Mwanzo 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 24:1-67

Isaki Na Rebeka

124:1 Mwa 17:17; Yos 23:1; Mwa 12:2; Gal 3:9Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, naye Bwana alikuwa amembariki katika kila njia. 224:2 Mwa 15:3; 39:4-6; 47:29Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu, 324:3 Mwa 10:15-19; 47:31; 50:25; 14:19; Hes 20:14; 2Kor 6:14-17Ninataka uape kwa Bwana, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao, 424:4 Mwa 12:1; 21:21; Amu 14:3bali utakwenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaki mwanangu mke.”

524:5 Ebr 11:15Yule mtumishi akamuuliza, “Je, kama huyo mwanamke atakataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimpeleke mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?”

6Abrahamu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko. 724:7 Mwa 12:1, 7; 16:7; Rum 4:15; Gal 3:16Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa nyumbani kwa baba yangu na nchi yangu niliyozaliwa na aliyesema nami na akaniahidi kwa kiapo, akisema, ‘Nitawapa watoto wako nchi hii,’ atatuma malaika wake akutangulie ili umpatie mwanangu mke kutoka huko. 824:8 Yos 2:12-20; 9:20Kama huyo mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi utafunguliwa kutoka kiapo nilichokuapisha. Ila usimrudishe mwanangu huko.” 924:9 Mwa 32:4; 33:8Basi yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la bwana wake Abrahamu akamwapia kuhusu shauri hili.

1024:10 1Fal 10:2; 1Nya 12:40; Isa 30:6; Mwa 11:29; 43:11; 45:25; Hes 23:7; Kum 23:4; Amu 3:8Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu24:10 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. na kushika njia kwenda mji wa Nahori. 1124:11 Kut 2:15-16; 1Sam 9:11; Yn 4:7; Mwa 29:2, 9-10Akawapigisha ngamia magoti karibu na kisima cha maji nje ya mji, ilikuwa inaelekea jioni, wakati ambapo wanawake wanakuja kuteka maji.

1224:12 Mwa 19:19; 26:24; 27:20; 28:13; 31:42, 53; 32:9; 43:23; 46:3; Kut 3:6; 1Fal 18:36; Za 75:9; 94:7; Neh 1:11; Yos 2:12; Ay 10:12Kisha akaomba, “Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nipatie ushindi leo, uonyeshe huruma kwa bwana wangu Abrahamu. 13Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji. 1424:14 Amu 6:17, 37; 1Sam 14:10; 1Fal 13:3; Za 86:17; Isa 38:7; Yer 44:29Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaki. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu.”

1524:15 Mwa 22:22-23; 11:29Ikawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti wa Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Abrahamu. 1624:16 Mwa 12:11; Kum 22:15-21Huyu msichana alikuwa mzuri sana wa sura, bikira, ambaye hakuna mtu aliyekuwa amekutana naye kimwili. Aliteremka kisimani, akajaza mtungi wake akapanda juu.

1724:17 1Fal 17:10; Yn 4:7Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye akamwambia, “Tafadhali nipe maji kidogo katika mtungi wako.”

18Yule msichana akasema, “Kunywa, bwana wangu.” Akashusha kwa haraka mtungi mkononi mwake na akampa, akanywa.

19Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, “Nitateka maji kwa ajili ya ngamia zako pia mpaka wote watosheke.” 20Akafanya haraka kumimina maji kwenye birika ya kunyweshea wanyama, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na akateka ya kuwatosha ngamia wake wote. 21Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama Bwana ameifanikisha safari yake, au la.

2224:22 Mwa 41:42; Isa 3:21; Eze 16:11-12Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja24:22 Beka moja ya dhahabu ni sawa na gramu 5.5. na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.24:22 Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110. 2324:23 Amu 19:15; 20:4Kisha akamuuliza, “Wewe ni binti wa nani? Tafadhali uniambie, je, kuna nafasi katika nyumba ya baba yako tutakapoweza kulala?”

2424:24 Mwa 11:29Yule msichana akamjibu, “Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Milka aliyemzalia Nahori.” 2524:25 Amu 19:19Akaendelea kusema, “Kwetu kuna majani mengi na malisho, tena kuna nafasi kwa ajili yenu kulala.”

2624:26 Kut 4:31; 12:27; 1Nya 29:20; 2Nya 20:18Yule mtumishi akasujudu na kumwabudu Bwana, 2724:27 Mwa 14:20; 32:10; 47:29; Kut 18:20; Rut 4:14; 1Sam 25:32; 2Sam 18:28; 1Fal 8:56; Za 28:6; 41:13; 68:19; 98:3; 106:48; Yos 2:14; Lk 1:68akisema, “Atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, Bwana ameniongoza safarini akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu.”

2824:28 Mwa 29:12Yule msichana akakimbia akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya. 2924:29 Mwa 25:20; 27:43; 28:2-5; 29:5, 12-13Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani, huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani. 3024:30 Eze 23:42Mara alipoiona ile pete puani, na bangili mikononi mwa dada yake na kusikia yale maneno Rebeka aliyoambiwa na huyo mtumishi, alimwendea huyo mtumishi, akamkuta amesimama karibu na ngamia wake pale karibu na kisima. 3124:31 Mwa 26:29; Rut 3:10; Za 115:15Akamwambia, “Karibu nyumbani wewe uliyebarikiwa na Bwana, kwa nini unasimama huko nje? Mimi nimekuandalia nyumba na mahali kwa ajili ya ngamia.”

3224:32 Mwa 18:4; Amu 19:21Hivyo yule mtumishi akaenda nyumbani, mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu. 33Ndipo chakula kikaandaliwa kwa ajili yake, lakini akasema, “Sitakula mpaka niwe nimewaambia yale niliyo nayo ya kusema.”

Labani akasema, “Basi tuambie.”

3424:34 Mwa 15:3Hivyo akasema, “Mimi ni mtumishi wa Abrahamu. 3524:35 Mwa 12:2, 16; 23:6Bwana amembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ngʼombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda. 3624:36 Mwa 17:17; 25:5; 26:14Sara mkewe bwana wangu amemzalia mwana katika uzee wake, naye amempa kila kitu alichokuwa nacho. 3724:37 Mwa 50:5Naye bwana wangu ameniapisha na akasema, ‘Kamwe usimtwalie mwanangu mke katika binti za Wakanaani, ambao ninaishi katika nchi yao, 3824:38 Mwa 21:21ila uende mpaka kwa jamaa ya baba yangu na ukoo wangu mwenyewe, ukamtwalie mwanangu mke huko.’

39“Kisha nikamuuliza bwana wangu, ‘Je, kama huyo mwanamke hatakubali kurudi nami?’

4024:40 Mwa 5:22; 12:1; 16:7“Akanijibu, ‘Bwana ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka jamaa ya baba yangu. 41Kisha, utakapokwenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu hata kama wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’

42“Nilipokuja kisimani leo nilisema, ‘Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ikikupendeza, naomba uifanikishe safari niliyoijia. 4324:43 Mit 30:19; Isa 7:14Tazama, ninasimama kando ya kisima hiki, kama mwanamwali akija kuteka maji nami nikimwambia, tafadhali niruhusu ninywe maji kidogo kutoka kwenye mtungi wako, 44naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambaye Bwana amemchagulia mwana wa bwana wangu.’

4524:45 1Sam 1:13; Yn 4:7“Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, amebeba mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ninywe.’

46“Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa na nitawanywesha ngamia wako pia,’ basi nikanywa, akawanywesha na ngamia pia.

4724:47 Mwa 22:22; Isa 3:19; Eze 16:11-12“Nikamuuliza, ‘Wewe ni binti wa nani?’

“Akasema, ‘Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia.’

“Ndipo nilipotia pete puani mwake na bangili mikononi mwake, 48nikasujudu na nikamwabudu Bwana. Nikamtukuza Bwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake. 49Ikiwa mtaonyesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie, la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.”

5024:50 Za 118:23; Mwa 22:22; 31:24-29; 48:16Labani na Bethueli wakajibu, “Jambo hili limetoka kwa Bwana, hatuwezi kukuambia jambo lolote baya au jema. 51Rebeka yuko hapa, mchukue na uende, awe mke wa mwana wa bwana wako, sawasawa na Bwana alivyoongoza.”

52Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu mpaka nchi mbele za Bwana. 5324:53 Mwa 45:22; Kut 3:22; 12:35; 2Fal 5:5Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha pamoja na mavazi, akampa Rebeka, pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye. 5424:54 Mwa 30:25Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala palepale.

Walipoamka asubuhi, yule mtumishi, akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”

5524:55 Amu 19:3-4Lakini ndugu yake Rebeka pamoja na mama yake wakajibu, “Acha binti akae kwetu siku kumi au zaidi, ndipo mwondoke.”

56Lakini yule mtumishi akawaambia, “Msinicheleweshe, kwa kuwa Bwana amefanikisha safari yangu, nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”

57Ndipo wakasema, “Acha tumwite huyo binti tumuulize, tusikie atakavyosema.” 5824:58 Rum 1:16Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?”

Akasema, “Nitakwenda.”

5924:59 Mwa 35:8Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake. 6024:60 Mwa 17:16; 22:17; 27:4; 31:55; 48:9, 15, 20; Yos 22:6; Mit 27:11Wakambariki Rebeka, wakamwambia,

“Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu,

mara elfu nyingi,

nao wazao wako wamiliki

malango ya adui zao.”

6124:61 Mwa 16:1; 30:3; 46:25Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka.

6224:62 Mwa 16:14; 12:9Basi Isaki alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa anaishi nchi ya Negebu. 6324:63 Za 77:12; 119:15, 27; 143:5; 145:5; Mwa 18:2Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja. 6424:64 Mwa 31:17, 34; 1Sam 30:17Rebeka pia akainua macho akamwona Isaki. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake 6524:65 Mwa 38:14; Wim 4:1-3; 6:7; Isa 47:2na akamuuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule aliye kule shambani anayekuja kutulaki?”

Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.

66Kisha yule mtumishi akamweleza Isaki mambo yote aliyoyatenda. 6724:67 Mwa 31:33; 18:9; 25:20; 49:31; 29:18-20; 23:1-2; 34:3; Amu 16:4Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.