Mwanzo 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 17:1-27

Agano La Tohara

117:1 Mwa 5:22; 12:4-7; 20:5; 28:3; 35:11; 43:14; 48:3; 49:25; Kut 6:3; 18:13; Rut 1:20; Ay 5:17; 6:4, 14; 22:21; 33:19; 36:16; Isa 13:6; Yoe 1:15; Mik 6:9; 1Fal 3:6; 9:4; Za 15:2; 18:23; 78:72; 101:2Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi;17:1 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. 217:2 Mwa 12:2; 15:18; 22:16-18Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

317:3 Mwa 18:2; 19:1; 33:3; Kut 18:7; Hes 14:5; Yos 5:14; 7:6; Amu 13:20; Eze 1:28; 3:23Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 417:4 Mwa 15:18; 12:2; 25:23“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 517:5 Mwa 32:28; 35:10; 37:3, 13; 43:6; 46:2; 1Fal 18:31; 2Fal 17:34; 1Nya 1:34; Neh 9:7; Isa 48:1; Yn 1:42; Rum 4:17Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu,17:5 Abrahamu maana yake Baba wa watu wengi. kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi. 617:6 Mwa 1:28; 18:10; 21:1; 22:17; 26:22; 28:3; 35:11; 36:31; 41:52; 47:27; 48:4; 49:22; Law 26:9; Mt 1:6; Kum 7:13; Isa 51:2Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 717:7 Mwa 6:18; 9:16; 18:15; Kut 6:7; 20:2; 29:45-46; Law 11:44-45; 18:2; 22:33; 25:38; 26:9, 12, 15; Hes 15:41; Kum 4:20; 7:6, 21; 29:13; 2Sam 7:24; Ebr 13:20; Yer 14:9; Ufu 21:7; Rum 9:8; Gal 3:16Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 817:8 Mwa 10:19; 12:7; 15:7; 23:4; 28:4; 35:27; 37:1; Kut 6:4; Yer 31:1; 1Nya 29:15Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”

917:9 Mwa 18:19; 22:18; Kut 19:5; Kum 5:2Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo. 1017:10 Mwa 21:4; Law 12:3; Yos 5:2-7; Rum 4:11; Yn 7:22; Mdo 7:8Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. 1117:11 Kut 12:48; Kum 10:16; Mwa 9:12; Rum 4:11Mtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi. 1217:12 Mwa 9:12; 21:4; Law 12:3; Yos 5:2; Lk 1:59; 2:21Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako. 1317:13 Kut 12:44-48; Mwa 9:16Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele. 1417:14 Kut 4:24-26; 12:15, 19; 30:33; Eze 44:7; Yos 5:2-8; Law 7:20, 25; 17:4; 18:29; 19:8; 20:17; Hes 9:13; 15:30; 19:13; Kum 17:12; Ay 38:15; Za 37:28Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.”

1517:15 Mwa 11:29Pia Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara. 1617:16 Mwa 18:10; 24:60; Isa 29:22; Gal 4:31Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.”

1717:17 Mwa 12:4; 18:11-13; 21:6, 7; 24:1, 36; Yer 20:15; Lk 1:18; Rum 4:19; Gal 4:23; Ebr 11:11Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 1817:18 Mwa 16:15; 21:11Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”

1917:19 Mwa 9:16; 16:11; 18:14; 21:2; 26:3; 50:24; Kut 13:11; Kum 1:8; Gal 3:16; 1Sam 1:20; Mt 1:21; Lk 1:13, 31Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki.17:19 Isaki maana yake Kucheka. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. 2017:20 Mwa 13:16; 16:10; 25:12-18; 48:19Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 2117:21 Kut 34:10; Mwa 18:10-14; 21:2Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 2217:22 Mwa 18:33; 35:13; Hes 12:9Wakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu.

2317:23 Mwa 12:5Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 2417:24 Mwa 12:4; Rum 4:11Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa, 2517:25 Mwa 16:16naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu. 26Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile, 2717:27 Mwa 14:14Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.