Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mwanzo 18:1-33

Wageni Watatu

118:1 Mwa 12:7; 13:18; 14:13; 19:1; 23:10, 18; 34:20-24; Rut 4:1; Ebr 11:9; Za 69:12Bwana akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. 218:2 Mwa 17:2-3; 19:1, 10; 24:63; 32:24; 43:28; Yos 5:13; Ebr 13:2; Amu 13:6-11; Hos 12:2-4Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

3Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 418:4 Mwa 19:2; 24:32; 43:24; Amu 19:21; 2Sam 11:8; Lk 7:44Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 518:5 Amu 13:15; 19:5Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.”

Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”

618:6 Mwa 19:3; 2Sam 13:8Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.”

718:7 1Sam 28:24; Lk 15:23Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye kundi, akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha. 818:8 Isa 7:15, 22; Amu 4:19; 5:25; 6:19Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti.

918:9 Mwa 3:9; 24:67; Ebr 11:9Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?”

Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.”

1018:10 Mwa 17:6, 21; 21:2; 2Fal 4:16; Rum 6:6Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.”

Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake. 1118:11 Mwa 11:30; 17:17; Lk 1:18; Rum 4:19; Ebr 11:11-12Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 1218:12 Mwa 17:17; 21:6; 1Pet 3:6Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”

1318:13 Mwa 17:17Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ 1418:14 Ay 42:2; Isa 40:29; 50:2; 51:9; Gal 4:23; Yer 32:17; Mt 19:26; Rum 4:21; 9:9; Mwa 17:19Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”

15Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”

Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”

Abrahamu Aiombea Sodoma

16Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize. 1718:17 Amo 3:7; Mwa 19:24; Ay 1:16; Za 107:34Ndipo Bwana akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya? 1818:18 Mwa 12:2; Gal 3:8Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. 1918:19 Mwa 16:11; 17:9; 22:12, 18; 26:5; Kum 4:9-10; 6:7; Isa 14:1; Efe 6:4; Yos 24:15; Yer 23:5; 2Sam 8:15; Za 17:2; 99:4Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”

2018:20 Isa 1:10; Yer 23:14; Eze 16:46; Mwa 13:13; 19:13Basi Bwana akasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana, 2118:21 Mwa 11:5kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.”

2218:22 Mwa 19:1, 27Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele za Bwana. 2318:23 Kut 23:7; 2Pet 2:9; Law 4:3, 22, 27; Hes 16:22; Eze 18:4; Kum 27:25; 2Sam 24:17; Za 11:4-7; 94:21Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu? 2418:24 Yer 5:1Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake? 2518:25 Mwa 20:4; 44:7; Kum 32:4; 1:16-17; Rum 3:6; Ay 8:3-7; 9:15; 34:10; 36:23; Isa 3:10-11; 5:20; Amo 5:15; Mal 2:17; 3:18; Amu 11:27; Za 7:11; 58:11; 75:7; 94:2; 119:137; Ebr 12:23; 2Nya 19:7; Ezr 9:15; Neh 9:33; Eze 18:25; Dan 4:37; 9:14Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”

26Bwana akasema, “Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao.”

2718:27 Mwa 2:7; Ay 2:8Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu; 28je, kama hesabu ya wenye haki imepungua watano katika hamsini, utauangamiza huo mji wote kwa ajili ya hao watano waliopungua?”

Bwana akamwambia, “Kama nikiwakuta huko watu arobaini na watano, sitauangamiza.”

29Abrahamu akazungumza naye kwa mara nyingine, “Je, kama huko watapatikana watu arobaini tu?”

Akamjibu, “Kwa ajili ya hao arobaini, sitauangamiza.”

3018:30 Mwa 44:18; Kut 32:22Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?”

Akajibu, “Sitapaangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.”

31Abrahamu akasema, “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri sana kuzungumza na Bwana, je, kama wakipatikana huko watu ishirini tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.”

3218:32 Amu 6:39; Yer 5:1Abrahamu akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze tena mara moja tu. Itakuwaje kama watapatikana huko watu kumi tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao kumi, sitauangamiza.”

3318:33 Kut 31:18; Mwa 17:22; 31:55Bwana alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, akaondoka, naye Abrahamu akarudi nyumbani kwake.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

創世記 18:1-33

上帝應許撒拉生子

1耶和華在幔利的橡樹那裡向亞伯拉罕顯現。那時天氣很熱,亞伯拉罕坐在帳篷口, 2抬頭看見三個人站在對面,就跑去迎接他們,俯伏在地, 3說:「我主,你們若肯賞光,請不要匆匆路過僕人這裡。 4我讓人拿點水來,你們洗洗腳,在樹下歇一會兒。 5我拿點餅來,你們補充一下體力再上路吧。你們既然路過這裡,我理應招待你們。」他們說:「好,就照你說的做吧!」

6於是,亞伯拉罕連忙進帳篷對撒拉說:「快準備三斗18·6 三斗」希伯來文是「三細亞」,大約是十公斤。細麵粉,和麵烤餅。」 7亞伯拉罕又跑到牛群中牽了一頭肥嫩的小牛,吩咐僕人趕快準備好。 8亞伯拉罕把奶、乳酪和準備好的牛肉擺在客人面前,站在樹蔭下招待他們。

9那三位客人問亞伯拉罕:「你妻子撒拉在哪裡?」亞伯拉罕回答說:「在帳篷裡。」 10其中一人說:「明年這時候,我會再來你這裡,撒拉必生一個兒子。」這話被站在那人後面帳篷口的撒拉聽見了。 11亞伯拉罕撒拉已經年紀老邁,撒拉的月經也已經停了。 12撒拉暗自發笑,心想:「我已經這麼老了,還會有這種福氣嗎?況且我的丈夫也很老了。」 13耶和華問亞伯拉罕:「撒拉為什麼偷笑說,『我這把年紀還會有孩子嗎?』 14什麼事難得住耶和華呢?明年這時候,我會再來你這裡,撒拉必生一個兒子。」 15撒拉聽見後非常害怕,連忙否認說:「我沒有笑!」但耶和華說:「不,你確實笑了。」

亞伯拉罕為所多瑪求情

16那三個人就起身朝所多瑪眺望,亞伯拉罕與他們同行,要送他們一程。 17耶和華說:「我要做的事怎麼可以瞞著亞伯拉罕呢? 18亞伯拉罕必成為強盛的大國,世上萬國必因他而蒙福。 19我揀選了他,是要他教導自己的子孫後代持守我的道、秉公行義。這樣,我必實現對他的應許。」 20耶和華說:「所多瑪蛾摩拉罪惡深重,人們怨聲載道。 21我現在要下去看看他們的所作所為是否如所說的那樣邪惡,如果不是,我也會知道。」

22其中二人轉身向所多瑪走去,亞伯拉罕卻仍舊站在耶和華面前。 23亞伯拉罕上前說:「你要把義人和惡人一同毀滅嗎? 24倘若城中有五十個義人,你還要毀滅那城嗎?你會不會為了五十個義人而饒恕那座城呢? 25你絕不會黑白不分,把義人和惡人一同毀滅。你是普天下的審判者,難道不秉公行事嗎?」 26耶和華回答說:「倘若我在所多瑪城中找到五十個義人,我就要因他們的緣故饒恕全城。」 27亞伯拉罕說:「主啊,雖然我渺小如灰塵,但我還要大膽地求問你, 28倘若只有四十五個義人,你會因為少了五個義人而毀滅全城嗎?」耶和華說:「倘若我在城裡找到四十五個義人,我也不會毀滅那城。」 29亞伯拉罕又說:「倘若在那裡找到四十個義人呢?」耶和華說:「為了那四十個人的緣故,我不會毀滅那城。」 30亞伯拉罕說:「求主不要發怒,容許我再問一次,倘若在那裡只找到三十個義人呢?」耶和華說:「倘若在那裡只找到三十個,我也不會毀滅那城。」 31亞伯拉罕說:「我大膽再問一次,倘若在那裡只找到二十個義人呢?」耶和華說:「為了那二十個人的緣故,我也不會毀滅那城。」 32亞伯拉罕又說:「求主不要發怒,讓我問最後一次,倘若在那裡只找到十個義人呢?」耶和華說:「為了那十個人的緣故,我也不會毀滅那城。」 33耶和華跟亞伯拉罕說完話便離開了,亞伯拉罕也回家去了。