Mithali 20 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 20:1-30

120:1 Law 10:9; Hab 2:5; 1Sam 25:36; 1Fal 20:16; Mit 31:4Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;

yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.

220:2 Mit 8:36; 19:12; Es 7:7Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;

yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.

320:3 Mwa 13:8; Mit 17:14Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,

bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.

420:4 Mit 6:6; Mhu 10:18Mvivu halimi kwa majira;

kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama

lakini hapati chochote.

520:5 Za 18:16Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,

lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.

620:6 Za 12:1; Mt 6:2; Mhu 7:28; Lk 18:8Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,

bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?

720:7 Za 26:1; 37:25-26; 112:2Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,

wamebarikiwa watoto wake baada yake.

820:8 1Fal 7:7; Mit 25:4-5Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu,

hupepeta ubaya wote kwa macho yake.

920:9 Mhu 7:20; 1Fal 8:46; 1Yn 1:8Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi;

mimi ni safi na sina dhambi?”

1020:10 Mit 20:23; 11:1Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti,

Bwana huchukia vyote viwili.

1120:11 Za 39:1; Mt 7:16Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,

kama tabia yake ni safi na adili.

1220:12 Kut 4:11; Rum 11:26; Za 94:9Masikio yasikiayo na macho yaonayo,

Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.

1320:13 Mit 6:11; 19:15; Rum 12:11Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,

uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.

14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi,

kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.

1520:15 Ay 28:12, 16, 17, 18, 19Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi,

lakini midomo inenayo maarifa

ni kito cha thamani kilicho adimu.

1620:16 Kut 22:26; Mit 27:13Chukua vazi la yule awekaye dhamana

kwa ajili ya mgeni;

lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo

kwa ajili ya mwanamke mpotovu.

17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,

bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.

1820:18 Mit 11:14; 24:6Fanya mipango kwa kutafuta mashauri,

ukipigana vita, tafuta maelekezo.

1920:19 Mit 11:13Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,

kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.

2020:20 Kut 21:17; Mit 30:11; Ay 18:5; Law 20:9Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,

taa yake itazimwa katika giza nene.

2120:21 Mit 28:8; Hab 2:6Urithi upatikanao haraka mwanzoni,

hautabarikiwa mwishoni.

2220:22 Mit 24:29; Yer 42:11; Kum 32:35; Rum 12:17-19Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”

Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

2320:23 Kum 25:13Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu,

nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

2420:24 Mit 19:21; Yer 10:23; Rum 8:26Hatua za mtu huongozwa na Bwana.

Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?

2520:25 Mhu 5:2-5; Yer 44:25Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka

na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

2620:26 Mit 20:8Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu,

hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.

2720:27 Za 119:105; Mit 16:2Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu,

huchunguza utu wake wa ndani.

2820:28 Mit 29:14; Isa 16:5Upendo na uaminifu humweka mfalme salama,

kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.

2920:29 Mit 16:31Utukufu wa vijana ni nguvu zao,

mvi ni fahari ya uzee.

3020:30 Za 51:2; Mit 22:15Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,

nayo michapo hutakasa utu wa ndani.