Mwanzo 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 16:1-16

Hagari Na Ishmaeli

116:1 Mwa 11:29, 30; 24:61; 29:24-29; 31:33; 46:18; 21:14; 25:12; 30:2; Lk 1:7, 36; Gal 4:24-25Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari, 216:2 Mwa 19:31-32; 30:3-10hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.”

Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. 316:3 Mwa 12:4-5Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake. 416:4 Mwa 30:1; 1Sam 1:6Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba.

Hagari alipojua kuwa ana mimba, alianza kumdharau Sarai. 516:5 Mwa 31:53; Kut 5:21; Amu 11:27; 1Sam 24:12-15; 26:10, 23; Za 50:6; 75:7Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Bwana na aamue kati yako na mimi.”

616:6 Yos 9:25; Mwa 31:50Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.

716:7 Mwa 21:17; 22:11-15; 24:7, 40; 25:18; 31:11; 48:16; Kut 3:2; 14:19; 15:22; 23:20-23; 32:34; 33:2; Amu 2:1; 6:11; 13:3; Za 34:7; 2Sam 24:16; 21:19; 1Fal 19:5; 2Fal 1:3; 19:35; Zek 1:11; Mdo 5:19; 1Sam 15:7Malaika wa Bwana akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri. 816:8 Mwa 3:9Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?”

Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.”

9Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” 1016:10 Mwa 13:16; 17:20Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.”

1116:11 Mdo 5:19; Mwa 3:15; 12:2-3; 18:19; 17:19; 21:3; 37:25-28; 29:32; 31:42; Neh 9:7; Isa 44:1; Amo 3:2; Mt 1:21; Lk 1:13, 31; Amu 8:24; Kut 2:24; 3:7, 9; 4:31; Hes 20:16; Kum 26:7; 1Sam 9:16Pia malaika wa Bwana akamwambia:

“Wewe sasa una mimba

nawe utamzaa mwana.

Utamwita jina lake Ishmaeli,16:11 Ishmaeli maana yake Mungu husikia.

kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.

1216:12 Ay 6:5; 11:12; 24:5; 39:5; Hos 8:9; Za 104:11; Yer 2:24; Mwa 25:18Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu,

mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu

na mkono wa kila mtu dhidi yake,

naye ataishi kwa uhasama

na ndugu zake wote.”

1316:13 Za 139:1-12; Mwa 32:30; 33:10; Kut 24:10; 33:20-23; Hes 12:8; Amu 6:22; 13:22; Isa 6:5Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.” 1416:14 Mwa 24:62; 25:11; 14:7Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,16:14 Beer-Lahai-Roi maana yake Yeye Aliye Hai Anionaye Mimi. ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi.

1516:15 Mwa 21:9; 17:18; 25:12; 28:9; Gal 4:22Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli. 1616:16 Mwa 12:4Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli.