Faida Za Hekima
12:1 Mit 1:8Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu
na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
22:2 Mit 22:17kutega sikio lako kwenye hekima
na kuweka moyo wako katika ufahamu,
32:3 Yak 1:5na kama ukiita busara
na kuita kwa sauti ufahamu,
42:4 Ay 3:21; Mt 13:44; 6:19-21na kama utaitafuta kama fedha
na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
52:5 Kum 4:6ndipo utakapoelewa kumcha Bwana
na kupata maarifa ya Mungu.
62:6 Ay 12:13; Lk 21:15; Yak 1:5Kwa maana Bwana hutoa hekima,
na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
72:7 Mwa 6:9; 15:1; Mit 30:5-6; Za 84:11Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,
yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
82:8 1Sam 2:9; Za 18:25kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki
na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
92:9 Kum 1:16Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki
na sawa: yaani kila njia nzuri.
102:10 Mit 14:33Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako,
nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
112:11 Mit 4:6Busara itakuhifadhi
na ufahamu utakulinda.
122:12 Mit 2:16; 3:13-18; 4:5Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu,
kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,
132:13 Mit 4:19; Yn 3:19; Efe 4:18wale waachao mapito yaliyonyooka
wakatembea katika njia za giza,
142:14 Mit 15:21; Yer 11:15wale wapendao kutenda mabaya
na kufurahia upotovu wa ubaya,
152:15 Za 125:5; Mit 21:8ambao mapito yao yamepotoka
na ambao ni wapotovu katika njia zao.
162:16 Mit 6:20-29; 7:5-27Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,
kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno
ya kushawishi kutenda ubaya,
172:17 Mal 2:14; Mwa 2:24aliyemwacha mwenzi wa ujana wake
na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.
182:18 Mit 5:5; 7:27; 9:18Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo
na mapito yake kwenye roho za waliokufa.
192:19 Mit 5:8; Mhu 7:26; Ebr 13:4Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi,
au kufikia mapito ya uzima.
202:20 Ebr 6:12Hivyo utatembea katika njia za watu wema
na kushikamana na mapito ya wenye haki.
212:21 Za 37:29Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi,
nao wasio na lawama watabakia ndani yake.
222:22 Ay 18:17; Za 37:38; Kum 29:28Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi,
nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.