Mwanzo 22 – NEN & HTB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 22:1-24

Kujua Uthabiti Wa Abrahamu

122:1 Kut 15:25; 16:4; 20:20; Kum 8:2, 16; 13:3; Amu 2:22; 3:1; 2Nya 32:31; Za 66:10; Ebr 11:17; Yak 1:12-13; Mwa 31:11; 46:2; 1Sam 3:4-8; Isa 6:8Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”

Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”

222:2 Yn 3:16; Ebr 11:17; 1Yn 4:9; Mwa 8:20Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

322:3 Yos 8:10Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. 4Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. 522:5 Kut 24:14Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.”

622:6 Yn 19:17; Amu 19:29Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 722:7 Kut 29:38-42; Law 1:10; Ufu 13:8Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”

Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”

Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”

822:8 Yn 1:29Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

922:9 Mwa 4:26; 8:20; Law 1:7; 1Fal 18:33; Ebr 11:17-19; Yak 2:21Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 1022:10 Mwa 18:19Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 1122:11 Mwa 16:7; 21:17; 46:2Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

1222:12 Mwa 18:19; 42:18; Kut 18:21; 1Sam 15:22; Ay 1:1; 37:24; Mit 8:13; Yak 2:21-23; Yn 3:16; 1Yn 4:9Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

1322:13 Mwa 8:20; Rum 8:32Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 1422:14 Kut 17:15; Amu 6:24; Isa 30:29Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.22:14 Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

1522:15 Mwa 21:17Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 1622:16 Kut 13:11; 32:13; 33:1; Isa 45:23; 62:8; Yer 22:5; 44:26; 49:13; 51:14; Amo 6:8; Ebr 6:13; Lk 1:73akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, 1722:17 Mwa 12:2; 15:5; 26:24; 24:60; Ebr 6:14; Kut 32:13; Kum 7:7; 28:62; Hos 1:10; Rum 9:27; Ebr 11:12; Es 9:2hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, 1822:18 Mwa 12:2-3; 17:2, 9; Mdo 3:25; Gal 3:8; Za 105:9na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”

1922:19 Mwa 21:14; 26:23; 28:10Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.

Wana Wa Nahori

2022:20 Mwa 11:29Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 2122:21 Mwa 10:23; Ay 32:2; Yer 25:23Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 2222:22 Mwa 24:15, 47; 25:20Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 2322:23 Mwa 24:15; 11:29Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane. 2422:24 Mwa 25:6; 35:22; 36:12; Amu 8:31; 2Sam 3:7; 1Fal 2:22; 11:3; 1Nya 1:32; Wim 6:8Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

Het Boek

Genesis 22:1-24

Abrahams geloof op de proef gesteld

1Enige tijd later stelde God Abraham op de proef. ‘Abraham!’ zei God. ‘Ja Here, hier ben ik,’ antwoordde Abraham. 2‘Neem uw zoon, uw enige, van wie u zoveel houdt, Isaak, ga naar het land Moria en offer hem daar als een brandoffer aan Mij. De plaats waar u dat moet doen, zal Ik u wijzen.’

3De volgende morgen stond Abraham vroeg op, zadelde zijn ezel, nam twee knechten mee en zijn zoon Isaak. Hij hakte hout voor het offer en ging op weg naar de plaats die God had genoemd. 4Na drie dagen reizen zag Abraham in de verte de plaats die God hem had gezegd. 5‘Jullie blijven hier bij de ezel,’ beval hij de twee dienaren, ‘ik en de jongen gaan daarheen om te aanbidden. Daarna komen wij hier terug.’ 6Abraham liet Isaak het hout voor het offervuur dragen en nam zelf het mes en het vuur. Zo liepen zij samen verder.

7‘Vader,’ zei Isaak. ‘Wat is er, mijn jongen?’ vroeg Abraham. ‘We hebben hout en het vuur,’ zei Isaak, ‘maar waar is het lam dat wij moeten offeren?’ 8‘God zal Zelf voor een offerlam zorgen, jongen,’ antwoordde Abraham. En weer gingen zij samen verder. 9Toen zij aankwamen op de plaats die God Abraham had aangewezen, bouwde Abraham een altaar en stapelde het hout erop. Toen bond hij Isaak vast en legde hem op het altaar, op het hout. 10Hij pakte het mes en hief zijn arm op om zijn zoon te doden. 11Op dat moment riep de Engel van de Here uit de hemel: ‘Abraham, Abraham!’ ‘Ik luister,’ antwoordde Abraham. 12‘Leg het mes weg en laat de jongen ongemoeid,’ zei de Engel. ‘Ik weet nu dat God de belangrijkste is in uw leven. Zelfs uw eigen zoon, uw enige, van wie u zoveel houdt, wilde u Mij geven.’

13Abraham keek rond en zag vlakbij een ram, die met zijn horens in de struiken vastzat. In plaats van zijn zoon offerde hij die ram als een brandoffer op het altaar. 14Abraham noemde die plaats ‘De Here voorziet erin.’ Daarom wordt ook nu nog gezegd: ‘Op de berg van de Here zal Hij voorzien.’

15Toen sprak de Engel van de Here opnieuw tegen Abraham vanuit de hemel. 16-17 ‘Ik, de Here, heb Mijzelf gezworen dat Ik u en uw nageslacht rijk zal zegenen, omdat u Mij hebt gehoorzaamd en Mij zelfs uw enige zoon wilde geven. Uw nakomelingen zullen net zo talrijk zijn als de sterren aan de hemel en het zand langs de zee. 18Zij zullen hun vijanden overwinnen en een zegen zijn voor alle volken van de wereld en dat alles, omdat u Mij hebt gehoorzaamd.’ 19Abraham keerde terug naar zijn twee dienaren en samen gingen ze terug naar Berseba, hun woonplaats.

20Enige tijd later kreeg Abraham bericht dat Milka, de vrouw van zijn broer Nachor, haar man acht zonen had gegeven. Us, de oudste, Buz, de op een na oudste, Kemuël (de vader van Aram), Kesed, Chazo, 21-24Pildas, Jidlaf en Betuël (de vader van Rebekka). Nachor kreeg ook nog vier zonen van zijn bijvrouw Reüma: Tebach, Gacham, Tachas en Maächa.