Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 21:1-34

Kuzaliwa Kwa Isaki

121:1 Mwa 17:20; 1Sam 2:21; Mwa 8:1; 17:6; 18:14; 4:23; Ebr 11:11Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 221:2 Mwa 17:19; 30:6; 18:10; Gal 4:22; Ebr 11:11Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 321:3 Mwa 16:11; Yos 24:3Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 421:4 Mwa 17:10-12; Mdo 7:8Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 521:5 Mwa 12:4; Ebr 6:15Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.

621:6 Mwa 17:17; Ay 8:21; Za 126:2; Isa 12:6; 35:2; 44:23; 52:9; 54:1Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” 721:7 Mwa 17:17Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.”

Hagari Na Ishmaeli Wafukuzwa

821:8 1Sam 1:23Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaki alipoachishwa kunyonya, Abrahamu alifanya sherehe kubwa. 921:9 Mwa 16:15; 39:14; Gal 4:29Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki, 1021:10 Mwa 39:17; 25:6; Gal 4:30Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyo mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwanangu Isaki.”

1121:11 Mwa 17:18Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe. 1221:12 Mt 1:2; Rum 9:7; Ebr 11:18Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki. 1321:13 Mwa 13:16Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”

1421:14 Mwa 16:1; 22:19; 26:33; 28:10; 46:1-5; Yos 15:28; 19:2; Amu 20:1; 1Sam 3:20; 1Nya 4:28; Neh 11:27Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.

15Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka. 1621:16 Yer 6:26; Amo 8:10; Zek 12:10Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.

1721:17 Kut 3:7; Hes 20:16; Za 6:8; Kum 26:7; Mwa 16:7; 22:11, 15; 15:1; 17:20Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale. 18Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.”

1921:19 Hes 22:31; Mwa 16:7Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.

2021:20 Mwa 26:3, 24; 28:15; 39:2; Lk 1:66Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. 2121:21 Mwa 14:6; 24:4, 38; 28:2; 34:4-8; Amu 14:2Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.

Mapatano Katika Beer-Sheba

2221:22 Mwa 20:2; 26:26-28; 28:15; 31:3-5, 42; 39:2-3; Za 46:7; 1Sam 3:19; 16:18; Isa 7:14; 8:8-10; 41:10; 43:5Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 2321:23 Mwa 25:33; 26:31; 31:53; Yos 2:12; 1Fal 2:8; 1Sam 24:21Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”

24Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

2521:25 Mwa 26:15-22Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. 26Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”

2721:27 Mwa 26:28-31; 31:44, 53Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. 28Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi, 29Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?”

3021:30 Mwa 31:44-52; Isa 19:20; Yos 22:27-34; 24:27; Mal 2:14Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.”

31Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.

3221:32 Mwa 10:14; 26:33Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti. 3321:33 1Sam 22:6; 31:13; Mwa 4:26; Kut 15:18; Kum 32:40; 33:27; Ay 36:26; Za 10:16; 45:6; 90:2; 93:2; 102:24; 103:19; 146:10; Isa 40:28; Yer 10:10; Hab 1:12; 3:6; Ebr 13:8Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la Bwana, Mungu wa milele. 3421:34 Mwa 10:14Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 21:1-34

以撒出生

1耶和华按着自己说过的话眷顾撒拉,实现给她的应许。 2亚伯拉罕年老的时候,撒拉怀了孕,在上帝指定的日期为他生了一个儿子。 3亚伯拉罕为儿子取名叫以撒4以撒出生后第八天,亚伯拉罕就照着上帝的吩咐为他行了割礼。 5以撒出生时亚伯拉罕已经一百岁。 6撒拉说:“上帝使我欢笑,凡听见这事的人也必跟我一同欢笑。 7谁曾料到我会为亚伯拉罕哺养孩子呢?我竟然在丈夫年老的时候给他生了儿子。”

夏甲和以实玛利被逐

8以撒渐渐长大,亚伯拉罕在他断奶的那天摆设宴席。 9撒拉埃及夏甲亚伯拉罕生的儿子以实玛利嘲笑以撒10就对亚伯拉罕说:“赶走这婢女和她的儿子,因为这婢女的儿子不可和我的儿子以撒一同承受产业。” 11亚伯拉罕因儿子以实玛利的事非常烦恼。 12上帝对亚伯拉罕说:“你不要再为这孩子和你的婢女烦恼,只管照撒拉的意思去做,因为以撒生的才可算为你的后代。 13至于那婢女的儿子以实玛利,我也会使他自成一国,因为他也是你的儿子。”

14第二天,亚伯拉罕清早起来,把食物和一皮袋水放在夏甲肩上,让她和孩子离开。夏甲别示巴的旷野流浪。 15皮袋的水喝光了,夏甲把儿子留在一丛灌木下, 16自己走到离孩子约一箭之远的地方,对着孩子坐下,说:“我不忍心看着他死啊!”夏甲坐在那里放声大哭起来。 17上帝听见孩子的哭声,就差遣天使从天上安慰夏甲说:“夏甲,你怎么了?不要害怕,上帝已经听见孩子的哭声了。 18你去扶他起来,安慰他,我必使他成为大国。” 19上帝使夏甲的眼睛明亮,让她看见一口水井,她就上前把皮袋装满水拿给儿子喝。 20在上帝的看顾下,孩子在旷野渐渐长大,成为一个射箭能手。 21他住在巴兰旷野,他母亲为他娶了一个埃及女子。

亚伯拉罕与亚比米勒立约

22有一次,亚比米勒和他的将领非各亚伯拉罕说:“你做的一切都有上帝保佑。 23现在请你在这里当着上帝的面向我起誓,你不会欺骗我和我的子孙后代。我怎样善待你,请你也同样善待我以及你所寄居之地的百姓。” 24亚伯拉罕说:“我愿起誓。”

25由于亚比米勒的仆人霸占了一口水井,亚伯拉罕就指责亚比米勒26亚比米勒说:“我不知道是谁做的,你以前没有告诉我,我今天才听说这事。” 27亚伯拉罕把牛羊送给亚比米勒,他们二人立了约。 28亚伯拉罕又从羊群中分出七只母羊羔。 29亚比米勒亚伯拉罕:“你分出七只母羊羔是什么意思?” 30亚伯拉罕回答说:“你要从我手中接受这七只母羊羔,表示你承认这口井是我挖的。” 31所以,那地方被称为别示巴21:31 别示巴”意思是“盟誓之井”。,因为他们二人在那里起了誓。

32他们立约以后,亚比米勒和他的将领非各便回非利士去了。 33亚伯拉罕别示巴栽了一棵红柳,又在那里呼求耶和华——永恒上帝的名。 34亚伯拉罕非利士住了很长时间。