Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 40:1-23

Mnyweshaji Na Mwokaji

1Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. 240:2 Mit 16:14; Es 2:21Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, 340:3 Mwa 37:36; 39:20akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu. 440:4 Mwa 37:36; 42:17Mkuu wa kikosi cha ulinzi akawakabidhi kwa Yosefu, naye akawahudumia.

Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda, 5kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti.

6Yosefu alipowajia asubuhi yake, akawaona kwamba walikuwa na huzuni. 7Ndipo Yosefu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”

840:8 Mwa 41:8, 15; Kum 29:29Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri.”

Ndipo Yosefu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”

9Basi mkuu wa wanyweshaji akamweleza Yosefu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu niliona mzabibu mbele yangu, 1040:10 Isa 27:6; Hos 14:7nao mzabibu ulikuwa na matawi matatu. Mara tu ulipoanza kuchipua, maua yalichanua na vishada vyake vikawa zabibu zilizoiva. 11Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.”

1240:12 Dan 2:36Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. 1340:13 Yos 1:11Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake. 1440:14 1Sam 25:31; 1The 2:7Lakini wakati mambo yatakapokuwia mazuri, unikumbuke, unifanyie wema, useme mema juu yangu kwa Farao ili niondoke huku gerezani. 15Kwa maana nilichukuliwa kwa nguvu kutoka nchi ya Waebrania, na hata hapa nilipo sikufanya lolote linalostahili niwekwe gerezani.”

1640:16 Amo 8:1-2Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yosefu amefasiri ikiwa na maana nzuri, akamwambia Yosefu, “Mimi pia niliota ndoto: Kichwani mwangu kulikuwepo vikapu vitatu vya mikate. 17Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.”

1840:18 Mwa 40:12Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 1940:19 Kum 21:22-23; 1Sam 17:44Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.”

20Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake: 2140:21 2Fal 25:27; Yer 52:31Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mikononi mwa Farao tena, 22lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, sawasawa na jinsi Yosefu alivyowaambia katika tafsiri yake.

2340:23 Mhu 1:11Pamoja na hayo, mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yosefu, bali alimsahau.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 40:1-23

約瑟解夢

1後來,埃及王的侍酒總管和膳食總管得罪了王, 2王非常憤怒, 3把他們囚禁在護衛長波提乏府內的監牢裡,也就是約瑟被囚的地方。 4護衛長派約瑟去伺候他們。他們在監裡待了一段日子。

5一天晚上,他們倆都做了夢,他們的夢各有不同的意思。 6第二天早上,約瑟過來見他們神情沮喪, 7就問:「你們今天為什麼滿面愁容?」 8他們回答說:「我們都做了夢,可是沒有人給我們解夢。」約瑟說:「解夢的能力不是來自上帝嗎?請你們把夢告訴我。」

9侍酒總管便把自己的夢告訴約瑟,說:「我夢見一棵葡萄樹, 10樹上有三根枝子,枝子發芽開花,結滿了成熟的葡萄。 11我手上拿著法老的酒杯,摘下葡萄,把汁擠在酒杯中,然後遞給法老。」 12約瑟說:「這夢的意思是,三根枝子代表三天, 13三天之內,法老必定釋放你,恢復你侍酒總管的職位。你仍要和從前一樣伺候法老飲酒。 14當你再被重用的時候,請你記得恩待我,在法老面前提及我,救我出獄。 15我是從希伯來人那裡被拐來的,無辜被囚在監。」

16膳食總管見夢解得好,就對約瑟說:「我也做了個夢,我夢見自己頭上頂著三筐白餅, 17最上面的一筐裡放著為法老烤製的各種食物,有鳥來吃筐內的食物。」 18約瑟說:「這夢的意思是,三筐就是三天, 19三天之內,法老必砍下你的頭,把你掛在木頭上,鳥要來吃你的肉。」

20第三天是法老的生日,他宴請文武百官,把侍酒總管和膳食總管從監牢裡提出來, 21恢復了侍酒總管的職位,讓他仍舊伺候自己飲酒, 22卻處死了膳食總管,正應驗了約瑟的話。 23然而,法老的侍酒總管把約瑟忘了。