Mwanzo 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 15:1-21

Agano La Mungu Na Abramu

115:1 1Sam 3:10; 15:10; 2Sam 7:4; 22:3, 31; 1Fal 6:11; 12:22; Yer 1:8, 13; Eze 3:16; Dan 10:1; Mwa 21:17; 26:24; 46:3; 46:2; Rut 1:20; Hes 12:6; 24:4; Ay 33:15; Kut 14:13; 20:20; 2Fal 6:16; Hag 2:5; 2Nya 20:15-17; Za 3:3; 5:12; 18:2, 20; 37:25; 58:11; 28:7; 33:20; 84:11; 119:114; 144:2; 27:1; Isa 7:4; 41:10-14; 43:1, 5; Kum 33:29; Mit 2:7; 30:5Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono:

“Usiogope, Abramu.

Mimi ni ngao yako,

na thawabu yako kubwa sana.”

215:2 Isa 49:22; Yer 44:26; Eze 5:11; 16:48; Mdo 7:5; Mwa 14:15Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 315:3 Mwa 24:2, 34; 12:5Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”

415:4 Gal 4:28Ndipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 515:5 Ay 11:8; 35:5; Za 8:3; 147:4; Yer 30:19; 33:22; Mwa 12:2; Rum 4:18; Ebr 11:12; Kut 32:13Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”

615:6 Za 106:31; Rum 4:3, 20-24; Gal 3:6; Yak 2:23Abramu akamwamini Bwana, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

715:7 Mwa 12:1; 13:17; 17:8; 28:4; 35:12; 48:4; Kut 6:8; 20:2; Mdo 7:3; Ebr 11:8; Kum 9:5Pia akamwambia, “Mimi ndimi Bwana, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.”

815:8 Lk 1:18; Kum 12:20; 19:8Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?”

915:9 Hes 19:2; Kum 21:3; Hos 4:16; Amo 4:1; 1Sam 1:24; Law 1:14; 5:7, 11; 12:8Ndipo Bwana akamwambia, “Niletee mtamba wa ngʼombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.”

1015:10 Yer 34:18; Law 1:17; 5:8Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. 1115:11 Kum 28:26; Yer 7:33Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza.

1215:12 Mwa 2:21Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. 1315:13 Kut 1:11; 3:7; 5:6-14; 12:40; Ay 3:18; Kum 5:15; Mdo 7:6; Hes 20:15; Gal 3:17Kisha Bwana akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. 1415:14 Mwa 50:24; Kut 3:8; 6:6-8; 12:25; 12:32-38; Hes 10:29; Yos 1:2; Mdo 7:7Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. 1515:15 Mwa 25:8; 35:29; 47:30; 49:29; Kum 31:16; 34:7; 2Sam 7:12; 1Fal 1:21; Za 49:19; 91:16; Kut 23:29; Yos 14:11; Amu 8:32; 1Nya 29:28; Ay 5:26; 21:23; 42:17; Mit 3:16; 9:11; Isa 65:20Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema. 1615:16 Kut 3:8, 17; 12:40; Mwa 28:15; 46:4; 48:21; 50:24; Law 18:28; Yos 13:4; Amu 10:11; Eze 16:3; 1Fal 21:26; 2Fal 16:3; 21:11Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

1715:17 Amu 7:16-20; 14:4-5Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. 1815:18 Mwa 2:14; 4:7; 12:7; 17:2-7; Kut 6:4; 34:10, 27; 1Nya 16:16; Za 105:9; Hes 34:5; Isa 27:12; Yos 15:4, 47; 1Fal 8:65; 2Fal 24:7; 2Nya 7:8; Yer 37:5; 46:2; Mao 4:17; Eze 30:22; 47:19Siku hiyo Bwana akafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri15:18 Kijito cha Misri hapa ina maana Wadi-el-Arish kwenye mpaka wa kusini wa Yuda. hadi mto ule mkubwa, Frati, 1915:19 Hes 24:21; Amu 1:16; 4:11; 5:24; 1Sam 15:6; 27:10; 30:29; 1Nya 2:55yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 2015:20 Mwa 10:15; Kum 7:1; Mwa 13:7; 14:5Wahiti, Waperizi, Warefai, 2115:21 Mwa 10:16; Yos 3:10; 24:11; Neh 9:8Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”