Mithali 19 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 19:1-29

119:1 Mit 28:6Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama,

kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.

219:2 Hos 4:6; Yn 16:3; Rum 10:2Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa,

wala kufanya haraka na kuikosa njia.

319:3 Mit 14:1; 9:13; 24:9; Isa 32:6; Yak 1:13-15Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake

hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.

419:4 Mit 19:7; 14:20Mali huleta marafiki wengi,

bali rafiki wa mtu maskini humwacha.

519:5 Kut 23:1; Kum 19:19; Mit 1:28Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

naye amwagaye uongo hataachwa huru.

619:6 Mit 29:26; 17:8; 18:16Wengi hujipendekeza kwa mtawala

na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.

719:7 Mit 10:15Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:

Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!

Ingawa huwafuata kwa kuwasihi,

hawapatikani popote.

819:8 Mit 16:20Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,

yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.

919:9 Kum 19:19Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,

naye amwagaye uongo ataangamia.

1019:10 Mit 26:1; 30:21-23; Mhu 10:5-7Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa,

itakuwa vibaya kiasi gani

kwa mtumwa kuwatawala wakuu.

1119:11 2Fal 5:12; Mit 16:32; Mt 25:21; Efe 4:32Hekima ya mtu humpa uvumilivu,

ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.

1219:12 Za 33:3; 72:5-6; Es 1:12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba,

bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.

1319:13 Mit 10:1; Es 1:18; Mit 21:9Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye,

naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

1419:14 2Kor 12:14; Mit 18:22Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,

bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

1519:15 Mit 10:4; 20:13Uvivu huleta usingizi mzito,

naye mtu mzembe huona njaa.

1619:16 Mit 16:17; Lk 10:28; Rum 2:7Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake,

bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

1719:17 Kum 24:19; Mt 10:42; 2Kor 9:6Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana,

naye atamtuza kwa aliyotenda.

1819:18 Mit 13:24; 23:13-14Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini,

usiwe mshirika katika mauti yake.

19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake,

kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.

2019:20 Mit 4:1; 12:15Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho,

nawe mwishoni utakuwa na hekima.

2119:21 Es 9:25; Mhu 7:29; Yer 4:29; Mao 3:37; Ebr 6:17Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,

lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,

afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

2319:23 Za 25:13; 1Tim 4:8; Ay 4:7; Mit 10:27Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,

kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,

bila kuguswa na shida.

2419:24 Mit 26:15Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,

lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!

2519:25 Za 141:5; Mit 9:9; 21:11Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara,

mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.

2619:26 Mit 28:24Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake

ni mwana aletaye aibu na fedheha.

2719:27 Mt 7:15; Mk 4:24; Efe 4:14Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,

utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.

2819:28 Ay 15:16Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu

na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.

2919:29 Kum 25:2; Mit 26:3Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka

na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.