Mithali 22 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 22:1-29

122:1 Mhu 7:1Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi,

kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.

222:2 Ay 31:15; Mt 5:45; Za 49:1-2Tajiri na maskini wanafanana kwa hili:

Bwana ni Muumba wao wote.

322:3 Mit 14:16; 27:12; Isa 26:20Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,

bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.

422:4 Mit 15:33; 10:27; Dan 4:36Unyenyekevu na kumcha Bwana

huleta utajiri, heshima na uzima.

522:5 Mit 15:19; 1Yn 5:18Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego,

bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.

622:6 Efe 6:4Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,

naye hataiacha hata akiwa mzee.

722:7 Yak 2:6Matajiri huwatawala maskini

naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.

822:8 Hos 10:13; 8:7; Kut 1:20; Gal 6:7-8; Za 125:3Yeye aupandaye uovu huvuna taabu,

nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.

922:9 Kum 14:29; 2Kor 9:6; Mit 11:25; 28:27Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa

kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.

1022:10 Mit 26:20; Mwa 21:9, 10; Za 101:5Mfukuze mwenye dhihaka,

na mvutano utatoweka;

ugomvi na matukano vitakoma.

1122:11 Mit 16:13; Mt 5:8Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema,

mfalme atakuwa rafiki yake.

12Macho ya Bwana hulinda maarifa,

bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.

1322:13 Mit 26:13Mvivu husema, “Yuko simba nje!”

au, “Nitauawa katika mitaa!”

1422:14 Mit 6:12; Mhu 7:26Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;

yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana

atatumbukia ndani yake.

1522:15 Mit 13:24; 20:30Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,

bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

1622:16 Ay 20:19-23; Amo 2:6-8; Isa 3:14-15; Yak 2:13Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali,

naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.

Misemo Ya Wenye Hekima

1722:17 Mit 1:8; 1:6; 30:1; 31:1; 2:2Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,

elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,

18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako

na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.

19Ili tumaini lako liwe katika Bwana,

hata wewe, ninakufundisha leo.

2022:20 Mit 8:6Je, sijakuandikia misemo thelathini,

misemo ya mashauri na maarifa,

2122:21 1Pet 3:15; Mhu 12:10kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika,

ili uweze kutoa majibu sahihi

kwake yeye aliyekutuma?

2222:22 Law 25:17; Zek 7:10; Kut 23:6; Mal 3:5Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini,

wala kumdhulumu mhitaji mahakamani,

2322:23 Ay 29:16; Za 12:5; 1Sam 25:39kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao

naye atawateka wao waliowateka.

24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,

usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,

2522:25 1Kor 15:33la sivyo utajifunza njia zake

na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

2622:26 Kum 19:14; Mit 23:10Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani,

au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.

2722:27 Mit 11:15; 17:18Kama ukikosa njia ya kulipa,

kitanda chako

kitachukuliwa ukiwa umekilalia.

2822:28 Kum 19:14Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani

lililowekwa na baba zako.

2922:29 1Fal 11:28; Mwa 41:46; Mhu 9:10Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake?

Atahudumu mbele ya wafalme;

hatahudumu mbele ya watu duni.