Mithali 18 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 18:1-24

1Mtu ajitengaye na wengine

hufuata matakwa yake mwenyewe;

hupiga vita kila shauri jema.

218:2 Mit 12:23Mpumbavu hafurahii ufahamu,

bali hufurahia kutangaza

maoni yake mwenyewe.

3Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia,

pamoja na aibu huja lawama.

418:4 Za 18:16Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,

bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.

518:5 Law 19:15; Mit 28:21; Za 82:2; Ay 13:7-8Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,

au kumnyima haki asiye na hatia.

618:6 Mit 10:14Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi

na kinywa chake hualika kipigo.

718:7 Za 140:9; 64:8; Mhu 10:12Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake

na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

818:8 Mit 26:22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

huingia sehemu za ndani sana za mtu.

918:9 Mit 28:24Mtu aliye mlegevu katika kazi yake

ni ndugu na yule anayeharibu.

1018:10 2Sam 22:3; Za 61:3; 18:2Jina la Bwana ni ngome imara,

wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

1118:11 Mit 10:15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,

wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.

1218:12 Mit 11:2; 15:33Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,

bali unyenyekevu hutangulia heshima.

1318:13 Mit 20:25; Yn 7:51Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,

huo ni upumbavu wake na aibu yake.

1418:14 Mit 15:13; 17:22Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa

bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?

1518:15 Mit 15:14; Efe 1:17Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa,

masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.

1618:16 Mwa 32:20; 39:2-6; 41:38-44; 1Sam 10:4Zawadi humfungulia njia mtoaji,

nayo humleta mbele ya wakuu.

17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi,

hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.

18Kupiga kura hukomesha mashindano

na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.

1918:19 1Sam 17:28Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika

kuliko mji uliozungushiwa ngome,

nayo mabishano ni kama malango

ya ngome yenye makomeo.

2018:20 Mit 12:14Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,

atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.

2118:21 Mit 13:2-3; Mt 12:37Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,

nao waupendao watakula matunda yake.

2218:22 Mit 12:4; 31:10; Ay 33:26Apataye mke apata kitu chema

naye ajipatia kibali kwa Bwana.

2318:23 Mwa 42:13-16; Yak 2:3Mtu maskini huomba kuhurumiwa

bali tajiri hujibu kwa ukali.

2418:24 1Sam 20:42; Yn 15:13-15Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu,

bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.