Mithali 16 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 16:1-33

116:1 Mt 10:19; Mit 19:21Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

216:2 1Sam 16:7; 2Nya 6:30; Lk 16:15; Dan 5:27Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,

bali makusudi hupimwa na Bwana.

316:3 2Nya 20:20; Za 20:4Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo,

nayo mipango yako itafanikiwa.

416:4 Isa 43:7; Kut 9:16; 2Nya 34:24; Rum 9:22Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe;

hata waovu kwa siku ya maangamizi.

516:5 Za 40:4; Mit 6:16; 11:20-21Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo.

Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.

616:6 Kut 20:20; Mit 14:16; Dan 4:26Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa;

kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.

716:7 Kol 1:10; Mwa 39:21; Za 105:15; Yer 39:12; 40:1; 42:12; Dan 1:9Njia za mtu zinapompendeza Bwana,

huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.

816:8 Za 37:16; Mit 15:16; 17:1; Mhu 4:6Afadhali kitu kidogo pamoja na haki

kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.

916:9 Yer 10:23Moyo wa mtu huifikiri njia yake,

bali Bwana huelekeza hatua zake.

1016:10 Mit 17:7Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu,

wala kinywa chake hakipotoshi haki.

1116:11 Law 19:36; Mit 11:1; Eze 45:10Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana;

mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.

1216:12 Mit 26:28; 25:5; 29:14; 31:5Wafalme huchukia sana kutenda maovu,

kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.

1316:13 Mit 22:11Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu;

humthamini mtu asemaye kweli.

1416:14 Mwa 40:2; Ay 29:24Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti,

bali mtu mwenye hekima ataituliza.

1516:15 2Nya 36:16; Mit 29:1; Yer 19:1116:15 Mwa 40:2; Ay 29:24; Mit 19:12; 25:2-7Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai;

upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli.

1616:16 Za 49:20; Ay 28:15; Mit 3:13-14Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu,

kuchagua ufahamu kuliko fedha!

1716:17 Mit 4:24-27; Isa 35:8; Mdo 24:16Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya;

yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.

1816:18 Es 5:12; Mit 29:23Kiburi hutangulia maangamizi,

roho ya majivuno hutangulia maanguko.

19Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho

miongoni mwa walioonewa

kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.

2016:20 Isa 30:18; Za 32:10; Yer 17:7Yeyote anayekubali mafundisho hustawi,

tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.

2116:21 Mit 16:23Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu,

na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho.

2216:22 Mit 10:11Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao,

bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu.

2316:23 Ay 15:5; Mit 16:21Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake,

na midomo yake huchochea mafundisho.

2416:24 Mit 24:13-14Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali,

ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa.

2516:25 Mit 12:15; 14:12; Es 3:6Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

bali mwisho wake huelekeza mautini.

2616:26 Mit 9:12; Mhu 6:7Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi;

njaa yake humsukuma aendelee.

2716:27 Yak 3:6Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya,

maneno yake ni kama moto uunguzao.

2816:28 Mit 14:17; 17:9Mtu mpotovu huchochea ugomvi,

nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.

29Mtu mkali humvuta jirani yake

na kumwongoza katika mapito yale mabaya.

3016:30 Mit 6:13Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu;

naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.

3116:31 Mit 20:29Mvi ni taji ya utukufu;

hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

3216:32 Mit 19:11Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,

mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.

3316:33 Yos 7:14; Yn 1:7Kura hupigwa kwa siri,

lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.