Mithali 27 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 27:1-27

127:1 Lk 12:19-20; Yak 4:13; Mt 6:34; 1Fal 20:11Usijisifu kwa ajili ya kesho,

kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.

227:2 Mit 25:27Mwache mwingine akusifu,

wala si kinywa chako mwenyewe;

mtu mwingine afanye hivyo

na si midomo yako mwenyewe.

327:3 Ay 6:3; Es 1:12Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo,

lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.

427:4 1Yn 3:12Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika,

lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?

527:5 Gal 2:14Afadhali karipio la wazi

kuliko upendo uliofichika.

627:6 Za 141:5; Mit 28:23Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu,

bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

727:7 Ay 6:7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali,

bali kwa mwenye njaa

hata kile kilicho kichungu

kwake ni kitamu.

827:8 Isa 16:2; Ay 39:14Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake,

ndivyo alivyo mtu atangatangaye

mbali na nyumbani mwake.

927:9 Es 2:12; Za 45:8Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,

nao uzuri wa rafiki huchipuka

kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

1027:10 Mit 17:17Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,

tena usiende nyumbani mwa ndugu yako

wakati umepatwa na maafa.

Bora jirani wa karibu

kuliko ndugu aliye mbali.

1127:11 Mit 10:1; 23:15-16; Mwa 24:60Mwanangu, uwe na hekima,

nawe ulete furaha moyoni mwangu,

ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote

anitendaye kwa dharau.

1227:12 Mit 22:3Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,

bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.

1327:13 Mit 20:16Chukua vazi la yule awekaye dhamana

kwa ajili ya mgeni;

lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo

kwa ajili ya mwanamke mpotovu.

1427:14 Za 12:2Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu

asubuhi na mapema,

itahesabiwa kama ni laana.

1527:15 Es 1:18; Mit 19:13Mke mgomvi ni kama

matone yasiyokoma ya siku ya mvua.

16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo

au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.

17Kama vile chuma kinoavyo chuma,

ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

1827:18 1Kor 9:7; Lk 19:12-27; Kum 20:6Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake,

naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.

19Kama uso uonekanavyo kwenye maji,

ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

2027:20 Mit 30:15-16; Hab 2:5; Mhu 6:7Kuzimu na Uharibifu havishibi

kadhalika macho ya mwanadamu.

2127:21 Mit 17:3Kalibu ni kwa ajili ya fedha

na tanuru kwa ajili ya dhahabu,

bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.

2227:22 Isa 1:5; Yer 5:3; Mit 23:35Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,

ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,

hutauondoa upumbavu wake.

2327:23 Mit 12:10; Yer 5:3Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako

ya kondoo na mbuzi,

angalia kwa bidii ngʼombe zako.

2427:24 Mit 23:5Kwa kuwa utajiri haudumu milele,

nayo taji haidumu vizazi vyote.

2527:25 Za 104:14Wakati majani makavu yameondolewa

na mapya yamechipua,

nayo majani toka milimani yamekusanywa,

26wana-kondoo watakupatia mavazi

na mbuzi thamani ya shamba.

27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi

kukulisha wewe na jamaa yako,

na kuwalisha watumishi wako wa kike.

Nueva Versión Internacional

Proverbios 27:1-27

1No te jactes del día de mañana,

porque no sabes lo que el día traerá.

2No te jactes de ti mismo;

que sean otros los que te alaben.

3Pesada es la piedra y pesada es la arena,

pero más pesada aún es la ira del necio.

4Cruel es la furia y arrolladora la ira,

pero ¿quién puede enfrentarse a los celos?

5Más vale ser reprendido con franqueza

que ser amado en secreto.

6Más confiable es el amigo que hiere

que los abundantes besos del enemigo.

7Al que no tiene hambre, hasta la miel lo empalaga;

al hambriento, hasta lo amargo le es dulce.

8Como ave que se aleja del nido

es el hombre que se aleja del hogar.

9El perfume y el incienso alegran el corazón;

la dulzura de un amigo

proviene de su consejo sincero.

10No abandones a tu amigo ni al amigo de tu padre;

ni vayas a la casa de tu hermano el día que tengas una desgracia.

Más vale vecino cercano que hermano distante.

11Hijo mío, sé sabio y alegra mi corazón;

así podré responder al que me desprecie.

12El prudente ve el peligro y busca refugio;

el inexperto sigue adelante y sufre las consecuencias.

13Toma la prenda del que salga fiador por un extraño;

retenla en garantía si la da en favor de desconocidos.

14La mejor bendición se juzga como maldición

si se da a gritos y de madrugada.

15La mujer pendenciera es gotera constante

en un día lluvioso.

16Quien la domine podrá dominar el viento

y retener27:16 y retener. Lit. y llamará. aceite en la mano derecha.

17El hierro se afila con el hierro

y el hombre en el trato con el hombre.

18El que cuida de la higuera comerá de sus higos

y el que vela por su amo recibirá honores.

19El agua refleja el rostro;

el corazón refleja la persona.

20La Muerte27:20 la Muerte. Lit. el Seol. y el Destructor27:20 el Destructor. Lit. el Abadón. jamás se dan por satisfechos,

y tampoco los ojos del hombre.

21En el crisol se prueba la plata

y en el horno se prueba el oro;

ante las alabanzas, el pueblo.

22Aunque al necio lo muelas, lo remuelas

y lo machaques como al grano,

no le quitarás la necedad.

23Asegúrate de saber cómo está tu ganado;

cuida mucho de tus rebaños;

24pues las riquezas no son eternas

ni la corona está siempre segura.

25Cuando se limpien los campos y brote el verdor

y en los montes se recoja la hierba,

26las ovejas te darán para el vestido

y las cabras para comprar un campo;

27tendrás leche de cabra en abundancia

para que se alimenten tú, tu familia,

y tus criadas.