Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 38:1-30

Yuda Na Tamari

138:1 Yos 12:15; 2Nya 11:7Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami. 238:2 1Nya 2:3Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua, akamwoa na akakutana naye kimwili, 338:3 Mwa 38:6; Hes 26:19akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. 4Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. 538:5 Hes 26:20Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.

6Yuda akampatia Eri, mzaliwa wake wa kwanza, mke aitwaye Tamari. 738:7 Mwa 46:12Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana akamuua.

838:8 1Nya 2:3Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako, na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako, ili umpatie ndugu yako uzao.” 9Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao. 10Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa Bwana, hivyo, pia Bwana akamuua Onani.

1138:11 Rut 1:13Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako mpaka mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Angeweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari alikwenda kuishi nyumbani kwa baba yake.

12Baada ya muda mrefu mke wa Yuda binti wa Shua akafariki. Baada ya msiba, Yuda alikwenda Timna, kwa watu waliokuwa wakikata kondoo wake manyoya, naye alifuatana na rafiki yake Hira Mwadulami.

13Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani kwenda Timna kukata kondoo wake manyoya,” 1438:14 Mwa 24:65alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.

1538:15 Amu 11:1Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. 16Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.”

Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?”

1738:17 Mwa 38:20Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”

Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?”

1838:18 1Fal 21:8; Isa 49:16Akamuuliza, “Nikupe amana gani?”

Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. 1938:19 Mwa 38:14Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane.

20Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke. 2138:21 Law 19:29; 2Fal 23:7Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?”

Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”

22Kwa hiyo akamrudia Yuda na kumwambia, “Sikumpata. Zaidi ya hayo, watu wanaoishi mahali pale walisema ‘Hapakuwahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.’ ”

2338:23 Ay 12:3; Yer 20:7Kisha Yuda akasema, “Mwache avichukue vitu hivyo, ama sivyo tutakuwa kichekesho. Hata hivyo, nilimpelekea mwana-mbuzi, lakini hukumkuta.”

2438:24 Yos 7:25; 1Sam 31:12Baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na matokeo yake ana mimba.”

Yuda akasema, “Mtoeni nje na achomwe moto hadi afe!”

25Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua kwamba pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.”

2638:26 1Sam 24:17; Mwa 38:11Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ana haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumkabidhi kwa mwanangu Shela ili awe mkewe.” Tangu hapo hakukutana naye kimwili tena.

27Wakati ulipofika wa kujifungua, kukawa na wana mapacha tumboni mwake. 28Alipokuwa akijifungua, mmoja akatoa mkono wake nje, kwa hiyo mkunga akachukua uzi mwekundu na kuufunga mkononi mwa yule mtoto, akasema, “Huyu ametoka kwanza.” 2938:29 Hes 26:20-21; Mt 1:3Lakini alipourudisha mkono wake ndugu yake akaanza kutoka, naye akasema, “Hivi ndivyo ulivyotoka kwa nguvu!” Akaitwa Peresi. 30Kisha ndugu yake, aliyekuwa na uzi mwekundu mkononi, akatoka, naye akaitwa Zera.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 38:1-30

犹大与她玛

1那时,犹大离开了他的兄弟们,到亚杜兰希拉的家里住。 2他在那里遇见了迦南书亚的女儿,就娶她为妻,与她同房。 3她怀孕生了一个儿子,犹大给他取名叫4她又怀孕生了一个儿子,给他取名叫俄南5她再次怀孕生了一个儿子,给他取名叫示拉示拉是在基悉出生的。

6犹大给长子娶了她玛为妻。 7耶和华见行为邪恶,就取走了他的性命。 8犹大俄南说:“你要与哥哥的妻子她玛同房,向她尽你做弟弟的本分,好替你哥哥传宗接代。” 9俄南知道生了儿子也不归自己,所以每次与她玛同房都把精液遗在地上,免得给他哥哥留后。 10耶和华见俄南行为邪恶,就取走了他的性命。 11犹大恐怕示拉会像他的两个哥哥一样死去,就对儿媳她玛说:“示拉还没有长大,你先回娘家守寡吧。”

12多年后,犹大的妻子,即书亚的女儿死了,等到守丧的日子满了,犹大就和他的朋友亚杜兰希拉亭拿,到替他剪羊毛的人那里。 13有人告诉她玛说:“你公公到亭拿去剪羊毛了。” 14她玛示拉已经长大,却仍然没有娶她,就脱下寡妇的衣服,蒙上脸,换了装束,坐在去亭拿路上的伊拿印城门口。 15犹大看见她蒙着脸,以为她是妓女, 16就走过去对她说:“你陪我睡觉吧。”犹大不知道她是自己的儿媳妇。她玛问道:“你要我陪你睡觉,你给我什么呢?” 17犹大回答说:“我会从羊群中取一只山羊羔送给你。”她玛问道:“羊还没有送来以前,你给我什么作抵押呢?” 18犹大问:“你要什么作抵押呢?”她玛说:“我要你的印、印带和你的手杖。”犹大给了她,然后跟她睡觉。她玛就这样怀了孕。 19事后,她起来走了。她拿掉蒙脸的布,仍旧穿上寡妇的装束。

20犹大托他的朋友亚杜兰人送去一只山羊羔,要从那女人手中换回抵押物,却找不到她。 21他的朋友就问当地的人:“伊拿印路旁的庙妓在哪里?”他们回答说:“这里没有庙妓。” 22他的朋友只好回去对犹大说:“我找不着她,当地人说那里没有庙妓。” 23犹大说:“让她留着我的东西吧,免得我们成为笑柄。反正我把羊送过去了,只是你找不到她。”

24大约过了三个月,有人告诉犹大说:“你的儿媳妇她玛不守妇道,并且怀孕了。”犹大说:“把她拉出来烧死!” 25他们正要把她拉出来,她请人带口信给他公公,说:“这些东西的主人使我怀了孕,请你看这印、印带和杖是谁的?” 26犹大认出是自己的东西,就说:“她比我更有理,因为我没有让示拉娶她。”犹大没有再与她睡觉。

27她玛临产的时候,才知道腹中是一对双胞胎。 28生产的时候,一个婴儿先伸出手来,接生婆就把一条红线系在他的手上,说:“他是先出生的。” 29可是那婴儿随后却把手缩回去,另一个婴儿先出生了,接生婆说:“你怎么抢先出来了?”因此,他的名字叫法勒斯38:29 法勒斯”意思是“抢先出来”。30后来,那个手上系有红线的孩子也出生了,给他取名叫谢拉38:30 谢拉”意思是“红色”或“光明”。