Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 42:1-38

Ndugu Za Yosefu Waenda Misri

142:1 Mdo 7:12Wakati Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka huko Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mnatazamana?” 242:2 Mwa 43:8Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Telemkeni huko mkanunue chakula kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi wala tusife.”

3Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakateremka huko Misri kununua nafaka. 442:4 Mwa 42:38Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yosefu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara. 542:5 Mdo 7:11Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale waliokwenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia.

642:6 Mwa 41:41Wakati huo Yosefu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yosefu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi. 7Mara Yosefu alipowaona ndugu zake, akawatambua, lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?”

Wakamjibu, “Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.”

8Ingawa Yosefu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua. 942:9 Mwa 37:7Ndipo Yosefu alipokumbuka ndoto zake kuwahusu wao, akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.”

10Wakamjibu, “Sivyo bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula. 11Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Watumishi wako ni watu waaminifu, wala sio wapelelezi.”

12Akawaambia, “La hasha! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.”

1342:13 Mwa 37:33Lakini wakamjibu, “Watumishi wako walikuwa kumi na wawili, wana wa mtu mmoja ambaye anaishi katika nchi ya Kanaani. Sasa mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu na mwingine alikufa.”

14Yosefu akawaambia, “Ni sawa kabisa kama nilivyowaambia: Ninyi ni wapelelezi! 1542:15 1Sam 17:55Na hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa mpaka ndugu yenu mdogo aje hapa. 1642:16 Mwa 42:11Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!” 1742:17 Mwa 40:4Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu.

1842:18 Law 25:43Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu: 19Ikiwa ninyi ni watu waaminifu, mmoja wa ndugu zenu na abaki kifungoni, nanyi wengine pelekeni nafaka kwa jamaa yenu wanaoteseka kwa njaa. 20Lakini ni lazima mniletee ndugu yenu mdogo hapa, ili maneno yenu yathibitike na kwamba msife.” Wakakubali kufanya hivyo.

2142:21 Mwa 45:5Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuponya maisha yake, lakini hatukumsikiliza, hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.”

2242:22 Mwa 9:5Reubeni akawajibu, “Sikuwaambieni msitende dhambi dhidi ya kijana? Lakini hamkunisikiliza! Sasa ni lazima tuadhibiwe kwa ajili ya damu yake.” 2342:23 Mwa 11:7Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani.

2442:24 Mwa 43:14, 23Yosefu akajitenga nao akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akataka Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao.

2542:25 Yer 40:5Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote, 26wakapakiza nafaka juu ya punda zao, wakaondoka.

2742:27 Isa 1:3Walipofika mahali pa kulala huko njiani mmoja wao akafungua gunia lake ili amlishe punda wake, akakuta fedha yake kwenye mdomo wa gunia lake. 2842:28 Mk 5:3Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.”

Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?”

2942:29 Mwa 44:24Walipofika kwa Yakobo baba yao katika nchi ya Kanaani, wakamweleza mambo yote yaliyowapata. Wakasema, 3042:30 Mwa 42:7“Huyo mtu ambaye ndiye bwana katika nchi hiyo alisema nasi kwa ukali, akatutendea kana kwamba sisi tulikuwa tunaipeleleza nchi. 31Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi. 32Tulizaliwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja. Mmoja alikufa, na mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu huko Kanaani.’

33“Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu pamoja nami hapa, kisha nendeni mpeleke chakula kwa ajili ya jamaa yenu inayoteseka kwa njaa. 3442:34 Mwa 34:10Lakini mleteni huyo ndugu yenu mdogo kwangu, ndipo nitajua kuwa ninyi sio wapelelezi, ila ni watu waaminifu. Kisha nitamrudisha ndugu yenu, nanyi mtaweza kufanya biashara katika nchi hii.’ ”

35Walipokuwa wanamimina nafaka kutoka kwenye magunia yao, ndani ya gunia la kila mtu kulikuwa na mfuko wa fedha! Wakati wao na baba yao walipoona mifuko ya fedha, wakaogopa. 3642:36 Mwa 42:24Yakobo baba yao akawaambia, “Ninyi mmenipokonya watoto wangu. Yosefu hayupo na Simeoni hayupo tena na sasa mnataka kumchukua Benyamini. Kila kitu ni kinyume nami!”

37Ndipo Reubeni akamwambia baba yake, “Waweza kuwaua wanangu wote wawili, ikiwa sitamrudisha Benyamini kwako. Mkabidhi Benyamini katika uangalizi wangu, nami nitamrudisha.”

3842:38 Mwa 37:33Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa naye ndiye peke yake aliyebaki. Ikiwa atapatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.”

New International Version – UK

Genesis 42:1-38

Joseph’s brothers go to Egypt

1When Jacob learned that there was grain in Egypt, he said to his sons, ‘Why do you just keep looking at each other?’ 2He continued, ‘I have heard that there is grain in Egypt. Go down there and buy some for us, so that we may live and not die.’

3Then ten of Joseph’s brothers went down to buy grain from Egypt. 4But Jacob did not send Benjamin, Joseph’s brother, with the others, because he was afraid that harm might come to him. 5So Israel’s sons were among those who went to buy grain, for there was famine in the land of Canaan also.

6Now Joseph was the governor of the land, the person who sold grain to all its people. So when Joseph’s brothers arrived, they bowed down to him with their faces to the ground. 7As soon as Joseph saw his brothers, he recognised them, but he pretended to be a stranger and spoke harshly to them. ‘Where do you come from?’ he asked.

‘From the land of Canaan,’ they replied, ‘to buy food.’

8Although Joseph recognised his brothers, they did not recognise him. 9Then he remembered his dreams about them and said to them, ‘You are spies! You have come to see where our land is unprotected.’

10‘No, my lord,’ they answered. ‘Your servants have come to buy food. 11We are all the sons of one man. Your servants are honest men, not spies.’

12‘No!’ he said to them. ‘You have come to see where our land is unprotected.’

13But they replied, ‘Your servants were twelve brothers, the sons of one man, who lives in the land of Canaan. The youngest is now with our father, and one is no more.’

14Joseph said to them, ‘It is just as I told you: you are spies! 15And this is how you will be tested: as surely as Pharaoh lives, you will not leave this place unless your youngest brother comes here. 16Send one of your number to get your brother; the rest of you will be kept in prison, so that your words may be tested to see if you are telling the truth. If you are not, then as surely as Pharaoh lives, you are spies!’ 17And he put them all in custody for three days.

18On the third day, Joseph said to them, ‘Do this and you will live, for I fear God: 19if you are honest men, let one of your brothers stay here in prison, while the rest of you go and take grain back for your starving households. 20But you must bring your youngest brother to me, so that your words may be verified and that you may not die.’ This they proceeded to do.

21They said to one another, ‘Surely we are being punished because of our brother. We saw how distressed he was when he pleaded with us for his life, but we would not listen; that’s why this distress has come on us.’

22Reuben replied, ‘Didn’t I tell you not to sin against the boy? But you wouldn’t listen! Now we must give an accounting for his blood.’ 23They did not realise that Joseph could understand them, since he was using an interpreter.

24He turned away from them and began to weep, but then came back and spoke to them again. He had Simeon taken from them and bound before their eyes.

25Joseph gave orders to fill their bags with grain, to put each man’s silver back in his sack, and to give them provisions for their journey. After this was done for them, 26they loaded their grain on their donkeys and left.

27At the place where they stopped for the night one of them opened his sack to get feed for his donkey, and he saw his silver in the mouth of his sack. 28‘My silver has been returned,’ he said to his brothers. ‘Here it is in my sack.’

Their hearts sank and they turned to each other trembling and said, ‘What is this that God has done to us?’

29When they came to their father Jacob in the land of Canaan, they told him all that had happened to them. They said, 30‘The man who is lord over the land spoke harshly to us and treated us as though we were spying on the land. 31But we said to him, “We are honest men; we are not spies. 32We were twelve brothers, sons of one father. One is no more, and the youngest is now with our father in Canaan.”

33‘Then the man who is lord over the land said to us, “This is how I will know whether you are honest men: leave one of your brothers here with me, and take food for your starving households and go. 34But bring your youngest brother to me so I will know that you are not spies but honest men. Then I will give your brother back to you, and you can trade42:34 Or move about freely in the land.” ’

35As they were emptying their sacks, there in each man’s sack was his pouch of silver! When they and their father saw the money pouches, they were frightened. 36Their father Jacob said to them, ‘You have deprived me of my children. Joseph is no more and Simeon is no more, and now you want to take Benjamin. Everything is against me!’

37Then Reuben said to his father, ‘You may put both of my sons to death if I do not bring him back to you. Entrust him to my care, and I will bring him back.’

38But Jacob said, ‘My son will not go down there with you; his brother is dead and he is the only one left. If harm comes to him on the journey you are taking, you will bring my grey head down to the grave in sorrow.’