Mwanzo 33 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 33:1-20

Yakobo Akutana Na Esau

133:1 Mwa 32:6Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. 2Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. 333:3 Mwa 42:6Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake.

4Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. 533:5 Za 127:3; Isa 8:18Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?”

Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”

6Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu. 7Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu.

833:8 Mwa 24:9; 32:14-16Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?”

Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”

933:9 Mwa 13:6Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.”

1033:10 Mwa 16:13Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa. 1133:11 1Sam 25:27Tafadhali ukubali zawadi iliyoletwa kwako, kwa kuwa Mungu amenineemesha na ninavyo vyote ninavyohitaji.” Kwa sababu Yakobo alisisitiza, Esau akapokea.

12Ndipo Esau akasema, “Na tuendelee na safari, nitakuwa pamoja nawe.”

1333:13 Isa 40:11Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ngʼombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa. 1433:14 Kut 12:38Hivyo bwana wangu umtangulie mtumishi wako, wakati mimi nikija polepole kwa mwendo wa makundi yaliyo mbele yangu na mwendo wa watoto, mpaka nifike kwa bwana wangu huko Seiri.”

1533:15 Mwa 32:5Esau akamwambia, “Basi na niwaache baadhi ya watu wangu pamoja nawe.”

Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo, niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.”

1633:16 Mwa 14:6Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri. 1733:17 Amu 8:5, 6, 8, 14-16Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,33:17 Sukothi maana yake Vibanda. mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi.

1833:18 Mwa 12:6Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji. 1933:19 Yos 24:32; Yn 4:5Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake. 20Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli.33:20 El-Elohe-Israeli maana yake Mungu, Mungu wa Israeli au Mwenye Nguvu ni Mungu wa Israeli.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

创世记 33:1-20

弟兄重逢

1雅各抬头看见以扫带着四百人迎面而来,便把孩子们分别交给利亚拉结和两个婢女, 2又让两个婢女和她们的孩子走在前面,利亚和她的孩子跟在后面,拉结约瑟走在最后。 3他自己则走在他们前面,接连俯伏下拜七次,直到他哥哥跟前。

4以扫跑上去迎接他,拥抱他,亲吻他,二人抱头痛哭。 5以扫抬眼看见跟在雅各后面的妇女和孩子,就问:“这些和你同行的是谁?”雅各说:“这些孩子是上帝施恩赐给你仆人的。” 6雅各的两个婢女和她们的孩子上前下拜, 7利亚和她的孩子也上前下拜,最后约瑟拉结也上前向以扫下拜。

8以扫说:“我在路上遇见的那一群群牲畜是怎么回事?”雅各回答说:“我带来这些是想在我主面前蒙恩。” 9以扫说:“弟弟,我已经有很多了,你自己留着吧!” 10雅各说:“不,你若赏脸,就请收下!我见了你的面就像见了上帝的面,因为你这样善待我。 11请你收下我的礼物吧,因为上帝恩待了我,使我富足。”雅各再三恳求,以扫才收下。

12以扫说:“我们走吧!我陪你们走。” 13雅各却说:“我主知道孩子们还幼小,而且,我还要照料正在哺乳的牛羊,如果整天赶路,牛羊都会累死。 14请我主先走,我迁就牲畜和孩子的脚步慢慢走,我在西珥与我主会合。”

15以扫说:“我给你留几个随从吧。”雅各说:“不用了,能得到我主的恩待就够了。” 16于是,以扫在当天先回西珥去了, 17雅各却去了疏割,在那里为自己建造房屋,为牲畜搭起棚子。因此那地方叫疏割33:17 “疏割”意思是“棚子”。

18这样,雅各巴旦·亚兰平安地回到迦南示剑城,在城外搭营居住。 19他搭营居住的这块地是他用一百块银子向示剑的父亲哈抹的子孙买的。 20雅各在那里筑了一座坛,称之为伊利·伊罗伊·以色列33:20 “伊利·伊罗伊·以色列”意思是“以色列的上帝”。