Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 23:1-20

Kifo Cha Sara

1Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba. 223:2 Yos 14:15; 15:13; 20:7; 21:11; Mwa 13:18; 24:67Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara.

323:3 Mwa 10:15Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema, 423:4 Mwa 17:8; 19:9; 49:30; Kut 2:22; Law 25:23; Za 39:12; 105:12; 119:19; Ebr 11:9-13; Mdo 7:16“Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.”

5Wahiti wakamjibu Abrahamu, 623:6 Mwa 14:14-16; 24:35; 25:9“Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.”

7Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti. 8Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu 923:9 Mwa 25:9; 47:30; 49:30; 50:13ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.”

1023:10 Kum 22:15; 25:7; Yos 20:4; Rut 4:11; 2Sam 15:2; 2Fal 15:35; Za 127:5; Mit 31:23; Yer 26:10; 6:10Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji. 1123:11 2Sam 24:23“La hasha, bwana wangu, nisikilize, nakupa shamba, pia nakupa pango lililomo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu. Uzike maiti wako.”

12Abrahamu akasujudu tena, mbele ya wenyeji wa nchi, 13akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.”

14Efroni akamjibu Abrahamu, 1523:15 Eze 45:12“Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha,23:15 Shekeli 400 za fedha ni sawa na kilo 4.5. lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”

1623:16 2Sam 14:26; 24:24; Yer 32:9; Zek 11:12Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.

1723:17 Mwa 13:18Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwamo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa, 1823:18 Mwa 18:1, 7kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. 1923:19 Mwa 13:18; Yos 14:13; 1Nya 29:27; 23:20; Yer 32:10; Mwa 10:15; 35:29; 49:30, 31; 50:5Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani. 20Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 23:1-20

亞伯拉罕買地葬撒拉

1撒拉享年一百二十七歲, 2迦南境內的基列·亞巴,即希伯崙去世。亞伯拉罕在那裡痛哭,哀悼她。 3他從妻子屍體旁邊站起來對人說: 4「我是寄居在你們這裡的異鄉人,請你們給我一塊地,我好埋葬我的亡妻。」 5人回答說: 6「我主,請聽我們說,你在我們中間是一位尊貴的王子,你可以選我們這裡最好的墳地,沒有人會反對你使用他的墳地埋葬你的妻子。」 7亞伯拉罕就向他們下拜,說: 8「如果你們真的准我安葬妻子,就請你們代我求瑣轄的兒子以弗崙9請他當著你們的面,把他田地盡頭的麥比拉洞按實價賣給我作墳地。」

10當時以弗崙正坐在人當中,於是他在城門口人聚集的地方當眾答覆亞伯拉罕說: 11「不可!我主,請聽我說,我當著族人的面,把那塊地和山洞送給你,你只管去安葬你的妻子!」 12亞伯拉罕向當地的人下拜, 13當眾對以弗崙說:「你若願意,請聽我說,我要把地錢給你,請你收下,好讓我安葬我的妻子。」 14以弗崙回答說: 15「我主,請聽我說,四公斤半銀子的地對你我來說算什麼呢?去安葬你的妻子吧!」 16於是,亞伯拉罕就照以弗崙當眾提出的價錢,按通用的重量單位秤了四公斤半銀子給他。

17這樣,以弗崙麥比拉、靠近幔利的那塊地和山洞及地界內所有的樹木, 18都歸了亞伯拉罕。這是在城門口的人面前買下的。

19之後,亞伯拉罕把妻子撒拉安葬在迦南幔利附近、麥比拉田間的洞裡。幔利就是希伯崙20這塊人的地和其中的山洞從此成了亞伯拉罕家的墳地。