Mwanzo 35 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 35:1-29

Yakobo Arudi Betheli

135:1 Mwa 12:8Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.”

235:2 Yos 24:15; Kut 19:10, 14Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. 335:3 Mwa 32:7; Amu 2:15Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” 435:4 Mwa 24:22Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. 535:5 Kut 15:16Kisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo.

635:6 Mwa 28:19; 10:19Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. 735:7 Mwa 8:20Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli,35:7 El-Betheli maana yake Mungu wa Betheli. kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake.

835:8 Mwa 24:59; 12:8Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi.35:8 Alon-Bakuthi maana yake Mwaloni wa Kilio.

935:9 Mwa 28:13; 32:29Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 1035:10 Mwa 17:5Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli.

1135:11 Mwa 17:1; 17:6Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,35:11 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 1235:12 Mwa 28:13; 12:7Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 1335:13 Mwa 17:22Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.

1435:14 Mwa 28:18; Kut 29:40Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. 1535:15 Mwa 12:8Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.35:15 Betheli maana yake Nyumba ya Mungu.

Vifo Vya Raheli Na Isaki

1635:16 Mwa 48:7Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 1735:17 Kut 1:15; Mwa 30:24Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 1835:18 1Sam 4:21Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.35:18 Benoni maana yake Mwana wa huzuni yangu. Lakini babaye akamwita Benyamini.35:18 Benyamini maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.

1935:19 Mwa 48:7Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). 2035:20 1Sam 10:2; 6:18Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli.

21Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. 22Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili.

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:

23Wana wa Lea walikuwa:

Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,

Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.

2435:24 Mwa 30:24; 35:18Wana wa Raheli walikuwa:

Yosefu na Benyamini.

2535:25 Mwa 30:24Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa:

Dani na Naftali.

2635:26 Mwa 37:2Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa:

Gadi na Asheri.

Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.

2735:27 Mwa 13:18; Amu 1:10Yakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. 2835:28 Mwa 25:7Isaki aliishi miaka 180. 2935:29 Mwa 15:15; 25:8-9Kisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika.