Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 19:1-38

Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora

119:1 Mwa 11:27; 17:3; 18:1, 2, 22; 48:12; Rut 2:10; 1Sam 25:23; 2Sam 14:33; 2Fal 2:15; Ebr 13:2Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini. 219:2 Mwa 18:4; Lk 7:44; Amu 19:15, 20Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.”

Wakamjibu, “La hasha, tutalala hapa nje uwanjani.”

319:3 Mwa 18:6; 33:11; Ay 31:32; Kut 12:39Lakini akasisitiza kwa nguvu kwamba waingie pamoja naye nyumbani kwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala. 419:4 Mwa 13:13Kabla hawajaenda kulala, watu wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba. 519:5 Mwa 13:13; Law 18:22; Kum 23:18; Amu 19:22; Rum 1:24-27Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”

619:6 Amu 19:23Loti akatoka nje kuonana nao, akaufunga mlango nyuma yake, 7akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu. 819:8 Amu 19:24; 2Pet 2:7-8Tazama, ninao binti wawili ambao kamwe hawajakutana kimwili na mwanaume. Acha niwatoe nje kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lolote mnalotaka. Lakini msiwafanyie chochote watu hawa, kwa sababu wako kwenye ulinzi chini ya dari langu.”

919:9 Mwa 13:8; 23:4; Mdo 7:27Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Loti na kusonga mbele ili kuvunja mlango.

1019:10 Mwa 18:2Lakini watu wale waliokuwa ndani wakanyoosha mkono wakamvuta Loti ndani ya nyumba na kufunga mlango. 1119:11 Kum 28:28-29; 2Fal 6:18; Mdo 13:11Kisha wakawapiga kwa upofu wale watu waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango.

1219:12 Mwa 6:18; 7:1Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, 1319:13 Kut 12:29; 2Sam 24:16; 2Fal 19:35; 1Nya 21:12, 15; 2Nya 32:21; Mwa 18:20; Za 78:49; Yer 21:12; 25:18; 44:22; 51:45kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa Bwana dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.”

1419:14 Hes 16:21; Ufu 18:4; Kut 9:21; 1Fal 13:18; Yer 5:12; 43:2; Lk 17:28Kwa hiyo Loti alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa Bwana yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania.

1519:15 Hes 16:26; Ay 21:18; Za 58:9; 73:19; 90:5; Ufu 18:4Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.”

1619:16 2Pet 2:7; Kut 34:6; Za 33:8-9Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa Bwana alikuwa na huruma kwao. 1719:17 1Fal 19:3; Yer 48:6; Mwa 13:12; 14:10; Mt 24:16Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!”

18Lakini Loti akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini! 1919:19 Mwa 6:8; 18:3; 24:12; 39:21; 40:14; 47:29; Rut 1:8; 2:20; 3:10Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa. 20Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.”

2119:21 1Sam 25:35; 2Sam 14:8; Ay 42:9Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. 2219:22 Mwa 13:10Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.19:22 Soari maana yake Mdogo.)

2319:23 Mwa 13:10Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. 2419:24 Ay 18:15; Za 11:6; Isa 30:33; 34:9; Eze 38:22; Kum 29:23; Isa 1:9; 13:19; Yer 49:18; 50:40; Amo 4:11; Mwa 18:17; Law 10:2; Mt 10:15; Lk 17:29; Yud 7Ndipo Bwana akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa Bwana juu ya Sodoma na Gomora. 2519:25 Eze 16:48; 26:16; Sef 3:8; Hag 2:22; Mwa 13:12; Za 107:34; Isa 1:10; Yer 20:16; 23:14; Mao 4:6Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi. 2619:26 Lk 17:32Lakini mke wa Loti akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi.

2719:27 Mwa 18:22Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za Bwana. 2819:28 Mwa 15:17; Kut 19:18; Ufu 9:2, 18Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru.

2919:29 Mwa 8:1; 13:12; 14:12; Eze 14:16; 2Pet 2:7Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Loti kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Loti alikuwa ameishi.

Loti Na Binti Zake

3019:30 Mwa 13:10; 14:10Loti na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. 31Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. 3219:32 Mwa 16:2; 38:18Tumnyweshe baba yetu mvinyo kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.”

33Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo, alipolewa binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua wakati binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka.

34Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” 3519:35 Mwa 9:21Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka.

36Hivyo binti wawili wa Loti wakapata mimba kwa baba yao. 3719:37 Mwa 36:35; Kut 15:15; Hes 25:1; Isa 15:1; 25:10; Yer 25:21; 48:1; Eze 25:8; Sef 2:9; Hes 22:4; 24:17; Rut 1:4, 22; 1Sam 14:47; 22:3-4; 2Sam 8:2; 2Fal 3:4; Ezr 9:1; Za 108:9Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina lake Moabu; ndio baba wa Wamoabu hata leo. 3819:38 Hes 21:24; Kum 2:19; 23:3; Yos 12:2; Amu 3:13; 10:6-7; 1Sam 11:1-11; 14:47; 1Nya 19:1; 2Nya 20:23; 26:8; 27:5; Neh 2:19; 4:3; Yer 25:21; 40:14; 49:1; Eze 21:28; 25:2; Amo 1:13Binti mdogo naye pia akamzaa mwana, naye akamwita Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

创世记 19:1-38

上帝毁灭所多玛和蛾摩拉

1那两个天使在黄昏的时候来到所多玛罗得正坐在城门口,看见他们,便起来迎接,俯伏在地上说: 2“我主啊,请到仆人家洗洗脚,住一夜,明天早上再继续赶路吧!”他们说:“不,我们要在街上过夜。” 3罗得执意邀请他们,他们便答应到他家里作客。罗得设宴款待他们,烤无酵饼给他们吃。 4他们正准备就寝的时候,所多玛城的男人从老到少全都出来,团团围住罗得的房子, 5罗得大喊大叫:“今天晚上到你家中作客的人在哪里?把他们交出来,我们要跟他们性交!” 6罗得走出来,关上门,到众人面前, 7对他们说:“各位弟兄,请不要做这种邪恶的事! 8我有两个女儿,还是处女,我愿意把她们交出来任凭你们处置,只是请你们不要侮辱这两个人,他们是我家里的客人。” 9他们对罗得说:“走开!”又说:“这个寄居的人竟当起审判官来啦!现在我们要用更狠的手段对付你。”众人便推挤罗得,想要破门而入。 10那两位天使伸手把罗得拉进屋里,关上了门, 11并让门外的人,不论老少都眼目昏花,摸来摸去也找不着罗得家的门。

12天使对罗得说:“你还有什么亲人住在这里?你要带儿女、女婿和城里其他亲人离开这里, 13因为我们就要毁灭这城了。耶和华已经听见控诉这罪恶之城的声音,祂差遣我们来毁灭这城。” 14罗得听了就去通知他女儿的未婚夫说:“快走吧!耶和华要毁灭这城了!”可是他们却以为他是在开玩笑。

15天刚亮的时候,天使便催促罗得说:“起来,带着你的妻子和两个女儿离开,免得所多玛城因罪恶受惩罚的时候,你也一起被毁灭。” 16罗得却犹疑不决,天使便拉着罗得及其妻子和两个女儿的手出去,将他们安置在城外,因为耶和华怜悯他们。 17到了城外,其中一位天使说:“赶快逃!不要回头看,也不要留在平原,要往山上逃,免得你们被毁灭。” 18罗得说:“我主啊,请不要这样。 19仆人蒙你厚爱、施恩相救,但我无法逃到山上,要是这灾难追上我,我就没命了! 20请看,那座城离这里不远,容易跑到,又是座小城,请让我逃到那座小城活命吧!” 21天使回答说:“好吧,我答应你,不毁灭那座小城。 22你赶快逃吧,因为你还没有到那里之前,我不能动手。”从此那城便叫琐珥19:22 琐珥”意思是“小”。

23罗得到达琐珥的时候,太阳已经出来了。 24耶和华从天上把燃烧的硫磺降在所多玛蛾摩拉两地, 25毁灭了这两座城和其中的居民,包括整个平原和地上的植物。 26罗得的妻子跟在后面,她回头一望,就变成了一根盐柱。

27亚伯拉罕清早起来,走到他从前站在耶和华面前的地方, 28所多玛蛾摩拉和整个平原眺望,只见那里浓烟滚滚,好像火窑的烟一样。

29这样,为了亚伯拉罕的缘故,上帝毁灭平原各城的时候,让罗得逃离所住的城市,不致丧命。

罗得与他的女儿

30罗得不敢住在琐珥,便带着两个女儿来到山上,住进一个洞里。 31他的大女儿对妹妹说:“我们的父亲年纪大了,这里又没有男子可以照着世上的习俗娶我们。 32不如我们灌醉父亲,然后跟他睡觉,借着他替我们一家传宗接代吧。” 33于是,那晚她们灌醉了父亲,大女儿进去和父亲睡。她什么时候躺下,什么时候起来,罗得完全不知道。 34第二天,大女儿对妹妹说:“昨天晚上我已经和父亲睡了,今天晚上我们再灌醉他,你可以进去和他睡。这样,我们就可以借着父亲传宗接代。” 35当天晚上,她们又灌醉了罗得,小女儿进去与他睡。她什么时候躺下,什么时候起来,罗得完全不知道。 36这样,罗得的两个女儿都从父亲怀了孕。 37大女儿生了一个儿子,给他取名叫摩押19:37 摩押”意思是“出自父亲”。,他是今天摩押人的祖先。 38小女儿也生了一个儿子,给他取名叫便·亚米19:38 便·亚米”意思是“亲人的儿子”。,他是今天亚扪人的祖先。