Mwanzo 14 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 14:1-24

Abramu Amwokoa Loti

114:1 Mwa 10:10, 20Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu 214:2 Mwa 10:19; 13:10kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). 314:3 Hes 34:3-12; Kum 3:17; Yos 3:16; 12:3; 15:2-5; 18:19Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). 4Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi.

514:5 Mwa 15:20; Kum 2:10, 11, 20; 3:11-13; Yos 12:4; 13:12; 17:15; 1Nya 20:4Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu, 614:6 Mwa 21:21; 36:20; 32:3; 33:14-16; 36:8; Kum 2:11, 22; Yos 11:17; 24:4; 1Nya 4:42; Isa 34:5; Eze 25:8; 35:2; Amo 1:6; Hes 12:16; 10:12; 13:3, 26; Hab 3:3na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa. 714:7 Mwa 16:14; 20:1; Hes 13:26; 20:1; 32:8; Kum 1:2; 25:17; 29:23; Yos 10:41; Amu 3:13; 6:3; 10:12; 12:15; 11:16; Za 29:8; 83:7; Kut 17:8; Hes 13:29; 14:25; 24:20; 1Sam 14:48; 15:2; 28:18; 2Sam 1:1; 1Nya 4:43; Hos 11:8Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari.

814:8 Mwa 13:10; 19:17-29; Hos 11:8; Kum 29:23Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu 914:9 Mwa 10:22dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. 1014:10 Mwa 11:3; Za 11:1; Yos 2:16; 19:17, 30Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani. 11Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao. 1214:12 Mwa 11:27Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.

1314:13 Mwa 13:18; 37:28; 39:14-17; 40:15; 41:12; 43:32; Kut 3:18; 1Sam 4:6; 14:11; Hes 13:23; 32:9; Kum 1:24Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Wakati huu Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, aliyekuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu. 1414:14 Kum 4:9; 34:1; Mit 22:6; Mwa 12:5; Amu 18:29; 1Fal 15:20Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. 1514:15 Amu 1:3-8; 7:16; 15:2; 2Sam 8:5; 1Fal 20:34; 2Fal 16:9; Isa 7:8; 8:4; 10:9; 17:1; Yer 49:23, 27; Eze 27:18Wakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski. 1614:16 1Sam 30:8, 18Akarudisha mali zote, na akamrudisha Loti jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.

1714:17 2Sam 18:18Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme).

1814:18 Za 7:8; 76:2; 104:15; 110:4; Ebr 7:2, 17, 21; 5:6; Mwa 3:19; Amu 9:13; 19:19; Es 1:10; Mit 31:6; Mhu 10:19; Wim 1:2; Dan 7:27Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 1914:19 Ebr 7:6; Mwa 1:1; 24:3; Yos 2:11; Za 148:5; Mt 11:25Naye akambariki Abramu, akisema,

“Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,

Muumba wa mbingu na nchi.

2014:20 Mwa 9:26; 24:27; 28:22; Kum 14:22; 26:12; Lk 18:12; Ebr 7:4Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,

ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.”

Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.

21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.”

2214:22 Kut 6:8; Hes 14:30; Neh 9:15; Kum 32:40; Eze 20:5; Dan 12:7; Ufu 10:5-6Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa 2314:23 1Sam 15:3, 19; 2Fal 5:16; Es 8:11; 9:10-15kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’ 2414:24 Mwa 13:18Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”