Mwanzo 11 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 11:1-32

Mnara Wa Babeli

1Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 211:2 Mwa 10:10Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari11:2 Shinari ndio Babeli. nao wakaishi huko.

311:3 Kut 1:14; 5:7; Yer 43:9; Isa 9:10; Amo 5:11; Mwa 14:10Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 411:4 Kum 1:28; 6:10; 9:1; Ay 20:6; Yer 51:53; 31:10; 40:15; Mwa 6:4; 9:19; Kum 30:3; 4:27; 1Fal 22:17; Es 3:8; Za 44:11; Eze 6:8; Yoe 3:2Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”

511:5 Mwa 18:21; Kut 3:6-8; 19:11, 18-20; Za 18:9; 144:5Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. 6Bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 711:7 Mwa 1:26; 42:23; Kum 28:49; Isa 28:11; 33:19; Yer 5:15; 1Kor 2:11Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

811:8 Mwa 9:19; Kum 32:8; Lk 1:51Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 911:9 Mwa 10:10; Za 55:9; Mdo 2:5-11; Isa 2:10, 21; 13:14; 24:1Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.

Shemu Hadi Abramu

(1 Nyakati 1:24-27)

1011:10 Mwa 2:4; Lk 3:36Hivi ndivyo vizazi vya Shemu.

Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi. 11Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

1211:12 Lk 3:35Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. 13Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

14Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. 15Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

16Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

18Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. 19Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

2011:20 Lk 3:35Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

2211:22 Lk 3:34Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. 23Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

2411:24 Lk 3:34Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. 25Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

2611:26 Lk 3:34; Yos 24:2; 2Fal 19:12; Isa 37:12; Eze 27:23Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani.

Wazao Wa Tera

2711:27 Mwa 2:4; 31:53; 12:4; 13:1-5, 8, 12; 14:12; 19:1; Lk 17:28; 2Pet 2:5-7Hawa ndio wazao wa Tera.

Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. 2811:28 Mwa 15:7; Neh 9:7; Ay 1:17; 16:11; Eze 23:23; Mdo 7:4Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. 2911:29 Mwa 22:20-23; 24:10-24; 29:5; 12:5; 16:1; 17:15Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. 3011:30 Mwa 16:1; 18:11; 25:21; 29:31; 30:1, 22; Amu 13:2; 1Sam 1:5; Za 113:9Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto.

3111:31 Mwa 38:11; 10:19; 12:4; 27:43; 28:5-10; 29:4; Law 18:15; 20:21; Rut 1:6, 22; 2:20; 4:15; 1Sam 4:19; 1Nya 2:4; Mik 7:6; Eze 22:11; 27:23; Mdo 7:4; 2Fal 19:12Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.

3211:32 Yos 24:2Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.