Mithali 28 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 28:1-28

128:1 2Fal 7:7; Law 26:17; Za 53:5Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza,

bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

2Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi,

bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.

328:3 Mt 18:28Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi

ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao.

428:4 1Fal 18:18; Mt 3:7; Efe 5:11; 1Tim 5:20Wale waiachao sheria huwasifu waovu,

bali wale waishikao sheria huwapinga.

528:5 Yn 7:17; 1Kor 2:15Watu wabaya hawaelewi haki,

bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

628:6 Mit 19:1Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama

kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

728:7 Mit 23:19-21Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu,

bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

828:8 Ay 27:16-17; Eze 18:8; Kut 18:21; Mit 13:22; Lk 14:12-14Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno

hukusanya kwa ajili ya mwingine,

ambaye atawahurumia maskini.

928:9 Za 66:18; Zek 7:11; Isa 1:13; 2Tim 4:3Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria,

hata maombi yake ni chukizo.

1028:10 Za 34:9; 57:6; Mk 10:30; Mit 26:27; Rum 8:32Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya,

ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe,

bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.

11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe,

bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.

1228:12 2Fal 11:20; Ay 24:4; Mit 11:10Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa,

bali waovu watawalapo, watu hujificha.

1328:13 1Yn 1:8-10; 2Sam 12:13; Ay 31:33; Dan 4:27Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,

bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.

1428:14 Za 16:8; Mit 23:17; Rum 2:5; 11:20Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,

bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu

huangukia kwenye taabu.

15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye,

ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge.

16Mtawala dhalimu hana akili,

bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu

atafurahia maisha marefu.

1728:17 Mwa 9:6; 1Sam 30:17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua

atakuwa mtoro mpaka kufa;

mtu yeyote na asimsaidie.

1828:18 Es 6:13; Mit 10:9Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama

hulindwa salama,

bali yeye ambaye njia zake ni potovu

ataanguka ghafula.

1928:19 Mit 12:11Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,

bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.

2028:20 Mit 13:11; 20:21; 23:4, 22; 1Tim 6:9Mtu mwaminifu atabarikiwa sana,

bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka

hataacha kuadhibiwa.

2128:21 Eze 13:19; Za 94:21; Mit 18:5Kuonyesha upendeleo si vizuri,

hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate.

2228:22 Mit 28:20Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri,

naye hana habari kuwa umaskini unamngojea.

2328:23 Mit 27:5, 6Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi,

kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili.

2428:24 Mit 18:9; 19:26Yeye amwibiaye babaye au mamaye

na kusema, “Si kosa,”

yeye ni mwenzi wa yule aharibuye.

2528:25 1Tim 6:6; Mit 29:25Mtu mwenye tamaa huchochea fitina,

bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.

2628:26 Za 4:5; Mit 3:5Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu,

bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.

2728:27 Kum 15:7; Mit 19:17; 22:9Yeye ampaye maskini

hatapungukiwa na kitu chochote,

bali yeye awafumbiaye maskini macho

hupata laana nyingi.

2828:28 Mit 28:12; Ay 20:19Wakati waovu watawalapo,

watu huenda mafichoni,

bali waovu wanapoangamia,

wenye haki hufanikiwa.