Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 32:1-32

Yakobo Ajiandaa Kukutana Na Esau

1Yakobo pia akaondoka akaenda zake, nao malaika wa Mungu wakakutana naye. 2Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu.32:2 Mahanaimu maana yake Kambi mbili.

332:3 Mwa 25:30Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu. 432:4 Mwa 18:3Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema, nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwako huko mpaka sasa. 532:5 Mwa 24:9; 34:11Ninao ngʼombe na punda, kondoo na mbuzi, watumishi wa kiume na wa kike. Sasa ninatuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili nipate kibali machoni pako.’ ”

632:6 Mwa 33:1Wajumbe waliporudi kwa Yakobo, wakamwambia, “Tulikwenda kuonana na ndugu yako Esau, naye sasa anakuja kukulaki akifuatana na wanaume 400.”

7Kwa hofu kuu na huzuni, Yakobo akagawanya watu aliokuwa nao katika makundi mawili, pia akagawanya makundi ya kondoo na mbuzi, na vilevile ngʼombe na ngamia. 8Yakobo alifikiri, “Kama Esau akija na kushambulia kundi moja, kundi lililobaki litaweza likanusurika.”

932:9 Mwa 31:13Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, Mungu wa baba yangu Isaki, Ee Bwana, ambaye uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi,’ 1032:10 Mwa 24:27mimi sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa ninayo makundi mawili. 1132:11 Mwa 27:41Nakuomba, uniokoe na mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia mama pamoja na watoto wao. 1232:12 Hos 1:10Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ”

1332:13 Mwa 43:11, 15, 25, 26; Mit 18:16Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: 1432:14 Hes 7:88Mbuzi waume ishirini na mbuzi wake 200, kondoo dume ishirini na kondoo wake 200. 1532:15 Mwa 13:2Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi. 1632:16 Mwa 33:8Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.”

17Akamwagiza yule aliyetangulia kuwa, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’ 1832:18 Mwa 18:3Ndipo utakaposema, ‘Ni mali ya mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi ambazo zimetumwa kwa bwana wangu Esau, naye anakuja nyuma yetu.’ ”

19Akamwagiza pia yule mtumishi wa kundi la pili, la tatu na yale mengine yote yaliyofuata akiwaambia, “Mtamwambia Esau maneno hayo hayo mtakapokutana naye. 2032:20 1Sam 9:7Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza, hatimaye, nitakapomwona, huenda atanikubali.” 21Kwa hiyo zawadi za Yakobo zilitangulia mbele yake, lakini yeye mwenyewe alilala kambini usiku ule.

Yakobo Ashindana Mweleka Na Mungu

2232:22 Kum 2:37; 3:16Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki. 23Baada ya kuwavusha ngʼambo ya kijito, alivusha pia mali zake zote. 24Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. 25Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 2632:26 Hos 12:4Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.”

Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

27Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?”

Akajibu, “Yakobo.”

2832:28 Mwa 17:5Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,32:28 Israeli maana yake Yeye ashindanaye na Mungu. kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”

29Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.”

Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.

3032:30 Mwa 16:13Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli,32:30 Penieli maana yake Uso wa Mungu, ambalo ni sawa na Penueli kwa Kiebrania. akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.”

3132:31 Amu 8:9Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake. 32Kwa hiyo mpaka leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 32:1-32

雅各預備見以掃

1雅各繼續前行,遇見了上帝的天使。 2雅各看見他們,就說:「這是上帝的軍隊!」於是稱那地方為瑪哈念32·2 瑪哈念」意思是「兩營軍隊」。

3雅各先派人到西珥,就是以東,去見他哥哥以掃4並吩咐他們:「你們要這樣對我主以掃說,『你僕人雅各一直寄居在拉班家裡, 5現在他帶了牛羊、驢和僕婢回來見你,派我們來報信,希望得到你的恩待。』」

6報信的人回到雅各那裡,說:「我們到了你哥哥以掃那裡,他正帶著四百人前來見你。」 7雅各聽了非常害怕,便把隨從、牛群、羊群和駱駝分成兩隊, 8心想:「如果以掃來攻擊一隊,另一隊還可以逃生。」

9他禱告說:「耶和華,我祖父亞伯拉罕和我父親以撒的上帝啊!你吩咐我回到家鄉和親族那裡,答應厚待我。 10我不配蒙你以慈愛和信實相待,我先前過約旦河的時候,手上只有一根杖,現在卻有兩隊人丁家畜。 11求你救我脫離我哥哥以掃的手,我怕他會來殺我和我的妻兒。 12然而,你曾說,『我必厚待你,使你的後代多如海沙,不可勝數。』」

13那天晚上,雅各就在那裡過夜,又挑選牲畜送給哥哥以掃作禮物: 14母山羊二百隻、公山羊二十隻、母綿羊二百隻、公綿羊二十隻、 15哺乳的駱駝三十頭及其小駱駝、母牛四十頭、公牛十頭、母驢二十頭、驢駒十頭。 16雅各把牲畜每類分成一群,交給僕人看管,對他們說:「你們走在前頭,每群牲畜之間要保持一段距離!」 17又吩咐走在最前面的僕人說:「我哥哥以掃遇到你的時候,如果問你是誰家的人?要到哪裡去?前頭這些牲畜是誰的? 18你就說,『是僕人雅各要送給他主人以掃的禮物,他自己就跟在後面。』」 19雅各又吩咐看管第二群、第三群及其餘牲畜的僕人遇見以掃時也要這樣回答, 20並且一定要說:「你僕人雅各就在後面。」雅各想先用禮物去化解以掃的怨恨,或許見面時以掃會善待他。 21於是,他派人先把禮物送過去,自己則留在營裡過夜。

雅各遇見上帝

22那天晚上,雅各起來帶著兩個妻子、兩個婢女和十一個兒子渡過雅博渡口。 23雅各把他們連同一切所有都送過河以後, 24自己獨自留下。這時,有一個人來和他摔跤,直到黎明。 25那人見勝不過雅各,就在他的大腿窩摸了一下,他大腿的關節就脫了臼。 26那人說:「天亮了,讓我走吧!」但雅各說:「你不祝福我,我就不讓你走。」 27那人問道:「你叫什麼名字?」他說:「我叫雅各。」 28那人說:「你以後不要再叫雅各了,你要叫以色列,因為你跟上帝和人角力都得勝了。」

29雅各說:「請你告訴我你的名字。」那人說:「你為什麼問我的名字?」他就在那裡給雅各祝福。 30雅各稱那地方為毗努伊勒,因為他說:「我當面見過上帝,竟能活命。」 31雅各經過毗努伊勒的時候,太陽出來了,那時他的大腿瘸了。 32以色列人至今都不吃大腿窩的筋,因為那人摸過雅各大腿窩的筋。