Mwanzo 13 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 13:1-18

Abramu Na Loti Watengana

113:1 Mwa 45:25; 12:9; 11:27Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Loti akaenda pamoja naye. 213:2 Mwa 12:5; 26:13; 32:15; Mit 10:22; Ay 1:3; 42:12Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.

313:3 Mwa 12:8-9Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 413:4 Mwa 12:7; 4:26hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Bwana.

513:5 Mwa 11:27Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. 613:6 Mwa 12:5; 33:9; 36:7Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. 713:7 Mwa 26:20-21; 10:18; 15:20; 12:6; 34:30; Hes 20:3; Kut 3:8; Amu 1:4Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.

813:8 Mwa 11:27; 19:9; Mit 15:18; 20:3; Kut 2:14; Hes 16:13; Za 133:1Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu. 913:9 Mwa 20:15; 34:10; 47:6; Yer 40:4Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”

1013:10 1Fal 7:47; 2Nya 4:17; Hes 13:29; 33:48; Mwa 19:22; 2:8-10; 46:7; 14:2, 8Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.) 11Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana: 1213:12 Mwa 10:19; 11:27; 19:17-29; 14:12Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Loti aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. 1313:13 Mwa 18:20; 19:4; 19:5; 20:6; 39:9; Isa 1:10; 3:9; Hes 32:23; 1Sam 12:23; 2Sam 12:13; Za 51:4; Eze 16:49-50; 2Pet 2:8Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.

1413:14 Mwa 28:14; 32:12; 48:16; Kum 3:27; 13:17; Isa 54:3Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. 1513:15 Mwa 12:7; Gal 3:16Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 1613:16 Mwa 12:2; 16:10; 17:20; 21:13-18; 25:16; Hes 23:10Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. 1713:17 Mwa 12:7; 15:7; Hes 13:17-25Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”

1813:18 Mwa 8:20; 14:13; 18:1; 23:2, 17, 19; 25:9; 49:30; 50:13; 35:27; Hes 13:22; Yos 10:3, 36; Amu 1:10; 1Sam 30:31; 2Sam 2:1-11; 1Nya 11:1Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea Bwana madhabahu.