Mithali 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 6:1-35

Maonyo Dhidi Ya Upumbavu

16:1 Mwa 43:9; Ebr 7:22; Ezr 10:27; Mit 17:18Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,

ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi

kwa ajili ya mwingine,

2kama umetegwa na ulichosema,

umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,

kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:

Nenda ukajinyenyekeshe kwake;

msihi jirani yako!

46:4 Rut 3:18; Za 132:4Usiruhusu usingizi machoni pako,

usiruhusu kope zako zisinzie.

56:5 Za 91:3; 2Sam 2:18; Isa 13:14; Za 91:3Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji,

kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.

66:6 Mit 6:11Ewe mvivu, mwendee mchwa;

zitafakari njia zake ukapate hekima!

7Kwa maana yeye hana msimamizi,

wala mwangalizi, au mtawala,

86:8 Mit 30:24-25; 10:4lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

96:9 Mit 24:30-34; 26:13-16Ewe mvivu, utalala hata lini?

Utaamka lini kutoka usingizi wako?

106:10 Mit 24:33; Mhu 4:5Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

116:11 Mit 6:10-11; 20:13; 24:30-34hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

12Mtu mbaya sana na mlaghai,

ambaye huzungukazunguka

na maneno ya upotovu,

136:13 Za 35:19; Mit 16:30ambaye anakonyeza kwa jicho lake,

anayetoa ishara kwa miguu yake

na kuashiria kwa vidole vyake,

146:14 Za 36:4; 140:2; Mik 2:1; Isa 32:7ambaye hupanga ubaya

kwa udanganyifu moyoni mwake:

daima huchochea fitina.

15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula;

ataangamizwa mara, pasipo msaada.

166:16 Mit 3:32; 8:13; 15:8, 9, 26; 16:5Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,

naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

176:17 Za 120:2; Mit 12:22; Yer 2:34; Mik 7:2; Hos 4:1-2macho ya kiburi,

ulimi udanganyao,

mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

186:18 Mwa 6:5; Ay 15:31; Rum 3:15moyo uwazao mipango miovu,

miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

196:19 Kum 19:16; Za 27:12; Mit 15:18; Zek 8:17shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,

na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

Onyo Dhidi Ya Uasherati

206:20 Mit 3:21; 1:8Mwanangu, zishike amri za baba yako,

wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

216:21 Kum 6:8; Mit 3:3Yafunge katika moyo wako daima,

yakaze kuizunguka shingo yako.

226:22 Mit 3:23; 2:11Wakati utembeapo, yatakuongoza;

wakati ulalapo, yatakulinda;

wakati uamkapo, yatazungumza nawe.

236:23 Za 19:8; 10:17Kwa maana amri hizi ni taa,

mafundisho haya ni mwanga

na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

246:24 Mwa 39:8; Za 55:21yakikulinda na mwanamke aliyepotoka,

kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.

256:25 2Sam 11:2-5; Mt 5:28Moyo wako usitamani uzuri wake

wala macho yake yasikuteke,

266:26 Mit 27:22-23; 29:3; Eze 13:18kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,

hata ukose kipande cha mkate,

naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.

27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake

bila nguo zake kuungua?

28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka

bila miguu yake kuungua?

296:29 Kut 20:14; Mit 2:16-19Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;

hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.

30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba

kukidhi njaa yake wakati ana njaa.

316:31 Kut 22:1-14Pamoja na hayo, kama akikamatwa,

lazima alipe mara saba,

ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.

326:32 Kut 20:14; Mit 7:7; 9:4, 16Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;

yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

336:33 Mit 5:9-14Mapigo na aibu ni fungu lake

na aibu yake haitafutika kamwe;

346:34 Hes 5:14; Mwa 34:7kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,

naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.

356:35 Ay 31:9-11; Wim 8:7Hatakubali fidia yoyote;

atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.