Mwanzo 25 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 25:1-34

Kifo Cha Abrahamu

1Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura. 225:2 Yer 25:25; Mwa 36:35; 37:28, 36; Kut 2:15; Hes 22:4; 25:6; Amu 6:1-3; 8:22-24; 9:17; Za 83:9; Isa 9:4; 10:26; Hab 3:7; Ay 2:11Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. 3Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi. 425:4 Isa 60:6Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura.

525:5 Mwa 24:36Abrahamu akamwachia Isaki kila kitu alichokuwa nacho. 625:6 Mwa 22:24; 21:10; Amu 6:3, 33; 1Fal 4:30; Eze 25:4Lakini Abrahamu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki.

725:7 Mwa 12:4; 35:28; 47:9, 28; 50:22; Ay 42:16Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175. 825:8 Mwa 35:29; 49:29; Hes 20:24; 31:2; Kum 31:14; 32:50; 34:5Ndipo Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku, naye akakusanywa pamoja na watu wake. 925:9 Mwa 35:29; 47:30; 49:31; 23:9; 13:18; 50:13Watoto wake Isaki na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, 1025:10 Mwa 10:15Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara. 1125:11 Mwa 12:2; 16:14Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu akambariki mwanawe Isaki, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi.

Wana Wa Ishmaeli

1225:12 Mwa 2:4; 17:20; 21:18Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu.

1325:13 Mwa 28:9; 36:3; Za 120:5; Isa 21:16; 42:11; 60:7; Yer 2:10; 49:28; Eze 27:21Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 1425:14 Yos 15:25; Oba 1:1; Isa 21:11Mishma, Duma, Masa, 1525:15 Ay 6:19; Isa 21:14; Yer 25:23; 1Nya 5:19Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. 1625:16 Mwa 17:20; 13:16; Za 83:9Hawa walikuwa wana wa Ishmaeli na haya ni majina ya viongozi wa makabila kumi na mawili kulingana na makao yao na kambi zao. 17Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake. 1825:18 Mwa 17:20; 21:18; 16:7, 12Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, unapoelekea Ashuru. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote.

Yakobo Na Esau

19Hivi ndivyo vizazi vya Isaki mwana wa Abrahamu.

Abrahamu akamzaa Isaki, 2025:20 Mwa 26:34; 48:7; 35:28; 24:67; 22:22; 28:2-6; 30:20; 31:18; 33:18; 46:15; 24:29; Kum 26:5Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu.

2125:21 Mwa 30:17, 22; 11:30; Ezr 8:23; 1Sam 1:17, 23; 1Nya 5:20; 2Nya 33:13; Za 127:3Isaki akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. 2225:22 Kut 18:15; 28:30; 33:7; Law 24:12; Hes 9:6-8; 27:5; Kum 17:9; 2Fal 3:11; 22:13; Isa 30:2; Yer 21:2; 37:7; Eze 14:7; 2Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Bwana.

23Bwana akamjibu,

“Mataifa mawili yamo tumboni mwako,

na mataifa hayo mawili

kutoka ndani yako watatenganishwa.

Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine,

na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”

24Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. 25Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau.25:25 Esau maana yake Mwenye nywele nyingi. 26Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo.25:26 Yakobo maana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji, au Mwenye hila, au Mlaghai, au Mjanja. Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.

27Watoto wakakua, naye Esau akakuwa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, wakati Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. 28Isaki, ambaye alikuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.

29Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. 30Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)25:30 Edomu maana yake Mwekundu.

31Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”

32Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu ya kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?”

33Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya kuzaliwa.

34Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake.

Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.