Mithali 15 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Mithali 15:1-33

115:1 Mit 25:15; 2Nya 10:7; 1Fal 12:7Jawabu la upole hugeuza ghadhabu,

bali neno liumizalo huchochea hasira.

215:2 Mit 12:23; Mhu 10:12; Za 59:7Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu.

315:3 2Nya 16:9; Ay 34:21; Ebr 4:13; Mit 5:21; Yer 16:17Macho ya Bwana yako kila mahali,

yakiwaangalia waovu na wema.

415:4 Za 5:9; Mit 10:11; 12:18Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima,

bali ulimi udanganyao huponda roho.

5Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake,

bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara.

615:6 Mit 8:21; 10:16Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa,

bali mapato ya waovu huwaletea taabu.

715:7 Mit 15:2; 10:13Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa,

bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.

815:8 Isa 61:8; Yer 6:20; Ay 35:13; Yn 9:31; Amo 5:22Bwana huchukia sana dhabihu za waovu,

bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.

915:9 Kum 7:13; 1Tim 6:11; Isa 51:1-7Bwana huchukia sana njia ya waovu,

bali huwapenda wale wafuatao haki.

1015:10 Mit 15:13; 17:22Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia;

yeye achukiaye maonyo atakufa.

1115:11 Ay 26:6; Za 139:8; Isa 2:3; Yn 2:24; Ufu 2:23Mauti15:11 Yaani Sheol, maana yake ni Kuzimu. na Uharibifu15:11 Kwa Kiebrania ni Abadon. viko wazi mbele za Bwana:

je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu!

12Mwenye mzaha huchukia maonyo;

hatataka shauri kwa mwenye hekima.

13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke,

bali maumivu ya moyoni huponda roho.

14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa,

bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu.

15Siku zote za wanaoonewa ni za taabu,

bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu.

1615:16 Za 18:17; 1Tim 6:6; Mit 16:8Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana,

kuliko mali nyingi pamoja na ghasia.

1715:17 Mit 17:1; Mhu 4:6Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo

kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki.

1815:18 Mit 14:17; 26:21; Mwa 13:8; Mit 6:16-19; 14:17; Mwa 13:8Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi,

bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi.

1915:19 Mit 22:5Njia ya mvivu imezibwa na miiba,

bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.

2015:20 Mit 10:1Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake,

bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.

2115:21 Mit 2:14; 10:23; Efe 5:15Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili,

bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

2215:22 Mit 16:7; 1Fal 1:12; Mit 24:6; 11:14Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri,

bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa.

2315:23 Mit 12:14; 25:11Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa:

je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake!

2415:24 Flp 3:20; 3:20Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima

kumwepusha asiende chini kaburini.

2515:25 Mit 12:7; Kum 19:14; Za 68:5-6; Kum 19:14; Mit 23:10-11Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi,

bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

2615:26 Za 59:7Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu,

bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye.

2715:27 Za 15:5; Isa 1:23; Yos 6:18; Zek 5:3; Za 94:11; Mit 6:16; Za 18:27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu,

bali yeye achukiaye rushwa ataishi.

2815:28 1Pet 3:15; Mit 14:8Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake,

bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya.

2915:29 Isa 59:2; Efe 2:12; Yn 9:21; Rum 8:26Bwana yuko mbali na waovu,

bali husikia maombi ya wenye haki.

3015:30 Mit 25:25Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni,

nazo habari njema huipa mifupa afya.

3115:31 Mit 9:7-9; 12:1Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima

atakuwa miongoni mwa wenye hekima.

3215:32 Mit 1:7; 12:1; Mhu 7:5Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe,

bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu.

3315:33 Mit 29:23; Isa 66:2Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima,

nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.