Mwanzo 26 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 26:1-35

Isaki Na Abimeleki

126:1 Mwa 12:10; 20:1Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. 226:2 Mwa 12:1, 7; 46:3Bwana akamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. 326:3 Kut 3:12; Mwa 12:2, 7Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako. 426:4 Mwa 26:24; 48:4; 12:2Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, 526:5 Mwa 18:19; Za 119:80, 112; Eze 18:21kwa sababu Abrahamu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.” 626:6 Mwa 20:1Hivyo Isaki akaishi huko Gerari.

726:7 Mwa 12:13Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”

8Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake. 9Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ”

Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.”

1026:10 Mwa 12:8Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.”

1126:11 1Sam 24:6; 26:9; Za 105:15Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.”

1226:12 Mt 13:8; Mwa 26:3Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka huo huo, akavuna mara mia, kwa sababu Bwana alimbariki. 1326:13 Mwa 13:2; Kum 8:18Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana. 1426:14 Mwa 12:16; 24:36Akawa na mifugo ya kondoo na ngʼombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu. 1526:15 Mwa 21:30; 21:25Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo.

16Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.”

17Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. 18Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.

19Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,26:20 Eseki maana yake ni Ugomvi. kwa sababu waligombana naye. 21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.26:21 Sitna maana yake Upinzani. 2226:22 Kut 18:19; Mwa 17:6Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,26:22 Rehobothi maana yake ni Mungu ametufanyia nafasi. akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”

23Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. 2426:24 Mwa 24:12; 17:7Usiku ule Bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.”

25Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima.

2626:26 Mwa 21:22Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake. 27Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?”

2826:28 Mwa 21:22Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Bwana alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe 2926:29 Mwa 31:29, 52; 24:31kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’ ”

3026:30 Mwa 31:54; Kut 18:12Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. 3126:31 Mwa 21:23, 27Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.

3226:32 Mwa 21:30Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!” 3326:33 Mwa 21:14Naye akakiita Shiba,26:33 Shiba kwa Kiebrania maana yake ni Saba. mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba.26:33 Beer-Sheba maana yake ni Kisima cha wale saba, yaani wale kondoo saba ambao Abrahamu aliwatoa kama ushahidi kati yake na Abimeleki.

3426:34 Mwa 36:2Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti. 3526:35 Mwa 27:46; Ay 7:16Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka.