些是悉帕给雅各生的儿孙,共有十六人,悉帕是拉班给女儿利亚的婢女。
19雅各的妻子拉结生的儿子是约瑟和便雅悯。 20约瑟在埃及生的儿子是玛拿西和以法莲,他们的母亲是安城祭司波提非拉的女儿亚西纳。 21便雅悯的儿子是比拉、比结、亚实别、基拉、乃幔、以希、罗实、姆平、户平和亚勒。 22这些是拉结给雅各生的儿孙,共有十四人。
23但的儿子是户伸。 24拿弗他利的儿子是雅薛、沽尼、耶色和示冷。 25这些是辟拉给雅各生的儿孙,共有七人,辟拉是拉班给女儿拉结的婢女。
26跟雅各一同到埃及去的儿孙共有六十六人,他的儿媳妇除外。 27加上约瑟在埃及生的两个儿子,雅各一家来到埃及的共有七十人。
28雅各派犹大先去见约瑟,请他派人引路到歌珊去。他们来到歌珊, 29约瑟备好车前去迎接父亲以色列。父子重逢,约瑟抱住父亲哭了很久。 30以色列对约瑟说:“我现在看到你还活着,就是死也安心了。”
31约瑟对他的弟兄们和其他家人说:“我要去告诉法老,你们已经从迦南来到我这里。 32你们是牧人,以畜牧为业,已经把羊群、牛群和所有的一切都带来了。 33等法老召见你们,问你们以什么为业, 34你们要说,‘仆人们跟我们的祖先一样,从小以畜牧为业。’这样,你们就可以住在歌珊,因为埃及人厌恶牧羊的。”