114:1 Rut 3:11; Mit 24:3Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
214:2 Ay 12:4Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.
314:3 Mit 12:6; 10:13Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake.
414:4 Za 12:2; Mit 12:17Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.
514:5 Kut 20:16; Za 12:2; Mit 6:19Shahidi mwaminifu hadanganyi,
bali shahidi wa uongo humimina uongo.
614:6 Mit 9:9; 17:24Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.
7Kaa mbali na mtu mpumbavu,
kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.
814:8 Lk 12:20; 1Kor 3:19; Mit 15:28; 21:29Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,
bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
914:9 Mit 1:22; 10:23Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi,
bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.
10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,
wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake.
1114:11 Za 72:7; Ay 8:15; Mit 3:33Nyumba ya mwovu itaangamizwa,
bali hema la mnyofu litastawi.
1214:12 Rum 6:21; Mit 12:15; 16:25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
bali mwisho wake huelekeza mautini.
1314:13 Mhu 2:2; 7:3-6Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,
nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
1414:14 2Nya 15:7; Mit 12:14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao,
naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.
1514:15 Mit 14:8Mtu mjinga huamini kila kitu,
bali mwenye busara hufikiria hatua zake.
1614:16 Kut 20:20; Mit 22:3Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya,
bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.
1714:17 Mit 28:25; 29:22Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,
naye mtu wa hila huchukiwa.
18Mjinga hurithi upumbavu,
bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.
1914:19 Mit 11:29Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,
nao waovu kwenye malango ya wenye haki.
2014:20 Mit 19:4, 7Maskini huepukwa hata na majirani zao,
bali matajiri wana marafiki wengi.
2114:21 Mit 11:12; 19:17; Za 41:1Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,
bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.
2214:22 Mit 4:16-17Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?
Bali wale wanaopanga kilicho chema
hupata upendo na uaminifu.
23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,
bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.
2414:24 Mit 14:8Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,
bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.
2514:25 Mit 12:17Shahidi wa kweli huokoa maisha,
bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.
2614:26 Mit 19:23; Isa 33:6Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,
na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
2714:27 Za 18:5; Mit 13:14Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
2814:28 2Sam 19:7Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme,
bali pasipo watu mkuu huangamia.
2914:29 Mhu 7:8-9; Mit 15:18; Yak 1:19Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,
bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.
3014:30 Ay 5:2; Mdo 7:9; Mit 12:4Moyo wenye amani huupa mwili uzima,
bali wivu huozesha mifupa.
3114:31 Ay 31:15-16; Mit 17:5Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao,
bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.
3214:32 Za 34:21; Mit 6:15; Ay 13:15; 2Tim 4:18Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu,
bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio.
3314:33 Mit 2:6-10Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu
bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.
3414:34 Mit 11:11Haki huinua taifa,
bali dhambi ni aibu kwa watu wote.
3514:35 Es 8:2; Mt 25:14-30Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima,
bali ghadhabu yake humwangukia
mtumishi mwenye kuaibisha.