Mithali 31 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 31:1-31

Misemo Ya Mfalme Lemueli

131:1 Mit 22:17Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

231:2 Amu 11:30; Isa 49:15“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,

ee mwana wa nadhiri zangu,31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu.

331:3 Neh 13:26; Kum 17:17; Hos 4:11; 1Fal 11:3Usitumie nguvu zako kwa wanawake,

uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

431:4 Mhu 10:17; Isa 5:22“Ee Lemueli, haifai wafalme,

haifai wafalme kunywa mvinyo,

haifai watawala kutamani sana kileo,

531:5 1Fal 16:9; Mit 16:12; Hos 4:11wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru

na kuwanyima haki zao wote walioonewa.

631:6 Mwa 14:18Wape kileo wale wanaoangamia,

mvinyo wale walio na uchungu,

731:7 Es 1:10Wanywe na kusahau umaskini wao

na wasikumbuke taabu yao tena.

831:8 1Sam 19:4; Es 4:16; Ay 29:12-17“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,

kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.

931:9 Law 19:15; Yer 22:16; Kum 1:16; Isa 1:17Sema na uamue kwa haki,

tetea haki za maskini na wahitaji.”

Maneno Ya Mwisho: Mke Mwenye Sifa Nzuri

1031:10 Rut 3:11; Mit 19:14Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?

Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.31:10 Mithali 31:10-31 imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

1131:11 Mwa 2:18; Mit 12:4Mume wake anamwamini kikamilifu

wala hakosi kitu chochote cha thamani.

12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya,

siku zote za maisha yake.

1331:13 1Tim 2:9-10Huchagua sufu na kitani

naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.

14Yeye ni kama meli za biashara

akileta chakula chake kutoka mbali.

1531:15 Mt 24:45; Rum 12:11; Ay 23:12Yeye huamka kungali bado giza

huwapa jamaa yake chakula

na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

16Huangalia shamba na kulinunua,

kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

17Hufanya kazi zake kwa nguvu,

mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

18Huona kwamba biashara yake ina faida,

wala taa yake haizimiki usiku.

19Huweka mikono yake kwenye pia,

navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.

2031:20 Kum 15:11; Ebr 13:16; Efe 4:26-28Huwanyooshea maskini mikono yake

na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

2131:21 Yos 2:18-19; Ebr 9:19-22Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,

kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake,

yeye huvaa kitani safi na urujuani.

2331:23 Kut 3:16; Kum 16:18; Rut 4:1, 11; Mit 12:4Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji,

aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza,

naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

2531:25 1Tim 2:9, 10Amevikwa nguvu na heshima,

anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.

26Huzungumza kwa hekima

na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

2731:27 Mit 14:1; 1Tim 5:14; 2Tim 3:15; Tit 2:4-5Huangalia mambo ya nyumbani mwake

wala hali chakula cha uvivu.

2831:28 1Fal 2:19Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa,

mumewe pia humsifu, akisema:

29“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri,

lakini wewe umewapita wote.”

3031:30 Za 112:1Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi,

bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

31Mpe thawabu anayostahili,

nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.