Mithali 23 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 23:1-35

1Uketipo kula chakula na mtawala,

angalia vyema kile kilicho mbele yako,

2na utie kisu kooni mwako

kama ukiwa mlafi.

323:3 Za 141:4Usitamani vyakula vyake vitamu

kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

423:4 Yn 6:27; 1Tim 6:9; Rum 12:16Usijitaabishe ili kuupata utajiri,

uwe na hekima kuonyesha kujizuia.

523:5 Mt 6:19; Mit 27:24Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka,

huwa kama umepata mabawa ghafula,

ukaruka na kutoweka angani kama tai.

623:6 Za 141:4; Kum 15:9Usile chakula cha mtu mchoyo,

usitamani vyakula vyake vitamu,

723:7 Za 12:2kwa maana yeye ni aina ya mtu

ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama.

Anakuambia, “Kula na kunywa,”

lakini moyo wake hauko pamoja nawe.

8Utatapika kile kidogo ulichokula,

nawe utakuwa umepoteza bure

maneno yako ya kumsifu.

923:9 Mit 9:7Usizungumze na mpumbavu,

kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.

1023:10 Kum 19:14; Mit 22:28Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani

wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,

1123:11 Ay 19:25; Kut 22:22-24; Yer 50:34; Mit 15:25kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu,

atalichukua shauri lao dhidi yako.

1223:12 Mit 2:2Elekeza moyo wako kwenye mafundisho

na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.

1323:13 Mit 13:24; 19:18; 22:18; 22:15; 29:15, 16Usimnyime mtoto adhabu,

ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.

1423:14 Mit 13:24; 19:18Mwadhibu kwa fimbo

na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini.23:14 Mautini maana yake ni Kuzimu.

1523:15 Mit 23:24, 25; 29:3Mwanangu, kama moyo wako una hekima,

basi moyo wangu utafurahi,

1623:16 Mit 23:24utu wangu wa ndani utafurahi,

wakati midomo yako

itakapozungumza lililo sawa.

1723:17 Za 73:3; Mit 28:14Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi,

bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.

1823:18 Za 37:1-4; Mit 24:14-20Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako,

nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.

1923:19 Kum 4:9; Mit 28:7Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima,

weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.

2023:20 Hab 2:15; Rum 13:13; Isa 5:22Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo,

au wale walao nyama kwa pupa,

2123:21 Mit 21:17; 19:23; 19:15kwa maana walevi na walafi huwa maskini,

nako kusinzia huwavika matambara.

2223:22 Law 19:32; Efe 6:1-2Msikilize baba yako, aliyekuzaa,

wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

2323:23 Mit 4:7; 17:16; Mt 13:44Nunua kweli wala usiiuze,

pata hekima, adabu na ufahamu.

2423:24 Mit 23:15-16; 10:1; 15:20Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,

naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

2523:25 Mit 10:1Baba yako na mama yako na wafurahi,

mama aliyekuzaa na ashangilie!

2623:26 Mit 5:1-6; Za 18:21Mwanangu, nipe moyo wako,

macho yako na yafuate njia zangu,

2723:27 Mit 22:14kwa maana kahaba ni shimo refu

na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba.

2823:28 Mit 7:11-12; Mhu 7:26Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia,

naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.

2923:29 1Fal 20:16; Mit 20:1; Isa 5:11; Nah 1:10; Mt 24:49, 50; Efe 5:18Ni nani mwenye ole?

Ni nani mwenye huzuni?

Ni nani mwenye ugomvi?

Ni nani mwenye malalamiko?

Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?

Ni nani mwenye macho mekundu?

3023:30 Za 75:8; Efe 5:18; Mit 20:1; Efe 5:18; Za 75:8; Mit 9:2Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo,

hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,

wakati unapometameta kwenye bilauri,

wakati ushukapo taratibu!

32Mwishowe huuma kama nyoka

na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

33Macho yako yataona mambo mageni

na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.

34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,

alalaye juu ya kamba ya merikebu.

3523:35 Mit 27:22; Yer 5:3; Kum 29:19; Isa 56:12; 2Pet 2:22Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia!

Wamenichapa, lakini sisikii!

Nitaamka lini

ili nikanywe tena?”