Makaribisho Ya Hekima Na Ya Upumbavu
19:1 Efe 2:20-22; 1Tim 3:15; 1Pet 3:5Hekima amejenga nyumba yake;
amechonga nguzo zake saba.
29:2 Lk 14:16-23; Isa 25:6; 62:8Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake;
pia ameandaa meza yake.
39:3 Mit 1:20; 8:1-3; Mt 22:3, 4, 9; Lk 14:17; Rum 10:15Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita
kutoka mahali pa juu sana pa mji.
49:4 Mit 1:22; 6:32; Mt 11:25Anawaambia wale wasio na akili,
“Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
59:5 Za 42:2; Isa 44:3; Mt 26:26-28Njooni, mle chakula changu
na mnywe divai niliyoichanganya.
69:6 Mit 8:35; 3:1-2Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;
tembeeni katika njia ya ufahamu.
79:7 Mit 23:9; Mt 7:6“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha
hukaribisha matukano;
yeyote anayekemea mtu mwovu
hupatwa na matusi.
8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia;
mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
99:9 Mit 15:31; 19:25; Mt 13:12Mfundishe mtu mwenye hekima
naye atakuwa na hekima zaidi;
mfundishe mtu mwadilifu
naye atazidi kufundishika.
109:10 Ay 28:28“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
119:11 Mwa 15:15; Kum 11:21; Mit 10:27Kwa maana kwa msaada wangu
siku zako zitakuwa nyingi,
na miaka itaongezwa katika maisha yako.
129:12 Ay 35:6, 7Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;
kama wewe ni mtu wa mzaha,
wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”
139:13 Mit 7:11; 5:6Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele;
hana adabu na hana maarifa.
149:14 Eze 16:25Huketi kwenye mlango wa nyumba yake,
juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,
159:15 Mit 1:20akiita wale wapitao karibu,
waendao moja kwa moja kwenye njia yao.
169:16 Mit 1:22Anawaambia wale wasio na akili,
“Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”
179:17 Mit 20:17“Maji yaliyoibiwa ni matamu;
chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”
189:18 Mit 2:18; 7:26-27Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo,
kwamba wageni wake huyo mwanamke
wako katika vilindi vya kuzimu.