Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 3:1-24

Kuanguka Kwa Mwanadamu

13:1 Ay 1:7; 2:2; 2Kor 11:3; Ufu 12:9; 20:2; Mwa 2:17Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

23:2 Mwa 2:16-17Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, 3lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

43:4 Yn 8:44; 2Kor 11:3Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 53:5 Mwa 1:26; 14:18-19; Za 7:8; Isa 14:14; Eze 28:2Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

63:6 Yak 1:14-15; 1Yn 2:16; Hes 30:7-8; Yer 44:15, 19, 24; 2Kor 11:3; 1Tim 2:14Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala. 73:7 Mwa 2:25Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

83:8 Law 26:12; Kum 23:14; Ay 13:16; 23:7; 34:22-23; Isa 29:15; Za 139:7-12; Yer 16:17; 23:24; 49:10; Ufu 6:15-16Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 93:9 Mwa 4:9; 16:8; 18:9; 1Fal 19:9-13Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

103:10 Kut 19:16; 20:18; Kum 5:5; Mwa 2:25; 1Sam 12:18Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

113:11 Mwa 2:17, 25Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

123:12 Mwa 2:22Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

133:13 Rum 7:11; 2Kor 11:3; 1Tim 2:14Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

143:14 Za 72:9; Mik 7:17; Kum 28:15-20; Isa 49:23; 65:25Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili,

“Umelaaniwa kuliko wanyama wote

wa kufugwa na wa porini!

Utatambaa kwa tumbo lako

na kula mavumbi

siku zote za maisha yako.

153:15 Yn 8:44; 1Yn 3:8; Mdo 13:10; Mwa 16:11; Amu 13:5; Ebr 2:14; Isa 7:14; 8:3; 9:6; Mt 1:23; Lk 1:31; Gal 4:4; Ufu 12:17; Rum 16:20Nami nitaweka uadui

kati yako na huyo mwanamke,

na kati ya uzao wako na wake,

yeye atakuponda kichwa,

nawe utamuuma kisigino.”

163:16 Za 48:5-6; Isa 13:8; 21:3; 26:17; Yer 4:31; 6:24; Mik 4:9; 1Kor 11:3; Efe 5:22; 1Tim 2:15Kwa mwanamke akasema,

“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;

kwa utungu utazaa watoto.

Tamaa yako itakuwa kwa mumeo

naye atakutawala.”

173:17 Mwa 2:17; 5:29; 6:13; 8:21; 47:9; 29:32; 31:42; Hes 35:33; Za 66:11; 106:39; 127:2; Isa 24:5; Rum 8:20-22; Isa 54:9; Kut 3:7; Mhu 1:13; 2:23; Ay 5:7; 14:1; Yer 20:18Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’

“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,

kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo

siku zote za maisha yako.

183:18 Za 104:14; Ay 31:40; Isa 5:6; Ebr 6:8Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,

nawe utakula mimea ya shambani.

193:19 Mwa 2:7; 14:18; Kum 8:3, 9; 23:4; Rum 1:6; 2:14; 2The 3:10; Ay 7:21; Ebr 9:27; Za 146:4; 104:23; Rut 1:6; 2:14; 1Kor 15:47Kwa jasho la uso wako

utakula chakula chako

hadi utakaporudi ardhini,

kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,

kwa kuwa wewe u mavumbi

na mavumbini wewe utarudi.”

203:20 Mwa 2:20; 2Kor 11:3; 1Tim 2:13Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

21Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 223:22 Mwa 2:9; 1:26; Ufu 2:7Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” 233:23 Mwa 2:7-8Hivyo Bwana Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. 243:24 Kut 25:18-22; 1Sam 4:4; 2Sam 6:2; 22:11; 1Fal 6:27; 8:6; 2Fal 19:15; 2Nya 5:8; Za 18:10; 104:4; Isa 27:1; 37:16; Eze 10:1; Mwa 2:9; Ay 40:19Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 3:1-24

始祖犯罪

1在耶和華上帝所造的田野的各種動物中,蛇最狡猾。蛇對女人說:「上帝真的說過不許你們吃園中所有樹上的果子嗎?」 2女人回答說:「我們可以吃園中樹上的果子, 3只是不可以吃園子中間那棵樹的果子。上帝曾經吩咐說,『你們不可吃那果子,也不可摸,否則你們就會死。』」 4蛇對女人說:「你們一定不會死! 5上帝那樣說是因為祂知道你們吃了那樹的果子以後,眼睛就會明亮,像上帝一樣懂得分辨善惡。」 6女人見那棵樹上的果子可口,賞心悅目,可以使人有智慧,就摘下來吃了。她也把果子給跟她在一起的丈夫,他也吃了。 7二人的眼睛果然明亮起來,這才發覺自己原來赤身露體,便把無花果樹的葉子編起來遮體。

8傍晚天涼時,夫婦二人聽見耶和華上帝在園中行走的聲音,就藏在園子的樹叢中,想躲開耶和華上帝。 9耶和華上帝呼喚那人說:「你在哪裡?」 10那人說:「我聽見你在園中行走的聲音,就害怕得躲了起來,因為我赤身露體!」 11耶和華上帝問:「誰說你赤身露體?難道你吃了我吩咐你不可吃的果子嗎?」 12那人說:「你賜給我作伴的女人摘了那樹上的果子給我,我就吃了。」 13耶和華上帝對女人說:「你這做的是什麼事?」女人說:「是蛇誘騙我,我才吃的。」

上帝的審判

14耶和華上帝對蛇說:

「你既然做了這事,

你要比一切的牲畜和野獸受更重的咒詛,

你要用肚子爬行,

一生都要吃塵土。

15我要使你和女人結仇,

你的後代和女人的後代也要彼此為仇,

女人的後代必傷你的頭,

你必傷他的腳跟。」

16耶和華上帝對女人說:

「我必大大加重你懷孕的痛苦,

你分娩時必受痛苦。

你必戀慕3·16 戀慕」或譯「想控制」。自己的丈夫,

你的丈夫必管轄你。」

17耶和華上帝又對亞當說:

「因為你聽從妻子的話,

吃了我吩咐你不可吃的果子,

地必因你而受咒詛。

你必終生艱辛勞苦,

才能吃到地裡出產的食物。

18地必給你長出荊棘和蒺藜,

你要吃田間長出來的菜蔬。

19你必汗流滿面,才有飯吃,

一直到你歸回塵土。

因為你是塵土造的,

也必歸回塵土。」

20亞當給他的妻子取名叫夏娃,因為她是眾生之母。 21耶和華上帝做了皮衣給他們夫婦穿。 22耶和華上帝說:「看啊,那人已經與我們相似,能分辨善惡。現在,恐怕他會伸手去摘生命樹的果子吃,那樣他就會永遠活著。」 23因此,耶和華上帝就把亞當趕出伊甸園,讓他去開墾土地——他的本源。 24上帝趕走了亞當以後,就派遣基路伯天使駐守在伊甸園東邊,又用一把旋轉的火劍守護在通往生命樹的路上。