Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 28:1-22

128:1 Mwa 24:3Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani. 2Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. 328:3 Mwa 17:1; Hes 6:24Mungu Mwenyezi28:3 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). na akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu. 428:4 Mwa 12:2, 3; 17:8Na akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Abrahamu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Abrahamu.” 528:5 Hos 12:12; Mwa 24:29Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau.

6Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,” 7tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu. 828:8 Mwa 26:35Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani. 9Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.

Ndoto Ya Yakobo Huko Betheli

10Yakobo akatoka Beer-Sheba kwenda Harani. 11Alipofika mahali fulani, akalala hapo kwa sababu jua lilikuwa limetua. Akachukua jiwe moja la mahali pale, akaliweka chini ya kichwa chake akajinyoosha akalala usingizi. 1228:12 Yn 1:51Akaota ndoto ambayo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni na malaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka juu yake. 13Juu yake alisimama Bwana, akasema, “Mimi ni Bwana, Mungu wa baba yako Abrahamu na Mungu wa Isaki. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. 1428:14 Mwa 26:4; 12:3; Gal 3:8Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa. 1528:15 Kum 31:6, 8; Law 26:42; Za 105:10Niko pamoja nawe nami nitakulinda kila uendako na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha mpaka nitakapofanya hayo niliyokuahidi.”

1628:16 1Fal 3:15; Yer 31:26Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.” 1728:17 Kut 3:5; Yos 5:15Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.”

18Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake. 1928:19 Yos 16:2; Amu 1:23, 26Mahali pale akapaita Betheli,28:19 Betheli maana yake Nyumba ya Mungu. ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

2028:20 Mwa 31:13; Amu 1:23, 26Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae 2128:21 Kum 26:17; Za 48:14; 118:28na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu, 2228:22 Mwa 14:20; Lk 18:12nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 28:1-22

1以撒雅各叫來,給他祝福,又囑咐他說:「你不要娶迦南的女子為妻。 2馬上去巴旦·亞蘭,到你外祖父彼土利家,在你舅父拉班的女兒中選一個做妻子。 3願全能的上帝賜福給你,使你的子孫眾多,成為許多民族。 4願上帝把賜給亞伯拉罕的福氣賜給你和你的後代,讓你承受你寄居之地為產業,就是上帝賜給亞伯拉罕的地方。」 5以撒雅各前往巴旦·亞蘭,去亞蘭人彼土利的兒子拉班那裡。拉班雅各以掃的舅父。

6以掃看見父親給雅各祝福,讓他到巴旦·亞蘭娶妻,叮囑他不要娶迦南的女子, 7又看見雅各聽從父母到巴旦·亞蘭去了, 8就知道父親以撒不喜歡迦南的女子。 9他便到亞伯拉罕的兒子以實瑪利那裡,娶了以實瑪利的女兒、尼拜約的妹妹瑪哈拉為妻。他娶瑪哈拉以前已經有兩個妻子了。

雅各的夢

10雅各離開別示巴,前往哈蘭11到了一個地方,太陽已經下山,他便在那裡過夜。他枕著一塊石頭睡覺, 12夢中看見有個梯子立在地上,直通到天上,梯子上有上帝的天使上上下下。 13耶和華站在梯子上28·13 在梯子上」或譯「在他旁邊」。雅各說:「我是耶和華,是你祖父亞伯拉罕的上帝,也是以撒的上帝。我要把你現在躺臥的地方賜給你和你的後代。 14你的後代必多如地上的塵沙,遍佈四方,地上萬族必因你和你的後代而蒙福。 15我與你同在,無論你去哪裡,我都會保護你,領你返回這片土地。我必實現對你的應許,決不離棄你。」

16雅各一覺醒來,說:「耶和華居然在這裡,我卻不知道。」 17他就害怕起來,說:「這地方何等可畏!這裡是上帝的家,是通天的大門。」

18雅各清早起來,把枕的那塊石頭立成柱子作記號,在上面澆上油。 19他稱那地方為伯特利28·19 伯特利」意思是「上帝的家」。,那地方以前叫路斯20雅各許願說:「如果上帝與我同在,在路上保護我,供給我衣食, 21帶領我平安地回到父親的家,我就一定敬奉耶和華為我的上帝。 22我立為柱子的這塊石頭必成為上帝的殿。凡你賜給我的,我必把十分之一獻給你。」