Mwanzo 20 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 20:1-18

Abrahamu Na Abimeleki

120:1 Mwa 18:1; 12:9; 14:7; 16:7; 26:3Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni, 220:2 Mwa 12:13, 15; 26:1huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua.

320:3 Hes 12:6; 22:9, 20; Mwa 26:11; 28:12; 31:10, 24; 37:5-9; 40:5; 41:1; Kum 13:1; Kut 10:7; 12:33; Ay 33:15; Dan 2:1; 4:5; 1Nya 16:21; Za 105:14, 28Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.”

420:4 Mwa 18:25Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? 520:5 Mwa 12:19; 17:1; Za 7:8; 25:21; 26:6; 41:12Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.”

620:6 1Sam 25:26, 34; Mwa 13:13; Za 41:4; 51:4Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. 720:7 Kum 18:18; 34:10; 2Fal 3:11; 5:3; 1Nya 16:22; Za 105:15; Kut 8:8; Hes 11:2; 12:13; 1Sam 7:5; 1Fal 13:6; Ay 42:8; Yer 18:20; 37:3; 42:2; Za 9:5Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.”

8Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana. 920:9 Mwa 12:18; 34:7Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” 10Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?”

1120:11 Mwa 12:12; 31:31; 42:18; Neh 5:15; Ay 31:23; Za 36:1; Mit 16:6Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ 1220:12 Mwa 12:13Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. 1320:13 Kum 26:5; 1Nya 16:20; Isa 30:28; 63:17; Mwa 12:1Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ”

1420:14 Mwa 12:16Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ngʼombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe. 1520:15 Mwa 13:9; 45:18Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.”

16Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.”

1720:17 Ay 42:9Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena, 1820:18 Mwa 12:17kwa kuwa Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya wote katika nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya Sara, mke wa Abrahamu.