Mithali 17 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 17:1-28

117:1 Mit 15:16, 17; 16:8Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu

kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.

217:2 Mit 10:5; 19:26Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye,

naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.

317:3 Mit 27:21; Yer 17:10; 1Pet 1:7; Za 26:2Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu,

bali Bwana huujaribu moyo.

4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya;

mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.

517:5 Mit 14:31; Ay 31:39; Eze 25:3; Oba 1:12Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake;

yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.

617:6 Za 125:5; Mit 13:22Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

717:7 Mit 16:10Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu:

je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!

817:8 Mwa 39:21; Dan 6:3Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;

kokote kigeukiapo, hufanikiwa.

917:9 Mit 10:12; 16:28Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo,

bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu.

10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua

kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.

11Mtu mbaya hupenda kuasi tu;

mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.

1217:12 1Sam 25:25Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake,

kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.

1317:13 Yer 18:20; 1Sam 19:4; Rum 12:17; Za 109:4-5Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema,

kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.

1417:14 Mit 20:3; Mt 5:25-26; Mdo 6:1Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji;

kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.

1517:15 Za 94:21; Kut 23:6-7; Mit 18:5; Mao 3:34-36; Isa 5:23Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki,

naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki:

Bwana huwachukia sana wote wawili.

1617:16 Mit 23:23Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu,

wakati yeye hana haja ya kupata hekima?

1717:17 2Sam 15:21; Mit 27:10Rafiki hupenda wakati wote

naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

1817:18 Mit 6:1-5; 11:5Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani,

naye huweka dhamana kwa jirani yake.

19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi;

naye ainuaye sana lango lake17:19 Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno. hutafuta uharibifu.

20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;

naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.

2117:21 Mit 10:1Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni;

hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.

2217:22 Kut 12:46; Za 22:15Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,

bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.

2317:23 Kut 18:21; 1Sam 8:3Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri

ili kupotosha njia ya haki.

2417:24 Ay 31:1; Mhu 2:14Mtu wa ufahamu huitazama hekima,

lakini macho ya mpumbavu huhangaika

hadi kwenye miisho ya dunia.

2517:25 Mit 10:1Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake

na uchungu kwa yeye aliyemzaa.

2617:26 Za 94:21; Mit 18:5Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia,

au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.

2717:27 Ay 6:24; Mit 14:29Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia,

naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.

2817:28 Ay 2:13; Mit 10:19Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza,

na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake.