Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 27:1-46

Yakobo Anaipata Baraka Ya Isaki

1Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.”

Akajibu, “Mimi hapa.”

2Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu. 327:3 Mwa 25:27Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu. 4Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.”

5Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta, 6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, 7‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za Bwana kabla sijafa.’ 827:8 Mwa 27:13, 43Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: 9Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda. 10Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.”

1127:11 Mwa 25:25Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Lakini ndugu yangu Esau ana nywele mwilini, mimi nina ngozi nyororo. 1227:12 Mwa 27:22Itakuwaje kama baba yangu akinigusa? Itaonekana kwake kama niliyemfanyia ujanja na kuleta laana juu yangu badala ya baraka.”

13Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia, nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.”

14Kwa hiyo alikwenda akawaleta, akampa mama yake, akaandaa chakula kitamu, kama vile alivyopenda baba yake. 1527:15 Mwa 27:27Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. 16Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi. 17Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka.

18Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.”

Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”

1927:19 Mwa 27:4Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

20Isaki akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?”

Akajibu, “Bwana Mungu wako amenifanikisha.”

2127:21 Mwa 27:12Kisha Isaki akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.”

22Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaki, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.” 2327:23 Mwa 27:16Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki. 24Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?”

Akajibu, “Mimi ndiye.”

2527:25 Mwa 27:4Kisha akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nipate kukubariki.”

Yakobo akamletea naye akala, akamletea na divai akanywa. 26Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.”

2727:27 Kut 4:27; Ebr 11:20Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema,

“Aha, harufu ya mwanangu

ni kama harufu ya shamba

ambalo Bwana amelibariki.

2827:28 Kum 33:28; 33:11; 2Sam 1:21Mungu na akupe umande kutoka mbinguni

na utajiri wa duniani:

wingi wa nafaka na divai mpya.

2927:29 Mwa 9:25; 25:23; 12:3Mataifa na yakutumikie

na mataifa yakusujudie.

Uwe bwana juu ya ndugu zako,

na wana wa mama yako wakusujudie.

Walaaniwe wale wakulaanio,

nao wale wakubarikio wabarikiwe.”

3027:30 Mwa 31:54; Kut 18:12; 24:11Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni. 3127:31 Mwa 21:23, 27Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”

3227:32 Mwa 27:18; 21:30Isaki baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.”

3327:33 Mwa 21:14Isaki akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!”

3427:34 Ebr 12:17; Kut 12:32Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”

3527:35 Yer 9:4Lakini akasema, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako.”

3627:36 Mwa 25:26; Ebr 12:16-17Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?”

3727:37 Mwa 27:28; Kum 16:13Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?”

3827:38 Rut 1:9; Ebr 12:17Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.

3927:39 Ebr 11:20; Mwa 27:28Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia,

“Makao yako yatakuwa

mbali na utajiri wa dunia,

mbali na umande wa mbinguni juu.

4027:40 2Sam 8:14; 2Fal 8:20-22Utaishi kwa upanga,

nawe utamtumikia ndugu yako,

lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,

utatupa nira yake

kutoka shingoni mwako.”

Yakobo Anakimbilia Kwa Labani

4127:41 1Sam 17:28; Hos 10:14Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.”

42Rebeka alipokwisha kuambiwa yale aliyoyasema Esau mwanawe mkubwa, alimwita Yakobo mwanawe mdogo, akamwambia, “Ndugu yako Esau anajifariji kwa wazo la kukuua. 4327:43 Mwa 24:29; 11:31Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani. 44Ukae naye kwa muda mpaka ghadhabu ya ndugu yako itulie. 4527:45 Mwa 26:3Wakati ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze wote wawili kwa siku moja?”

4627:46 Mwa 26:35; Ay 7:7Kisha Rebeka akamwambia Isaki, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.”

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 27:1-46

以撒为儿子祝福

1以撒年老的时候,眼睛昏花,几乎看不见。他把大儿子以扫叫来,说:“我儿啊!”以扫说:“我在这里。” 2以撒说:“我年老了,不知道还能活多久。 3现在,带着你的弓箭去田野为我打些野味来, 4照我喜欢的口味,做成美食给我吃,以便我在死前给你祝福。”

5利百加听见了以撒跟儿子以扫说的话。以扫出去打猎后, 6利百加就对她儿子雅各说:“我听见你父亲对你哥哥以扫说, 7‘你去打些野味回来,做成美食给我吃,以便我死之前在耶和华面前给你祝福。’ 8现在,孩子,你要听我的话,照我的吩咐去做。 9你到羊群里选两头上好的山羊羔,我好照你父亲喜爱的口味做成美食, 10由你拿去给他吃,让他死前为你祝福。”

11雅各对母亲利百加说:“哥哥以扫浑身是毛,我的皮肤光滑。 12如果父亲用手摸我,一定会发觉我骗他,那时候我不但得不到祝福,反会招来咒诅。” 13他母亲利百加对他说:“孩子啊,有咒诅,我来承担。你只管听我的话,把羊羔牵来。”

14于是,雅各把羊牵来交给母亲,他母亲就照他父亲喜爱的口味做成美食。 15利百加又拿了大儿子以扫留在家里最好的衣服,给小儿子雅各穿上, 16再用山羊皮把雅各光滑的手和脖子都包起来, 17然后把做好的美味和饼交给雅各

18雅各来到父亲跟前,叫了一声:“父亲。”以撒回答说:“我在这里,孩子,你是谁?” 19雅各对父亲说:“我是你的大儿子以扫,你吩咐我的事,我已经办好了。请你坐起来,吃我打的野味,然后给我祝福。” 20以撒对他说:“孩子,你怎么这么快就打到野味了?”雅各回答说:“因为你的上帝耶和华让我碰见好机会。” 21以撒说:“孩子,过来,让我摸摸看你是不是我儿以扫。” 22雅各挨到父亲跟前,以撒摸着他说:“声音是雅各的声音,手却是以扫的手。” 23因为雅各手上有毛,与他哥哥以扫的手一样,以撒分辨不出来,就给他祝福。 24以撒又问:“你真是我的儿子以扫吗?”雅各回答说:“是。” 25以撒便说:“把野味拿给我,我吃了你打的野味就为你祝福。”雅各递上野味,以撒吃了;雅各又拿酒给他喝,他也喝了。 26以撒对他说:“孩子,你过来亲吻我。” 27雅各就挨上前去亲了父亲。以撒闻到他衣服上的气味,就祝福他说:

“我儿子的香气就像蒙耶和华赐福之田地的香气。

28愿上帝赐你天上的甘霖、肥沃的土地并丰富的五谷和新酒。

29愿万民都臣服于你,

万国都向你下拜。

愿你成为你弟兄的主人,

愿你母亲的儿子向你下拜。

咒诅你的,愿他受咒诅;

祝福你的,愿他蒙祝福。”

以扫求父亲祝福

30雅各接受了以撒的祝福才刚离开,他的哥哥以扫就打猎回来了。 31以扫把野味煮好,拿到父亲跟前,说:“父亲,请起来吃你儿子煮的野味,然后给我祝福。” 32他父亲以撒问道:“你是谁?”以扫回答说:“我是你的长子以扫。” 33以撒大为震惊,说:“你没有来之前,拿野味来给我吃的是谁呢?我已经吃了,也给那人祝福了,他将来必蒙祝福。”

34以扫听了放声痛哭,说:“父亲啊,求你也为我祝福!” 35以撒说:“你弟弟已经用诡计把你的福分夺去了。” 36以扫说:“怪不得他叫雅各,他已经骗了我两次,先前把我长子的名分夺去,现在又夺去我的福分!”接着他对父亲说:“难道你没有留下别的祝福可以给我吗?”

37以撒以扫说:“我已经立他做你的主人,使他的众弟兄做他的仆人,并给他五谷和新酒。孩子啊,我还能为你做什么呢?” 38以扫对父亲说:“父亲啊,你只有一个祝福吗?父亲啊,求你也为我祝福!”以扫又放声大哭。 39以撒对他说:

“你住的地方必远离肥沃的土地,

也不会有天上的甘霖。

40你必倚靠刀剑生活,

又必服侍你的弟弟。

到你无法忍受的时候,

你必挣脱颈上的重轭。”

雅各逃往舅父家

41以扫因为父亲把祝福给了雅各,就对雅各怀恨在心,暗自思量说:“父亲已经不久人世,他死后,我要把雅各杀掉!” 42以扫的计谋传到利百加耳中。她就派人把雅各叫来,对他说:“你哥哥以扫想要杀你泄愤! 43孩子,听我的话,现在就逃到哈兰你舅舅拉班那里, 44与他住些日子,一直住到你哥哥的气消了。 45等他气消了,忘了你对他所做的事,我会派人接你回来。我何必在一天之内失去你们两个呢?” 46利百加以撒说:“我被这些人女子烦死了。如果雅各也像以扫一样娶那些人女子为妻,我活着还有什么意思呢?”