Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 39:1-23

Yosefu Na Mke Wa Potifa

139:1 Mwa 37:36Wakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri.

2Bwana alikuwa pamoja na Yosefu, naye akastawi, Yosefu akaishi nyumbani kwa bwana wake Mmisri. 339:3 Mwa 21:22; Za 1:3Potifa alipoona kuwa Bwana alikuwa pamoja na Yosefu na kwamba Bwana alimfanikisha kwa kila kitu alichokifanya, 439:4 1Fal 11:28Yosefu alipata kibali machoni pa Potifa, akamfanya mhudumu wake. Potifa akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, naye akamkabidhi kuwa mwangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho. 539:5 2Sam 6:11; Za 128:4Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, Bwana aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yosefu. Baraka ya Bwana ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani. 6Kwa hiyo Potifa akamwachia Yosefu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho, Yosefu alipokuwa katika uongozi, Potifa hakuwa na sababu ya kujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula.

Yosefu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia; 7baada ya kitambo mke wa Potifa akamtamani Yosefu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!”

839:8 Mit 6:23-24Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi. 939:9 Hes 22:34Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” 10Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye.

1139:11 Kut 18:20Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. 1239:12 Mit 7:13; 2Tim 2:22Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia.

13Yule mwanamke alipoona kwamba Yosefu amemwachia vazi lake mkononi na kukimbilia nje ya nyumba, 1439:14 Kum 22:24, 27akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele. 15Aliposikia kelele za kuomba msaada, akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia nje.”

16Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani. 1739:17 Kut 20:16; Mwa 14:13Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki. 18Lakini mara nilipopiga kelele kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu akakimbia nje ya nyumba.”

19Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka. 2039:20 Za 105:18Potifa akamchukua Yosefu na kumweka gerezani, mahali ambapo wahalifu wa mfalme walikuwa wamefungwa.

Lakini wakati Yosefu alipokuwa huko gerezani, 2139:21 Kut 3:21; Mit 16:7Bwana alikuwa pamoja naye, akamhurumia na kumpa kibali mbele ya msimamizi wa gereza. 22Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. 2339:23 Mwa 21:20; Hes 14:43Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yosefu, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja na Yosefu akimfanikisha kwa kila alichofanya.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 39:1-23

约瑟遭陷害

1约瑟以实玛利商人带到埃及,卖给了法老的内臣护卫长波提乏2约瑟住在他的埃及主人家中,耶和华与他同在,使他凡事亨通。 3他主人看出耶和华与他同在,使他凡事亨通, 4就赏识他,让他服侍自己,派他管理自己家中一切事务。 5自从埃及波提乏约瑟管理自己家中一切事务以后,耶和华因为约瑟的缘故而赐福他主人家,使他主人家里和田间的一切都蒙福。 6于是,波提乏把一切事都交给约瑟管理,除了自己要吃的食物以外,什么也不管。

约瑟体格健壮,相貌英俊。 7后来,波提乏的妻子看中了约瑟,向他眉目传情,要引诱他上床。 8约瑟拒绝了她,说:“我主人信任我,把家里一切事都交给我管理。 9在这家里,没有人比我权力更大了,我主人把一切都交给了我,唯独你除外,因为你是他的妻子。我怎能做这种丑事得罪上帝呢?” 10但她还是每天勾引约瑟约瑟不从,并尽量避开她。

11一天,约瑟进屋里办事,那时屋里没有其他人。 12波提乏的妻子抓住约瑟的外衣,硬要与他上床。约瑟丢下外衣摆脱她逃了出去。 13她见约瑟丢下外衣逃了出去, 14就叫来家里的人,对他们说:“你们看,我丈夫带回家的这个希伯来人戏弄我们!他进来要与我上床,我就大声呼喊, 15他听见我大声喊叫,就把衣服丢在我这里,逃了出去。” 16她把约瑟的外衣留在身边,等她丈夫回来后, 17就对他说:“你带回来的那个希伯来人进来要戏弄我, 18我大声喊叫,他就把衣服丢在我这里,逃了出去。”

19波提乏听了妻子讲述约瑟如何对待她之后,勃然大怒, 20约瑟关进王囚禁犯人的监牢。 21约瑟坐牢的时候,耶和华与他同在,恩待他,使监狱长赏识他。 22监狱长把狱中所有囚犯及一切事务都交给约瑟管理。 23凡交到约瑟手中的事情,监狱长都很放心,因为耶和华与约瑟同在,使他凡事亨通。