Mwanzo 10 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 10:1-32

Mataifa Yaliyotokana Na Noa

(1 Nyakati 1:5-23)

110:1 Mwa 2:4; 5:32; 1Nya 1:4Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

Wazao Wa Yafethi

210:2 Eze 38:6; 39:1, 6; 27:13-19; 33:26; Ufu 20:8; Isa 66:19Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

310:3 Yer 51:27; Eze 27:13-14; 38:6Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

410:4 Eze 27:7, 10, 12, 25; 38:13; Za 48:7; 72:10; Isa 2:16; 23:1-6, 12; 66:19; Yer 2:10; 10:9; Yon 1:3; Hes 24:24; Dan 11:30Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

Wazao Wa Hamu

610:6 2Fal 19:9; Nah 3:9; 2Nya 12:3; 16:8; Isa 11:11; 18:1; 20:3; 43:3; Yer 46:9; Eze 27:10; 30:4-9; 38:5; Mwa 9:18; Sef 2:12; 3:10Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu,10:6 Yaani Misri. Putu na Kanaani.

710:7 Isa 21:13; 43:3; 60:6; Mwa 2:11; 25:3; Eze 38:13; 27:15, 20, 22; 1Fal 10:1; 2Nya 9:1; Ay 1:15; 6:19; 16:11; Za 72:10; Yer 25:23-24; 6:20; 49:8; Yoe 3:8; 1Nya 1:32Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

810:8 Mik 5:6Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 910:9 2Nya 14:9; 16:8; Isa 18:2; Mwa 25:27; 27:3Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 1010:10 Mwa 11:2, 9; 14:1; 2Nya 36:17; Isa 10:9; 13:1; Yer 21:2; 25:12; 50:1; Ezr 4:9; Amo 6:2; Zek 5:11Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 1110:11 Za 83:8; Isa 37:37; Mik 5:6; Sef 2:13; 2Fal 19:36; Yon 1:2; 3:2-3Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

13Misraimu alikuwa baba wa:

Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 1410:14 Mwa 21:32-34; 26:1, 8; Yos 13:2; Amu 3:3; Isa 14:31; Yer 47:1-4; Amo 9:7; Kum 2:23; 1Nya 1:12Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

1510:15 Mwa 9:18; 5:20; 23:3; 25:10; 26:34; 27:46; 49:32; Yos 1:4; 11:8; Amu 10:6; Isa 23:2-4; Yer 25:22; 27:3; 47:4; Eze 16:3; 28:21; 32:30; Yoe 3:4; Zek 9:2; Kut 4:22; Hes 1:20; 3:2; 13:29; 18:15; 33:4; 1Sam 26:6Kanaani alikuwa baba wa:

Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 1610:16 Amu 19:10; 1Nya 11:4; Ezr 9:1; Kut 3:8; 2Nya 8:7; Hes 13:29; 21:13; 32:39; Yos 2:10; Kum 1:4; 7:1; Yos 2:10; Mwa 15:18-21Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 1710:17 Mwa 34:2; 36:2; Kut 3:8; Kum 7:1; Amu 3:3Wahivi, Waariki, Wasini, 1810:18 Eze 27:8; 1Nya 18:3; Mwa 12:6; 13:17; 50:11; Kut 13:11; Hes 13:29; 14:25; 21:3; 33:40; Kum 7:1; Amu 1:1Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 1910:19 Mwa 11:31; 12:1; 13:12; 14:2; 17:8; 24:3; 26:34; 37:1; 27:46; 28:1-8; 31:18; 35:6; 49:13; Law 25:38; Yos 19:28; Amu 1:18, 31; 18:28; 6:4; 16:1, 21; 2Nya 24:6; 14:13; Kum 2:23; 29:23; Yos 10:41; 11:22; 15:47; 1Sam 6:17; Yer 25:20; 47:1; Amo 1:6; Sef 2:4na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Wazao Wa Shemu

2110:21 Hes 24:24Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

2210:22 Mwa 14:1; Isa 11:11; 21:2; Yer 25:25; 49:34; Eze 27:23; 32:24; Dan 8:2; Lk 3:36; Hes 24:22-24; Amu 3:10; 1Fal 11:25; 19:15; 20:34; 22:31; 2Fal 5:1; 8:7Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

2310:23 Mwa 22:21; Ay 1:1; Yer 25:20; Mao 4:21Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

2410:24 Lk 3:35Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,

naye Shela akamzaa Eberi.

25Eberi akapata wana wawili:

Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

26Yoktani alikuwa baba wa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 2710:27 Eze 27:19Hadoramu, Uzali, Dikla, 2810:28 1Fal 10:1; Ay 6:11; Za 72:10, 15; Isa 60:6; Eze 27:22Obali, Abimaeli, Sheba, 2910:29 1Fal 9:28; 1Nya 29:4; Ay 22:24; 28:16; Za 45:9; Isa 13:12; 10:32; Mwa 9:19Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.